Apigiliwa msalabani kwa tuhuma za kuiba baiskeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Apigiliwa msalabani kwa tuhuma za kuiba baiskeli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Balantanda, Feb 21, 2009.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  MKAZI wa Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam, amenusurika kufa baada ya kupigiliwa na misumari kwenye msalaba na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, kwa tuhuma za kuiba baiskeli.


  Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana maeneo ya Manzese Uzuri baada ya kijana huyo kukutwa na baiskeli iliyodaiwa kuwa ya wizi.


  Wakazi wa eneo hilo walimkamata na kisha kutengeneza msalaba na kumtundika juu kwa kumpigilia misumari ya nchi sita kisha kumwacha hapo.


  Baadaye wasamaria wema waliopita katika eneo hilo walimwona wakautoa ubao mmoja na kisha kijana huyo akaenda kujisalimisha katika kituo cha polisi akiwa na ubao wa mikononi ambako alipigiliwa mishumari.


  Polisi wa kituo hicho wakamkimbiza katika Hospitali ya Mwananyamala akiwa kwenye msalaba huo kwa ajili matibabu.


  "Sijawahi kuiona katika maisha yangu, wananchi kweli wamekuwa wanyama," alisema mfanyakazi mmoja wa hospitali hiyo mara baada ya kumpokea mtu huyo aliyeletwa na polisi hospitalini hapo mapema asubuhi jana.


  Akisimulia mkasa huo baada ya kumhudumia kwa kumtoa misumari iliyokuwa imepigiliwa mikononi na mabegani; mtumishi wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema: 'Baadhi misumari iliingia katika mifupa ya mikono na kumuumiza vibaya."


  "Ameumia sana na kuna mifupa ambayo imevunjika baada ya kutobolewa na misumari hiyo mikubwa, lakini ana bahati hajafa," alisema mtumishi huyo.


  Imeelezwa kuwa kijana huyo mara baada ya kukutwa na baiskeli hiyo, wananchi walimkamata na kumsulubu kwa kutengeneza msalaba na baadaye kumpigilia kwenye msalaba na kumwacha akiwa ananingÂ’inia.


  Baadaye walipita wasamaria wema walioamua kumsaidia kwa kuondoa ubao mkubwa uliokatisha mgongoni na hivyo yeye kujisalimisha polisi huku ubao uliopigiliwa mikono ukiwa bado mwilini mwake.


  Polisi walimchukua na kumpeleka hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu na hakufunguliwa mashtaka yoyote kwani hakukuwa na mtu aliyelalamika kuibiwa.


  Baada ya kufikishwa hospitalini hapo kijana huyo alikuwa kivutio kwa wagonjwa na ndugu waliowatembelea pamoja na baadhi ya watumishi waliokuwa hapo.


  Wengine kwa kushangazwa ama kuvutiwa na kitendo hicho waliamua kupiga picha kwa kutumia simu zao ambazo zilimwonyesha kijana huyo akiwa katika maumivu makali.


  Baada ya hapo wahudumu wa hospitali hiyo walimchukua na kumtoa misumari hiyo na kumpatia matibabu.
  Source: Gazeti la Mwananchi.
   
 2. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hivi unyama huu Tanzania utaisha lini jamani?????????,mamlaka haziyaoni matukio haya yanayozidi kuongezeka kila kukicha???,inasikitisha kwa kweli
   
 3. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kaka, mbona huzungumzii unyama wanaoufanya wezi kwa raia. Maana nao wanapokuja wanakuwa full armed ama zako ama zao japo ni maliyako. Kunajamaa yangu alikuwa eneo la tukio akanipigia simu yaliyojiri bongo. Kwakuwa hao wahusika wameshindwa kuwa nasuruhisho endelevu la kupambana na wezi ikiwa ni pamoja na kuwaadhibu vilivyo wakifikishwa polisi. Binafsi sina huruma nao kabisa kwa kuwa nshashuhudia unyama mwingi wanaoufanya kwa ndugu zetu na wanaendelea kudunda mtaani.
   
Loading...