Apigania Atambulike Kuwa Yeye Ndiye Mtu Mfupi Duniani


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
<table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;"></td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">

Khagendra Thapa Magar ameanza kampeni ya kutaka atambulike kuwa yeye ndiye mtu mfupi kuliko wote duniani</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top">
Mwanaume mwenye urefu wa sentimeta 56 tu toka nchini Nepal ameondoka nchini kwake na kuanza safari za kuzunguka nchi kadhaa akitaka atambulike kuwa yeye ndiye mtu mfupi kuliko wote duniani.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Khagendra Thapa Magar ameanza safari za kutembelea nchi za ulaya kupiga kampeni za kuingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness kuwa yeye ndiye mtu mfupi kuliko wote duniani.

Khagendra alituma maombi yake kwenye ofisi za London nchini Uingereza akitaka aingizwe kwenye rekodi za dunia pindi afikapo umri wa miaka 18 mwezi oktoba mwaka huu.

Hata hivyo, Khagendra amesema kuwa hajapata majibu yoyote toka kwenye ofisi hiyo.

Awali Khagendra alituma maombi yake ya kuingizwa kwenye rekodi za dunia alipokuwa na umri wa miaka 14 lakini maombi yake yalitupiliwa mbali kwasababu hajatimiza umri wa miaka 18 wa kumwezesha ahesabike kama mtu mzima huku ikihofiwa kuwa anaweza kurefuka.

Madaktari nchini Nepal wameshindwa kuelezea sababu zinazomfanya Khagendra awe mfupi kiasi hicho.

"Tunaenda Italia kujaribu kuingiza jina lake kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness " alisema baba yake Rup Bahadur Thapa Magar, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kabla ya kuanza safari toka mjini Katmandu.

Baada ya kutoka nchini Italia ambako watashiriki kwenye shoo moja kwenye Televisheni ya Italia, Khagendra na kambi yake wataamua nchi gani nyingine ya kwenda.

Mamia ya wapenzi wa Khagendra walijitokeza jana kumuaga na kumkabidhi mashada ya maua.

Hivi sasa He Pingping wa nchini China, ndiye anayeshikilia rekodi ya dunia ya mtu mfupi kuliko wote duniani akiwa na urefu wa sentimeta 73.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; text-align: center; width: 491px;">
</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;">
</td></tr></tbody></table>
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,580
Likes
39,002
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,580 39,002 280
Mbona mshikaji huyu ni mrefu kabisa???
Aje huku kwetu akutane na vibusshuti, akienda kwenye msitu wa congo ndio atajuta kujiona kuwa yeye amekithiri kwenye ufupi.
 
M-bongotz

M-bongotz

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Messages
1,734
Likes
44
Points
145
M-bongotz

M-bongotz

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2010
1,734 44 145
Aagh huyu jamaa mbona tall kabisa, wenzake hata wakikalia kiberiti miguu haigusi chini wamenyamaza tu yeye anapiga kelele.
 

Forum statistics

Threads 1,251,231
Members 481,615
Posts 29,763,626