Mbonea
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 640
- 20
Tuesday, September 29, 2009 4:31 AM
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani amefungua kesi mahakamani akidai fidia ya dola trilioni bilioni 1784 (usishangae tarakimu hazijakosewa) kutoka kwa benki moja nchini humo kwa kumuonyesha huduma mbovu. Dalton Chiscolm amefungua kesi mahakamani katika kitongoji cha Manhattan, New York, Marekani akidai fidia ya dola trilioni bilioni 1784 kutoka kwa benki ya Bank of America kwa kushindwa kumpa huduma bora kama mteja wa benki hiyo.
Chicolsom mbali na pesa hizo ameitaka benki hiyo imuingizie kiasi cha dola milioni 200 kwenye akaunti yake siku inayofuatia, limeripori shirika la habari la Reuters.
Jaji wa Manhattan, Denny Chin alisema kwamba hajawahi kuona kesi ya fidia ya kiwango hicho.
"Amelalamika kwamba alipiga simu nyingi sana kwenye tawi la benki hiyo New York na kupewa miongozo ambayo haikuwa sahihi na mfanyakazi mwanamke wa benki hiyo mwenye asili ya Hispania", ilisema taarifa ya jaji.
"Amelalamika kwamba hundi zake zilikataliwa kutokana na kutokamilika kwa taratibu za kibenki kufuatia miongozo aliyopewa na mfanyakazi wa benki hiyo".
Kiasi ambacho Chiscolm anadai kama fidia ni zaidi ya mara 1,000 ya kiasi ambacho dunia nzima iliingiza mwaka 2008 kwa mujibu wa takwimu za benki ya dunia.
Jaji Chin amempa muda Chiscolm hadi oktoba 23 mwaka huu kuelezea vizuri msingi wa madai yake.
Kama atashindwa kujielezea vizuri basi kesi yake itatupiliwa mbali na haitasikilizwa.
Source: Reuters
nifahamishe.com