JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,264
- 5,355
Mahakama ya Mkoa Kusini Pemba Chake Chake imemrudisha rumande Said Hassan Mabrouk maarufu kwa jina la Said King, mkazi wa Mtoni Chake Chake kwa tuhuma za kumlawiti mlemavu wa akili mwenye umri wa miaka 35.
Katika muendelezo wa kesi hiyo iliyosikilizwa Juni 28, 2022 mwendesha mashtaka wa Serikali Ali Amour Makame mbele ya hakimu wa Mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji Muumin Ali Juma, imedaiwa Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa siku ya tarehe 10\05\2022 Majira ya saa 1:30 za asubuhi Mtoni Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, mtuhumiwa alimlawiti mlemavu wa akili jambo ambalo ni kosa kisheria.
Shahidi nambari moja ambaye ni muathirika wa kesi hiyo ya udhalilishaji ameiambia Mahakama kuwa siku ya tarahe 10\05\2022 majira ya saa 1:30 asubuhi mtuhumiwa alimchukuwa kutoka nyumbani kwao (muathirika) na kumpeleka nyumbani kwake (mtuhumiwa) na kumuingiza chumbani kisha kumvua nguo na kumlaza kifudifudi na kumpaka mafuta sehemu yake ya siri ya haja kubwa na kumfanyia kitendo cha udhalilishaji.
“Alikuja kunichukua nyumbani na kunipeleka nyumbani kwake kisha akanitia chumbani na kunivua nguo akanilaza kifudifudi akanipaka mafuta nyuma na kunifanyia kitendo hicho na alipomaliza akanambia nisiseme nyumbani,” alieleza muathirika huyo.
Baada ya ushahidi huo kutolewa ambao uliwaacha watu vinywa wazi hakimu Muumini Ali Juma alighairisha kesi hiyo hadi Julai 12, 2022 itakaposikilizwa tena ushahidi.
Juni 28, 2022 ni mara ya nne kesi hiyo kurindima Mahakamani hapo, ambapo mara ya kwanza kesi hiyo kutajwa ilikuwa ni Mei 23, 2022, Juni 06, 2022 na Juni 14, 2022.
Chanzo: Idawaonline