Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
Apartments za JWTZ, Police na Magereza tumefanikiwa sana. Apartments za walimu wapya kwa majiji makuu kwanza inawezekana. Serikali na CWT waangalie hili 2020.
Shikamoo wakubwa zangu wote. Mimi mdogo wenu nipo mzima sana wa afya. Leo nimekuja na idea hii ambayo nipo tayari kukosolewa.
Serikali pamoja na Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) inayo uwezo wa kujenga apartments za walimu wapya wanaoanza kazi kila makao makuu ya majiji makuu mfano Dar, Arusha, Mwanza, Tanga (baadae iwe kila mkoa kadri budget itakavyoruhusu) ambapo walimu wapya (ama watumishi wapya wa kada zote za umma ambao sio watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama) watakua wanapokezana kila baada ya mwaka mmoja ama miaka miwili wakiwa wanajipanga na maisha aidha ya kupanga ama kujenga nyumba zao binafsi. This is very possible if there's political willingness.
Nimeamua kupendekeza walimu kwa sababu wao ndio watumishi wengi walioajiriwa na serikali kuliko watumishi wa kada zingine kama wauguzi na madaktari.
Ninajua fika hatuwezi kutengeneza apartments za walimu kwa kila shule nchi nzima, ila tunaweza kuwa na apartments kwa ngazi ya makao makuu ya mikoa hususani majiji makuu kwa sasa ambapo baadae itapanuka na kuwa kila mkoa hata katika mikoa ambayo sio majiji makuu kwa walimu wapya tu ama watumishi wa kada zingine za umma (mfano madereva, madaktari, wauguzi) ambao ndio kwanza wanaanza kazi. Familia ikikaa mwaka mmoja ama miwili atahitajika ahame akatafuta pahala kwingine pa kuishi.
Hili ni wazo langu binafsi na nipo tayari kukosolewa. I STAND TO BE CORRECTED.