Apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumtishia kifo Rais Magufuli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
HAMIMU Seif, mkazi wa Mwananyamala Ujiji, Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kumtishia kifo Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Helleni Liwa, Keneth Sekwao, Wakili wa Serikali, aliiambia mahakama kuwa kijana huyo alitishia kumuua rais Machi 10 mwaka huu, alipokuwa katika baa ya Soweto maeneo ya Makumbusho, Jijini Dar es Salaam.

Sekwao ameeleza mahakama kuwa kijana huyo alitamka kuwa amechoshwa na mambo anayofanya rais, na kwamba yupo tayari kujitoa mhanga kwa kujilipua na bomu.

Mshitakiwa amekana mashitaka, na mahakama imeweka wazi dhamana yake.

Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo tarehe 14 Aprili mwaka huu.
 
teh teh teh
sasa wakili wa serikali kakosa kesi, mpaka kaanza kuzunguka bar kukamata walevi??

Hivi kodi ya serikali huwa inatumikaje aiseee
sasa huko mahakamani siatasema alikuwa "under influence of alcohol" yaani hakuwa na akili timamu wakati anatamka, sasa mateja yanayoporomosha matusi kwenye vituo vya mabasi mbona hawayakamati?
 
Jamaa akisema alikua kalewa. sjui kesi itaendaje hapo, ngoja wataalamu wa sheria waje
 
Mwenzenu pengine alikuwa na hamu ya kumfuata 'kaka' yake jela. Angalia kwa uzembe mnampeleka kirahiiiiiiiiisi bila gharama.
 
HAMIMU Seif, mkazi wa Mwananyamala Ujiji, Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kumtishia kifo Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Helleni Liwa, Keneth Sekwao, Wakili wa Serikali, aliiambia mahakama kuwa kijana huyo alitishia kumuua rais Machi 10 mwaka huu, alipokuwa katika baa ya Soweto maeneo ya Makumbusho, Jijini Dar es Salaam.

Sekwao ameeleza mahakama kuwa kijana huyo alitamka kuwa amechoshwa na mambo anayofanya rais, na kwamba yupo tayari kujitoa mhanga kwa kujilipua na bomu.

Mshitakiwa amekana mashitaka, na mahakama imeweka wazi dhamana yake.

Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo tarehe 14 Aprili mwaka huu.
Ok alikuwa kwenye baa! Si anajilipua yeye na wala siyo Rais. Anyway, kesi iko mahakamani we need not comment further
 
Haha kuna wanao enda mbali kabisa humu jamii forum kumwita jamaa kama vile anko Mkapa alivyosema jangwani , ndio maana kina Melo wako mahakamani baada ya kulazimishwa kutoa taarifa za wanachama wao
 
sasa huko mahakamani siatasema alikuwa "under influence of alcohol" yaani hakuwa na akili timamu wakati anatamka, sasa mateja yanayoporomosha matusi kwenye vituo vya mabasi mbona hawayakamati?
Kachanganya viroba na "ukawa"..lazima matusi yamtoke!
 
HAMIMU Seif, mkazi wa Mwananyamala Ujiji, Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kumtishia kifo Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Helleni Liwa, Keneth Sekwao, Wakili wa Serikali, aliiambia mahakama kuwa kijana huyo alitishia kumuua rais Machi 10 mwaka huu, alipokuwa katika baa ya Soweto maeneo ya Makumbusho, Jijini Dar es Salaam.

Sekwao ameeleza mahakama kuwa kijana huyo alitamka kuwa amechoshwa na mambo anayofanya rais, na kwamba yupo tayari kujitoa mhanga kwa kujilipua na bomu.

Mshitakiwa amekana mashitaka, na mahakama imeweka wazi dhamana yake.

Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo tarehe 14 Aprili mwaka huu.

Rwanda, China, Russia, Malaysia, Indonesia hapo hakuna kesi...Unatangulizwa kwa GOD chap chap. Watu wa aina hii hapa Tanzania na hasa kwenye mabaa na vijiwe wako wengi sana.Wanatamka maneno hovyo hovyo kwa kisingizio cha uhuru wa habari na kutoa maoni.
 
bongo bwana hawana kazi za kufanya hao kesi gani sasa izo
ww unaona bora Bongo mkashinde Bar kunywa viroba saa za kazi?
Magufuli ndio kiboko yao wakafanye kazi mpaka wanyooke
mambo ya kuuza sembe safari hii hakuna
 
Back
Top Bottom