Aonavyo mtu

kalooo

JF-Expert Member
Jun 14, 2016
271
154
Basi nikaona niulize maana ya hayo yakuwa yana maana gani badae, yeye akanambia yasome vizuri alafu uyaseme kwao maana hayana budi kutokea (habakuki 2~4) basi nikaona kama mnyama simba aliyeinuliwa kwa miguu miwili kisha akafunikwa na manyoya ya ajabu yaliyochafuka na watu baada ya mda wake akawa na moyo wa ubinadamu. Nikauliza hii ina maana gani katika nchi niishiyo,akasema hiyo ni 2005~2015.

Ndipo nikamuuliza tena juu ya 2015~2025
Akajibu akasema tazama mwingine kama dubu ameinuliwa upande mmoja na mifupa mitatu ilikuwemo kinywani mwake,nikamuona mnyama huyo akiambiwa inuka ule akawa hawezi basi ikawa hivyo nikauliza upande mmoja na hiyo mifupa mitatu inauhisiano gani yeye akanijibu akasema haya uwe na amani tele maana neno lolote lifananalo na maandiko yangu likubali na usiogope kulisema maana utakuwa umenena ukuu wangu na utukufu wangu juu ya mbigu na ardhi.

Hakunijibu ila nikaona mnyama kama chui akapewa mammlaka na mgongoni mwake ana mabawa manne basi nikamuuliza juu ya hili akasema nawe umeyaona yote hayo huyu ni mtawala atakayetokana na kinywa cha yule dubu ambaye alikaa upande mmoja 2015~2021 ila yeye atachukua pande 3 yaani 2021~2035. Nikasema nahyo mabawa manne akasema cheo hicho amekianza 2015 akiwa na huyo mnyama dubu.

Nikashangaa nikauliza baada ya hapo kuna nini,Kwa haraka akasema usiogope atakuja mnyama mwingine ambaye ni tofauti na wale wote na yeye ana nguvu nyingi,na uwezo mkuu na mavazi yake yanafanana na hayo ya rangi ya utukufu yaani kama kaki ama njano ila ana uso mkali kinywa chake kimejaa mafumbo na uelewa naye ameitawala dunia yote na amestajabisha watu wote.

Nikauliza hiyo nayo inawezekanaje. Akajibu kwa upole watu wangu wameniasi vita vimeongezeka vifo ni vingi sana na njaa na magonjwa yametapakaa na mimi naumia basi huyo ndo mtumishi wangu aliyeapa kwa roho moja kuwa apigane na hayo yote. Nikaguna muh ndo mwisho akasema hapana ila majira yawepo mapya yaani mapenzi yangu na neno langu liwe lenu nyote huyo ndo neno walahi kama alivyokaaa yona tumboni mwa samaki ndivyo na mwanangu atakavyokaa kwenye moyo wanchi yaani sikutatu alafu atafufuka na wote watamuona akipaa mawinguni na hiyo ni utimilifu wa neno lote nililowaandikia yaani ile ahadi kuu.Nasema muwe na majira mapya ya kale yameisha.

Akili yangu ikasema kwa nini mimi jamani,kwa mbali akiniaga akasema waambie wote waisome timothy 1,12~19 inao mashaidi wengi waliosikia kwake na tena huo ndio udhuhirisho wa kristo kama alivyonena isaya katika kitabu changu maneno ya isaya 53. Wengi hawataki kusadiki nanasema mimi Mungu mkuu yote njia zake nimezifanya mimi awe yeye yawe majira yangu mapya.

Kama nilivyosema aminini na niaminini mimi na hao watakaokuja kwenu kwa neno langu niliitwa kwa sauti ya nani asimane kilio chetu kimulilie Mungu na kwa hayo macho yangu na akili yangu nikayajua maana watu wote hasa wakuu warudi kwa Mungu siyo kwa taifa letu Tanzania tu ila dunia nzima.

BASI YOTE HAYO MUNGU ALIYEMKUU ILI IWE FURAHA KWA WATU WOTE NA VIZAZI VYOTE.

Nitasema tena.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom