Radio Producer
JF-Expert Member
- Feb 4, 2011
- 724
- 295
- Thread starter
- #21
katika thread hii kila mtu ana negative review na nyinyi na ukiona kila mtu ana mashaka na wewe jua kabisa there is something kwako it is not right .....
na ukishaanza kupata negative reviews katika stage ya kwanza ya biashara kama hii biashara ambayo mtu anatumia pesa nyingi kuwekeza jua kabisa kuna tatizo
Mkuu hakuna negative review nyuma ya keyboard. Unapokuja na msimamo wa kwamba kuna tatizo naweza kusema labda una ajenda yako mwenyewe kichwani. Kama nawewe unakampuni au biashara inashabihiana na hii basi usitumie nguvu kucrash biashara ya mtu mwingine eti kuna tatizo, ina maana wewe hapo ulipo umefanya kazi namimi na kuona kuna tatizo?
Au kutokuweka fegure kamili kwenye title ndo sababu? Siwezi kukubaliana nawewe kusema tatizo, shida watu wengi wanapenda kuangalia matatizo ya biashara za wenzao huku ya kwake hana hata maboresho. Ningekuwa nimekufanyia kazi na kukawa na tatizo ilikuwa rahisi sana kusema hivyo na pia kutoa maoni kuwa sehemu fulani kuna tatizo na sehemu fulani kuna tatizo boresheni hivi. Wewe sijakufanyia kazi, hujafika hata ofisini, hujafanya chochote eti unaanza kusema kuna tatizo bainisha sasa ni tatizo gani, wivu utaua watu na kukaa kuangalia matatizo ya watu.
Umenikumbusha aina ya watu ambayo ilitolewa mfano huu "Kulikuwa na kijana alipata mbwa anayeweza kukimbia juu ya bahari au ziwa na kukamata bata mizinga, siku moja akamchukua rafiki yake kwenda kumuonyesha maajabu ya mbwa wake, walipofika kijana akamruhusu mbwa mbwa akakimbia juu ya maji na kukamata bata mmoja, wakaondoka kurudi nyumbani na yule rafiki yake na kijana alikuwa kimya na hakusema chochote, ikabidi kijana aondoe ukimya na kumuuliza rafiki yake Umeona kipi cha ajabu/tofauti juu ya mbwa wangu? Rafiki yake akamjibu nimegundua HAWEZI KUOGELEA"
Kuna watu ambao kazi yao ni kuangalia negatives tu na inawezekana huwa wanaumia sana wanapoona postives. Ningefurahi ungenipa maoni ya kuboresha na si kudai eti kuna tatizo bila kubainisha. Tunamshukuru Mungu mpaka sasa tuna tender 4.