Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Asante sana mkuu. Unaweza kutupa makadirio ya mtaji wa kuanzisha duka la kawaida la vipodozi na jinsi linavyozalisha? Natanguliza samahani kwa usumbufu lakini

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Kwa maelezo haya nadhani hata ukiwa na milion mbili unaweza kujaza duka! Kwasabu kama mafuta ya african dream yanauzwa elf 30 ukiweka laki mbili hapo inatosha kabisa! Kuna mafuta ya kupata yanauzwa elf kumi maduka ya rejareja manake jumla inaweza isizid elf sana ukiweka laki hapo una mafuta ya kutosha kabisa,
 
Kwa maelezo haya nadhani hata ukiwa na milion mbili unaweza kujaza duka! Kwasabu kama mafuta ya african dream yanauzwa elf 30 ukiweka laki mbili hapo inatosha kabisa! Kuna mafuta ya kupata yanauzwa elf kumi maduka ya rejareja manake jumla inaweza isizid elf sana ukiweka laki hapo una mafuta ya kutosha kabisa,
Kwenye hilo duka lako la vipodozi weka pia heleni, bangiri, mikufu na hata vikuku vya ile inayoitwa ENGLISH GOLD. Mchanganyiko huu unaweza kukutoa pia. Nashauri hivyo kwani wadada wanapenda pia vitu hivyo na kule Kariakoo vimejaa tele.
 
VIPODOZI

Anzisha Biashara ya Vipodozi Kiulaini Kabisa:- Mwanzo huu hapo. Unapotaja biashara ambazo watu huendelea kupiga pesa hata kama uchumi umedorora basi lazima utataja vyakula,Nk kwanza lakini kama ukiambiwa uongeze bidhaa nyingine hapo basi ongezea na vipodozi, hasa vya wakina mama.

American dream bei ya jumla ni 18,000

Mimi Nauza rejareja 25,000
 
Ahsante kwa taarifa inapendeza...

Ila hapo bei zao zipo juu kiasi...
Ukienda kwa wale wanaowauzia hao ndiyo unakuta bei ipo chini zaidi sema wanataka uwe unachukua mzigo mkubwa...
 
VIPODOZI

Anzisha Biashara ya Vipodozi Kiulaini Kabisa:- Mwanzo huu hapo. Unapotaja biashara ambazo watu huendelea kupiga pesa hata kama uchumi umedorora basi lazima utataja vyakula,Nk kwanza lakini kama ukiambiwa uongeze bidhaa nyingine hapo basi ongezea na vipodozi, hasa vya wakina mama.

Mwanamke lazima asuke, apake mafuta na ajipulizie perfyumu ndio atajiona yupo tayali kutoka kwenda ibadani, kazini, kutembea au hata kujibrand tu. Hivyo basi mahitaji ya vipodozi siku zote yapo juu na ukianzisha biashara hii ukiwa na malengo, uvumilivu na displini basi itakutoa na mchakato wake ni mwepesi kabisa. Endelea kusoma.

Ukifika Bigbon ya Kariakoo kama unatokea fire, vuka barabara, hayo majengo ya mbele yako ukiyazunguka au ukiingia ndani kupitia uchochoro wowote unatokea kwenye himaya ya vipodozi. Ingia kwenye hilohilo jengo la mbele yako. Eneo hilo zamani yalikuwa yanapaki madaladala ya kwenda Sinza na Ubungo na sasa hivi kuna kituo cha mwendo kasi pia.

Kwa kulia kuna mtaa wa Mafia ukishuka nao pia utaanza kukutana na maduka ya vipodozi. Kwa kushoto kuna barabara ya (Pemba) na Jangwani pia hayo ni maeneo ya vipodozi na nywele

Lakini sio tu nywele dizaini zote na vipodozi utavikuta hapa kwa bei ya jumla na rejareja lakini mazagazaga yote ya urembo utayakuta hapa, lipstick, rangi za kucha, perfyume, body freshener, mafuta ya lotion, ya mgando, ya nywele, scrub na kila kitu kinachohusiana na urembo na mambo ya saluni za wanawake.

Kama unamtaji wako na unandoto ya kuanzisha biashara ya vipodozi basi kabla hujafikiria kwenda china au dubai au Zambia anzia hapa. Kupata nywele za Brazilian sio lazima uende Brazil, utazitkuta hapa pia.

Ukiwa na pesa ya mtaji mdogo tu wa kawaida unaweza kufunga mzigo wa maana tu na kurudi nao kwenu kufungua biashara ya ndoto zako sababu hapa yamejaa maduka yanayouza jumla na rejareja. Kama umenunua nywele au mafuta mtaani kwako kuna uwezekanao mkubwa nywele au mafuta hayo yamenunuliwa hapa na muuzaji mwingine wa duka la jumla ambae kamuuzia aliyekuuzia wewe.

Kuuliza bei na ku bargain ni kitu muhimu sana hapa, usinunue vitu kwenye duka la kwanza utakalokutana nalo, utatakiwa uwe mjasiri wa kuuliza bei na kuondoka bila aibu ukiwa mkavu kabisa na kuuliza duka linalofuatia na linalofuatia. Usiishie kwenye maduka ya nje ingia na frame za ndani uone na kuuliza. Mfano, Mafuta ya American dream ambayo mitaani yanauzwa elfu 40 na zaidi kwenye hili soko la vipodozi yanaazia elfu 25, ingawa maduka mengi watakuambia elfu 30.

Hii inamaanisha kuwa kuna wenye maduka hapo wanauza jumla nao wananunua kwa wenzao hapohapo wanaongeza cha juu kidogo na wao pia wanauza kwa bei ya jumla. Mfano nywele zinaitwa coco ambazo mtaani huuzwa 1,500 humo utazikuta kwa 800 mpaka 1,350, na cha kufurahisha zaidi wadada wanaokimbia gharama za kusuka saluni za mitaani huenda kusukia hapo hapo. Ndio, wasusi ni wengi sana pia mitaa hiyo, unanunua nywele kwa bei ya jumla na kusukwa hapo hapo.

Kukupa uhakika kuwa hauingii chaka utaona kwenye maduka makubwa kuna mafurushi mengi na makubwa ya mizigo ya vipodozi inayonunuliwa na kufungwa kwenye mabox na viroba kwa ajili ya kutuma mikoani na maeneo mengine ya mji wa Dar. Kwahiyo wakati wewe utabaki unajiuliza maswali ninunue au nisinunue utaona wenzio wanafungasha na kupeleka kwenye malori.

Wauzaji wa hapa wanapataje hivyo vipodozi na nywele? Kwa mfanya biashara mdogo usijipe hii presha subiri mpaka ukue kwanza lakini kwa mfanyabiashara mkubwa ni kua kuna wachina wana magodown ambapo unatakiwa uweze kuchukua kiwango kikubwa sana kwa wakati mmoja..
Si ndo yale maduka yaliyoko karibu na kituo cha msimbazi kulia?
 
Vipodozi gani pendwa kwa wadada wa mjini..ambavyo havitakiwi kukosa..je mkorogo vipi?

#MaendeleoHayanaChama
 
Vipodozi gani pendwa kwa wadada wa mjini..ambavyo havitakiwi kukosa..je mkorogo vipi?

#MaendeleoHayanaChama

Usoni ni bomba zaidi

Anza na cleanser sina soko ni brand gani ipo juu kwa wakati huo

Scrub pia angalia Zile zinazotrend

Fuata toner chagua Zile top ten

Kisha serum. Angalia pia zinazouzwa zaidi kwenye page za watu

Oil/lotion/cream pia zingatia zinazotrend na zenye matokeo kwa ajili ya wateja wa kudumu

Sabuni pia angalia zinazotrend kwa wakati huo na zenye matokeo

FC_20211127_0063.jpg



FC_20211127_0062.jpg

431D945C-4680-413F-AE57-75A0E102C72C.jpg

B546FC30-EF80-4EED-AF91-6F295E5EF5CB.jpg

7269c491-f454-4aa5-87c1-9ec7fea14527.jpg

IMG_2698.jpg

dbb27400-f8e4-41e7-83b9-2391b4423faa.jpg

313ac8c3-0935-45e1-8372-cbc8e8101751.jpg

da54b19a-5661-4768-aea1-a697fac134b5.jpg
 
Asante mkuu
,hivi ni vigezo gani inatakiwa utimize ndo umiliki biashara hiyo ukiachana na TRA,na inatakiwa angalau uwe na mtaji(kianzio) kama sh ngapi?

maana Huku nilipo kuna fursa fursa,moja wapo hiyo.

Vigezo ni
Leseni
Tin number
Kibali cha TFDA


Mtaji inategemea na layout ya Duka lako unataka lionekane vipi
Maximum ukiwa na Milion 5
But hata ukiwa na Milion 3 kwa kuanzia sio mbaya.
 
Back
Top Bottom