Anzisha biashara ya vipodozi jua wapi pa kupata mzigo Kariakoo

Charles avb

Member
Apr 28, 2020
22
75
VIPODOZI

Anzisha Biashara ya Vipodozi Kiulaini Kabisa:- Mwanzo huu hapo. Unapotaja biashara ambazo watu huendelea kupiga pesa hata kama uchumi umedorora basi lazima utataja vyakula,Nk kwanza lakini kama ukiambiwa uongeze bidhaa nyingine hapo basi ongezea na vipodozi, hasa vya wakina mama.

Mwanamke lazima asuke, apake mafuta na ajipulizie perfyumu ndio atajiona yupo tayali kutoka kwenda ibadani, kazini, kutembea au hata kujibrand tu. Hivyo basi mahitaji ya vipodozi siku zote yapo juu na ukianzisha biashara hii ukiwa na malengo, uvumilivu na displini basi itakutoa na mchakato wake ni mwepesi kabisa. Endelea kusoma.

Ukifika Bigbon ya Kariakoo kama unatokea fire, vuka barabara, hayo majengo ya mbele yako ukiyazunguka au ukiingia ndani kupitia uchochoro wowote unatokea kwenye himaya ya vipodozi. Ingia kwenye hilohilo jengo la mbele yako. Eneo hilo zamani yalikuwa yanapaki madaladala ya kwenda Sinza na Ubungo na sasa hivi kuna kituo cha mwendo kasi pia.

Kwa kulia kuna mtaa wa Mafia ukishuka nao pia utaanza kukutana na maduka ya vipodozi. Kwa kushoto kuna barabara ya (Pemba) na Jangwani pia hayo ni maeneo ya vipodozi na nywele

Lakini sio tu nywele dizaini zote na vipodozi utavikuta hapa kwa bei ya jumla na rejareja lakini mazagazaga yote ya urembo utayakuta hapa, lipstick, rangi za kucha, perfyume, body freshener, mafuta ya lotion, ya mgando, ya nywele, scrub na kila kitu kinachohusiana na urembo na mambo ya saluni za wanawake.

Kama unamtaji wako na unandoto ya kuanzisha biashara ya vipodozi basi kabla hujafikiria kwenda china au dubai au Zambia anzia hapa. Kupata nywele za Brazilian sio lazima uende Brazil, utazitkuta hapa pia.

Ukiwa na pesa ya mtaji mdogo tu wa kawaida unaweza kufunga mzigo wa maana tu na kurudi nao kwenu kufungua biashara ya ndoto zako sababu hapa yamejaa maduka yanayouza jumla na rejareja. Kama umenunua nywele au mafuta mtaani kwako kuna uwezekanao mkubwa nywele au mafuta hayo yamenunuliwa hapa na muuzaji mwingine wa duka la jumla ambae kamuuzia aliyekuuzia wewe.

Kuuliza bei na ku bargain ni kitu muhimu sana hapa, usinunue vitu kwenye duka la kwanza utakalokutana nalo, utatakiwa uwe mjasiri wa kuuliza bei na kuondoka bila aibu ukiwa mkavu kabisa na kuuliza duka linalofuatia na linalofuatia. Usiishie kwenye maduka ya nje ingia na frame za ndani uone na kuuliza. Mfano, Mafuta ya American dream ambayo mitaani yanauzwa elfu 40 na zaidi kwenye hili soko la vipodozi yanaazia elfu 25, ingawa maduka mengi watakuambia elfu 30.

Hii inamaanisha kuwa kuna wenye maduka hapo wanauza jumla nao wananunua kwa wenzao hapohapo wanaongeza cha juu kidogo na wao pia wanauza kwa bei ya jumla. Mfano nywele zinaitwa coco ambazo mtaani huuzwa 1,500 humo utazikuta kwa 800 mpaka 1,350, na cha kufurahisha zaidi wadada wanaokimbia gharama za kusuka saluni za mitaani huenda kusukia hapo hapo. Ndio, wasusi ni wengi sana pia mitaa hiyo, unanunua nywele kwa bei ya jumla na kusukwa hapo hapo.

Kukupa uhakika kuwa hauingii chaka utaona kwenye maduka makubwa kuna mafurushi mengi na makubwa ya mizigo ya vipodozi inayonunuliwa na kufungwa kwenye mabox na viroba kwa ajili ya kutuma mikoani na maeneo mengine ya mji wa Dar. Kwahiyo wakati wewe utabaki unajiuliza maswali ninunue au nisinunue utaona wenzio wanafungasha na kupeleka kwenye malori.

Wauzaji wa hapa wanapataje hivyo vipodozi na nywele? Kwa mfanya biashara mdogo usijipe hii presha subiri mpaka ukue kwanza lakini kwa mfanyabiashara mkubwa ni kua kuna wachina wana magodown ambapo unatakiwa uweze kuchukua kiwango kikubwa sana kwa wakati mmoja..
 
sundoka

JF-Expert Member
Oct 9, 2011
1,939
2,000
VIPODOZI

Anzisha Biashara ya Vipodozi Kiulaini Kabisa:- Mwanzo huu hapo. Unapotaja biashara ambazo watu huendelea kupiga pesa hata kama uchumi umedorora basi lazima utataja vyakula,Nk kwanza lakini kama ukiambiwa uongeze bidhaa nyingine hapo basi ongezea na vipodozi, hasa vya wakina mama.
Asante sana mkuu. Unaweza kutupa makadirio ya mtaji wa kuanzisha duka la kawaida la vipodozi na jinsi linavyozalisha? Natanguliza samahani kwa usumbufu lakini
 
Gentlewoman

Senior Member
Aug 13, 2018
188
500
Asante mkuu
,hivi ni vigezo gani inatakiwa utimize ndo umiliki biashara hiyo ukiachana na TRA,na inatakiwa angalau uwe na mtaji(kianzio) kama sh ngapi?

maana Huku nilipo kuna fursa fursa,moja wapo hiyo.
 
Msweet

JF-Expert Member
Mar 26, 2014
2,459
2,000
Changamoto kubwa .... kuna vipodozi feki vingi sana ambavyo vipo mtaani ....
 
careenjibebe

JF-Expert Member
May 28, 2020
1,495
2,000
VIPODOZI

Anzisha Biashara ya Vipodozi Kiulaini Kabisa:- Mwanzo huu hapo. Unapotaja biashara ambazo watu huendelea kupiga pesa hata kama uchumi umedorora basi lazima utataja vyakula,Nk kwanza lakini kama ukiambiwa uongeze bidhaa nyingine hapo basi ongezea na vipodozi, hasa vya wakina mama.
Nilikua natafuta sana hilu chimbo!! Asante sana umemaliza kila kitu
 
careenjibebe

JF-Expert Member
May 28, 2020
1,495
2,000
Asante sana mkuu. Unaweza kutupa makadirio ya mtaji wa kuanzisha duka la kawaida la vipodozi na jinsi linavyozalisha? Natanguliza samahani kwa usumbufu lakini

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Kwa maelezo haya nadhani hata ukiwa na milion mbili unaweza kujaza duka! Kwasabu kama mafuta ya african dream yanauzwa elf 30 ukiweka laki mbili hapo inatosha kabisa! Kuna mafuta ya kupata yanauzwa elf kumi maduka ya rejareja manake jumla inaweza isizid elf sana ukiweka laki hapo una mafuta ya kutosha kabisa,
 
CHIEF MASALAKULANGWA

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
593
500
Kwa maelezo haya nadhani hata ukiwa na milion mbili unaweza kujaza duka! Kwasabu kama mafuta ya african dream yanauzwa elf 30 ukiweka laki mbili hapo inatosha kabisa! Kuna mafuta ya kupata yanauzwa elf kumi maduka ya rejareja manake jumla inaweza isizid elf sana ukiweka laki hapo una mafuta ya kutosha kabisa,
Kwenye hilo duka lako la vipodozi weka pia heleni, bangiri, mikufu na hata vikuku vya ile inayoitwa ENGLISH GOLD. Mchangiko huu unaweza kukutoa pia. Nashauri hivyo kwani wadada wanapenda pia vitu hivyo na kule Kariakoo vimejaa tele.
 
Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
23,932
2,000
VIPODOZI

Anzisha Biashara ya Vipodozi Kiulaini Kabisa:- Mwanzo huu hapo. Unapotaja biashara ambazo watu huendelea kupiga pesa hata kama uchumi umedorora basi lazima utataja vyakula,Nk kwanza lakini kama ukiambiwa uongeze bidhaa nyingine hapo basi ongezea na vipodozi, hasa vya wakina mama.

American dream bei ya jumla ni 18,000

Mimi Nauza rejareja 25,000
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
70,131
2,000
Ahsante kwa taarifa inapendeza...

Ila hapo bei zao zipo juu kiasi...
Ukienda kwa wale wanaowauzia hao ndiyo unakuta bei ipo chini zaidi sema wanataka uwe unachukua mzigo mkubwa...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom