Anzia hapa Ili kujenga mafanikio makubwa kupitia uwekezaji kwenye viwanja na majengo

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Kila eneo kwenye maisha hutegemea sana kitu hiki ili uweze kujenga mafanikio makubwa sana na ya kudumu.

Kitu chenyewe ni mtazamo wako. Huu ndio msingi wa kujenga mafanikio makubwa kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Ukiwa na mtazamo hasi, utakuwa unashindwa kila wakati mpaka ukate tamaa.

Anza kutengeneza mtazamo wa akili yako. Njia mojawapo ya kubadili mtazamo wako ni kujifunza kuhusu uwekezaji wa ardhi na majengo.

Usipokuwa na mtazamo sahihi kuhusu maisha ya mafanikio kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo huwezi kudumu kwenye mafanikio.

Kuwekeza Kwenye Akili Yako Ni Muhimu Kwenye Maeneo Yafuatayo.

1. Kuiongoza timu yako ya uwekezaji kwenye viwanja na nyumba

Ukiwa na timu imara na yenye ufanisi mkubwa unakuwa umejenga nyenzo ya kukusaidia kujenga utajiri kupitia viwanja na nyumba kwa haraka zaidi.

Mwanatimu wa kwanza kuwa naye ni menta au kocha atakayekusaidia kuwekeza bila kufanya makosa ya kujirudia rudia.

Kocha au menta mbobezi kwenye uwekezaji wa viwanja na nyumba atakusaidia katika mambo yafuatayo;-

✓ Kupunguza makosa ya uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

✓ Kuchagua mbinu bora za kuwekeza kwenye viwanja na nyumba.

✓ Kukuongezea maarifa sahihi na uzoefu bila kusahau taarifa sahihi ya uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

✓ Kukufahamisha mbinu mpya na bora za kuwekeza kwenye majengo uliyobobea kuwekeza.

✓ Utamshirikisha kila kitu kuhusu uwekezaji wa viwanja na nyumba.

✓ Atakuwa ni rafiki yako wa karibu sana kuhusu uwekezaji wa viwanja na nyumba.

Karibu ujiunge na kundi la UWEKEZAJI MAJENGO ili niwe menta au kocha wako niliyebobea kwenye uwekezaji wa viwanja na nyumba.

2. Kuchagua nyumba za kupangisha zenye kipato kikubwa

Kuna aina kuu tatu (3) za majengo. Nazo ni kama ifuatavyo:

✓ Majengo ya biashara. Haya hujumuisha majengo ya viwanda, majengo ya ofisi, majengo ya stoo au bohari, majengo ya fremu za biashara na apatimenti kubwa.

✓ Majengo ya familia au majengo ya makazi. Haya hujumuisha majengo ya familia moja, familia mbili, familia tatu, familia nne na familia nyingi.

✓ Majengo ya matumizi maalumu. Haya hujumuisha majengo ya shule na vyuo, majengo ya vituo vyote za afya, majengo ya vituo vya elimu kwa ujumla, majengo ya kuhifadhi wazee, majengo ya walemavu, majengo ya wenye magonjwa akili (psychiatric patients), na kadhalika.

3. Kufanya tathimini ya hali ya soko mahalia

Hali ya soko mahalia ndiyo unayoamua kiasi cha faida au kipato endelevu unachoweza kutengeneza kutoka kwenye nyumba au kijwanja husika.

Haiwezekani kutengeneza fedha kwenye hali mbaya ya soko mahalia isipokuwa kwa kutumia njia zifuatazo;-

✓ Kununua kutoka kwa muuzaji aliyehamasika.

✓ Kuuza kwa mnunuzi aliyehamasika.

✓ Kupangisha kwa wapangaji/mpangaji aliyehamasika.

4. Kuchagua njia bora za kupata mitaji fedha

Unaweza kupata mtaji fedha kwa njia zifuatazo;-

✓ Kuingia ubia na jamaa zako.

✓ Kutumia sehemu ya mshahara wako kuanza uwekezaji.

✓ Kutumia sehemu ya faida ya biashara yako kuwekeza kwenye ardhi na majengo.

✓ Kuomba michango kutoka kwa jamaa zako.

✓ Kuomba mkopo kutoka kwenye vikundi mbalimbali, VICOBA, benki za kati na taasisi nyingine za kifedha.

✓ Kufungua kampuni ya uwekezaji kwa kuuza hisa kwa ajili ya kuwekeza.

Njia zote hizi zinaweza kutumika kupata mtaji fedha wa kuwekeza kwenye viwanja na nyumba. Njia zote hizi sio rahisi kuzitumia, kama zingekuwa rahisi kila mtu angeweza kuzitumia. Utahitaji uvumilivu na bidii katika kila njia ya kupata mtaji fedha.

5: Njia za kuongeza thamani ya majengo

Thamani ya nyumba na kiwanja inaweza kuongezeka kaa njia kuu mbili (2). Njia hizo ni kama ifuatavyo;-

✓ Udhibiti binafsi wa msimamizi wa nyumba au kiwanja (forced property appreciation).

✓ Hali ya soko mahalia (market property appreciation).

Njia ya pili ya kuongezeka kwa thamani ya viwanja na nyumba inaathiriwa zaidi na nguvu zifuatazo;-

✓ Nguvu ya kisiasa (political forces). Hii hujumuisha sera za serikali za mitaa na sera za serikali kuu kuhusu mtaa/kata/jimbo/mkoa husika.

✓ Nguvu ya mitindo ya majengo (physical forces). Hapa hujumuisha jinsi majengo yalivyo na ubora na mpangilio mzuri kwenye mtaa husika.

✓ Nguvu ya kijamii (social forces). Hapa hujumuisha idadi ya watu na sababu nyingine za kijamii.

✓ Nguvu ya kiuchumi (economic forces). Hii hujumuisha ukuaji, uimara na usimamiaji wa biashara na uwekezaji kwenye halmashauri husika, mkoa husika na hata nchi husika.

Njia za kuongeza thamani kwa udhibiti binafsi ni njia ambazo wengi huzipuuza na hata kutojua jinsi ya kunufaika nazo. Njia za udhibiti binafsi za kuongeza thamani ya viwanja na nyumba ni kama ifuatavyo;-

✓ Kukarabati na kuboresha nyumba.

✓ Kupanda mazao ya chakula na mazao ya biashara kwenye mashamba.

✓ Kupima kiwanja na kuwa na hati ya hakimiliki ya kiserikali.

✓ Kugawanya kiwanja katika vipande vidogovidogo kulingana na mahitaji ya halmshauri husika.

✓ Kuongeza ukubwa wa mita za mraba za kupangisha.

✓ Kuongeza idadi ya vyumba vya kupangisha.

✓ Kuongeza idadi ya vyoo vya ndani ya vyumba au nyumba.

6: Kuchagua mbinu bora za kuanza kuwekeza kwenye viwanja na nyumba

Kuna mbinu nyingi tofauti tofauti za kuwekeza kwenye viwanja na nyumba. Jinsi unavyofanya mbinu nyingi ndivyo unavyoweza kuchagua mbinu bora sana kwako.

Mbinu ambayo hufaa zaidi kwa walioajiriwa na wenye biashara nyingine ni ile mbinu ya B-R-R-R-R ya majengo ya kupangisha.

Mbinu yoyote inayoingiza kipato endelevu cha kila mwezi inafaa zaidi kwa kujenga utajiri kwa walioajiriwa na wenye biashara tofauti tofauti.

Mbinu nyingine ambazo huweza kutumika kujenga utajiri kwa walioajiriwa au walioajiri ni kama ifuatavyo;-

✓ Kutoa mikopo ya majengo kwa wawekezaji kwenye viwanja na nyumba.

✓ Kumiliki nyumba za wageni mijini.

✓ Kumiliki hosteli za wanafunzi wa sekondari na vyuo.

✓ Kutoa huduma za uwekezaji kwenye viwanja na nyumba kama vile vile udalali, huduma za uwakili, huduma za uhasibu, huduma za ufundi ujenzi, huduma za michoro na ramani za nyumba, huduma za kupima viwanja, huduma za matangazo ya mauzo na masoko ya viwanja na nyumba na kadhalika.

✓ Kumiliki aina yoyote ya majengo ya kupangisha.

7. Kuchagua aina sahihi ya majengo yanayofaa kuwekeza.

Kwa kujifunza utaweza kutambua aina ya majengo ambayo huingiza kiasi kikubwa cha kipato endelevu katika mtaa au jimbo husika.

Kila mtaa, kata, jimbo na hata mkoa una aina chache za majengo ambayo huingiza kiasi kikubwa cha kodi ukilinganisha na aina nyingine ya majengo.

Ukiwa na maarifa sahihi kwenye akili yako na ukashirikiana vizuri na timu yako utaweza kuchagua majengo yanayolipa kiasi kikubwa cha kodi kuliko aina nyingine ya majengo.

Naomba niwe mmoja wa timu yako ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo. Nitakuwa mmoja wa watu muhimu sana kujenga mafanikio makubwa ya kifedha kupitia uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Namba ya WhatsApp; +255 752 413 711
 
*Fursa ya biashara kwa ubia (joint venture)
*
Abraar Bricks Nyumba kwa wote,

Kumejitojeza fursa ya kibiashara ambayo inahitaji active partners wa kuingia nao makubaliano ya kibiashara (joint ventures).

Yeyote kati ya hawa hapa chini wanaokidhi vigezo tuwasiliane;

1) Upo kwenye fani ya ujenzi kwa zaidi ya miaka 5.

2) Civil Engineers or Architects.

3) Mwekezaji kibiashara mwenye mtaji wa kutosha.

Tutaingia ubia na wewe kwa mtaji wako kikazi au mtaji wako kifedha, muhimu uwepo karibu. Hii project ni ya muda mrefu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Abdul Ghafur +255625249605

Sambazia na wengine.
 
*Fursa ya biashara kwa ubia (joint venture)
*
Abraar Bricks Nyumba kwa wote,

Kumejitojeza fursa ya kibiashara ambayo inahitaji active partners wa kuingia nao makubaliano ya kibiashara (joint ventures).

Yeyote kati ya hawa hapa chini wanaokidhi vigezo tuwasiliane;

1) Upo kwenye fani ya ujenzi kwa zaidi ya miaka 5.

2) Civil Engineers or Architects.

3) Mwekezaji kibiashara mwenye mtaji wa kutosha.

Tutaingia ubia na wewe kwa mtaji wako kikazi au mtaji wako kifedha, muhimu uwepo karibu. Hii project ni ya muda mrefu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Abdul Ghafur +255625249605

Sambazia na wengine.
 
Back
Top Bottom