Surya
JF-Expert Member
- Jun 7, 2015
- 8,378
- 12,573
Wana JF mie sina mengi ya kusema ila nina jambo moja tu la kusema kwenu. Ugumu huu wa maisha na kushindwa kwa mipango mbalimbali ambayo tunaipanga na kuifanyia kazi hapa duniani ni majibu tosha kua sisi sio wakamilifu. Mimi sio mkamilifu wewe pia sio mkamilifu.
Tuanze kujitizama sisi wenyewe matendo na tabia zetu. Mawazo na fikra zetu je yapo sahihi wakati wote? Hua tunakosea au hatukosei jambo.
Jambo kubwa ninalopenda kukusisitiza binadamu mwenzangu ni kwamba tujarbu kuzifundisha akili zetu zipate uelewa wa mambo, TUPENDE KUJIFUNZA.
Tupende kuja hapa jukwaa na kufundisha mambo mbali mbali ya kimaisha, huku tukiendelea kutafuta mbinu za kupata pesa huko uliko.
Tutumie utandawazi na teknologia hii ya mawasiliano kama nyenzo ya kujifunzia vitu mbali mbali. Tusipende kuangalia watu wakichekesha vitu visivyo na maudhui yoyote wala tusipende kusikiliza matatizo ya watu pasipo kuchambua kuna maudhui gani.
Tupende kujifunza ili hata mimi Surya wa mwaka huu, nibadilike na kuongeza kitu akilini ili mwaka ujao apatikane Surya mwingine.
Ni hayo tu.