Anyonga mtoto na kujinyonga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anyonga mtoto na kujinyonga

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Mar 21, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Joyce Joliga,Songea


  KATIKA hali ya kusikitisha, mwanaume aliyetambuliwa kuwa ni Mwidadi Hamisi,(32) mkazi wa Bombambili mjini Songea, mkoani Ruvuma, amemnyonga mtoto wake wa umri wa miaka minne na baadaye naye kujinyonga huku akiwa ameacha ujumbe kuwa uamuzi huo umetikana na shida alizokuwa akipata kutoka kwa mke wake wa zamani.


  Tukio hilo lilisikitisha wengi hasa kwa kitendo cha kumnyonga mtoto Mulla, ambaye hakuwa na hatia, lilitokea saa 5:00 asubuhi ya juzi katika maeneo ya Mlima wa Chandamali,nje kidogo wa mji wa Songea.

  Kabla ya kuamua kujinyonga, marehemu ambaye wakati wa uhai wake alikuwa mwendesha pikipiki zinazosafirisha watu,alimpiga simu kwa tajiri wake akimtaka afuate pikipiki yake katika maeneo ya mlimani huo.

  Habari zilisema katika simu hiyo marehemu alimwambia tajiri wake kuwa yeye ameamua kwenda kupumzika kaburini na mtoto wake, ili kuepuka shida alizokuwa akizipata kutoka kwa mke wake wa zamani.

  Kabla ya kujinyonga, Mwadadi, aliacha ujumbe huku akiambatanisha na orodha ya namba za simu za ndugu zake na kutaja sehemu anakotoka kuwa Newala mjini mkoani Mtwara.

  Katika ujumbe huo, marehemu alisema ameamua kujinyonga yeye na mtoto wake kufuatia kashfa alizokuwa akizipata kutoka kwa mama watoto wake.

  Katika ujumbe huyo marehemu alimtuhumu mama huyo kuwa amekuwa akimweleza mpenzi wake, siri za maungoni mwake.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio tajiri wa marehemu huyo,Hussein Msafiri, alisema siku kadhaa zilizopita, marehemu aliwahi kumweleza matatizo yake yeye na mke wa zamani.
  "Mara nyingi alionekana mtu ambaye hana amani moyoni mwake," alisema.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18615
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mhhhhh....
  huzuni sana.....
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  eeeh!! kumbe mtu unaweza kujinyonga eeh
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  niliisoma ile habari nkasisimka mwili mzima................... tumwombe sana Mungu............... watu wamejaa misongo ya mawazo.....................ndiyo matokeo yake...................
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  duh very sad.

  Lakini kwa nini habari hii imewekwa hapa kiwanja cha matangazo madogo2 au mpangilio wa forums umebadilika hapa ndani?.
   
Loading...