Anya sumu ya panya na kisha kumnywesha mwanae | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anya sumu ya panya na kisha kumnywesha mwanae

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbonea, Sep 29, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33


  Tuesday, September 29, 2009 10:14 AM
  MWANAMKE mmoja amefariki dunia Jijini Dar es Salaam baada ya kunywa sumu ya panya ambapo ilidaiwa pia kumnywesha mwanae aliyekuwa na umri wa miaka sita. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile amesema, tukio hilo la kuhuzunisha lilitokea jana mishale ya saa 8:00 mchana huko Ilala Mchikichini.

  Amesema mwanamke huyo aliyekuwa akitambulika kwa jina Samia Mwambata [36] mkazi Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam.

  Kamanda Shilogile amesema kuwa, mwanamke huyo alikunywa sumu hiyo ya panya Septemba 26 mwaka huu, na kisha akamnywesha mwanae aitwaye Leice Gerard [ 6] kwa nia ya kumuua.

  Amesema baada ya tukio hilo mwanamke huyo na mwanae walikimbizwa katika hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu.

  Hata hivyo amesema ilipofika jana mishale ya saa 8:00 mchana, mwanamke huyo alifariki dunia.

  Amesema mtoto Leice alitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani siku hiyo hiyo aliyonyweshwa sumu na mama yake huyo na kuponyeka.

  Kamanda Shilogile amesema chanzo cha kifo kifo hicho ni kutokana na mwanamke huyo kuambiwa na ndugu zake kuwa ana tabia mbaya na ndipo alipoamua afe pamoja na mwanae.

  Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Amana na Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
  Na Pilly Kigome, Dar
   
Loading...