Anusurika Kwenye Ajali, Afariki Kanisani Akimshukuru Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anusurika Kwenye Ajali, Afariki Kanisani Akimshukuru Mungu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 12, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Friday, September 11, 2009 4:53 AM
  Jamaa mmoja wa nchini Austria alipiga dua zote alizozijua wakati aliponasa kwenye lifti na baada ya kuokolewa alikimbilia moja kwa moja kanisani kumshukuru mungu na kuangukiwa na sanamu na kufariki. Gunther Link, muumini mkubwa wa kanisa katoliki alipiga dua zote alizokuwa akizijua kumuomba mungu amuokoe baada ya kunasa kwenye lifti kwenye jengo moja la ghorofa katika jiji la Vienna, Austria.

  Link mwenye umri wa miaka 45, alikimbilia moja kwa moja kanisani baada ya kuokolewa ili amshukuru mungu kwa kumuokoa.

  Akiwa kwenye kanisa hilo, Link aliangukiwa na sanamu la kihistoria la yesu lililotengenezwa kwa mawe lililokuwa na uzito wa kilo 390 na alifariki papo hapo.

  Roman Hahslinger, msemaji wa polisi wa AVienna alisema: " Link alikuwa ni mtu wa dini sana na alihofia sana maisha yake baada ya kunasa ndani ya lift. aliomba dua sana kwa mungu amuokoe".

  "Muda mfupi baada ya kuokolewa kutoka kwenye lift hiyo, alienda moja kwa moja kanisani kumshukuru mungu".

  "Inaonekana kama aliiegemea na kuitingisha nguzo ambayo sanamu hilo lilikuwepo na ndipo lilipomdondokea. Alifariki papo hapo".

  "Tumezigundua alama za vidole kwenye nguzo na tunalifanyia uchunguzi zaidi suala hili" alisema msemaji huyo wa polisi.

  Mwili wa Link uligunduliwa siku iliyofuatia na waumini walioenda kanisani kusali huku ndugu zake wakiwa wametoa ripoti polisi kupotea kwa ndugu yao.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3055882&&Cat=2
   
 2. m

  mtanzaniaraia Member

  #2
  Sep 12, 2009
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani huko hayuko mungu wa kweli!Mungu wa kweli ni lazima angemwokoa!ahaaa,ahaa,ahaa.Tokeni huko mnaona wenyewe bado mnang'ang'ania uraia wa roma.
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hii habari ya uongo!duh! walijuaje haya yote kama mtu amekufa?
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Wale wanaounguaga moto pale kwenye Nyumba ya Mungu kwenye jiwe jeusi, mbona uwashauri watoke huko
   
Loading...