Antony Sanga: Mwaka 2025, lazima huduma ya maji iwe imefika mijini kwa asilimia 95

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Katibu mkuu Wizara ya maji Anthony Sanga imezitaka Mamlaka za maji nchini kuhakikisha ifikapo 2025 lazima huduma ya maji iwe imefika mijini kwa asilimia 95 na vijijini kwa asilimia 85 kutokana na ongezeko la mahitaji ya maji litakalo kuwepo kwa mwaka huo.

Ameyasema hayo Jijini dar es salaam Wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa Mamlaka za maji Safi na usafi wa mazingira kwa mwaka wa fedha 2020-2021 ambapo ripoti hiyo yenye miongozi mbalimbali iliyoandaliwa na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji -EWURA na Wizara ya maji.

Aidha amesema changamoto ya upotevu wa maji unaochangia upotevu wa maduhuli imekuwa ikizungumzwa kwa kipindi kirefu huku Mamlaka zikishindwa kudhibiti suala hilo, hivyo miongozi iliyoandaliwa na EWURA itasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto hiyo na zingine ili kuimarisha utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi na kufikia malengo ya Maendeleo endelevu.

Mbali na hayo pia amezitaka mamlaka za maji nchini kuhakikisha zinajitathmini na kuongeza juhudi Katika kutoa huduma za maji ikiwa ni pamoja na kutekeleza maelekezo yaliyolenga kuimarisha sekta ya maji yanayotolewa na viongozi nchini.

Kaimu MwenyeKiti wa bodi ya wakurugenzi EWURA Fadhil Manongi, Ameeleza kwamba EWURA imetoa kiasi cha shilingi Milioni 150 ili Mamlaka zilizofanya vizuri zitumie fedha hizo kuziungia maji taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo shule za msingi na sekondari pamoja na zahanati zinazonufaika na fedha za uviko 19.
 
tukiwanyima wabunge posho na mikopo ya magari na gratuity tuu hapo naamini huduma ya maji itafika kwa walengwa vijijini ila wakibaki wanalipwa subiri mpaka nguruwe ajue kuruka kama ndege ndipo maji yawe kinwaji cha anasa vijijini! unajua yule mtoto Khamisi wa kule mtwara alipokufa kwa ajili ya kugongwa na nyoka akitafuta maji mtoni , na yule msichana pale kilombero alizamishwa majini mtoni na mamba mpaka mwanae alikufa nilidhania hali hii ya kusikitisha ingeleta opereshi maji ya bomba vijijini kote lakini KUMBE NI Yahwe NAKOMITUNANKHA!
 
Katibu mkuu Wizara ya maji Anthony Sanga imezitaka Mamlaka za maji nchini kuhakikisha ifikapo 2025 lazima huduma ya maji iwe imefika mijini kwa asilimia 95 na vijijini kwa asilimia 85 kutokana na ongezeko la mahitaji ya maji litakalo kuwepo kwa mwaka huo.

Ameyasema hayo Jijini dar es salaam Wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa Mamlaka za maji Safi na usafi wa mazingira kwa mwaka wa fedha 2020-2021 ambapo ripoti hiyo yenye miongozi mbalimbali iliyoandaliwa na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji -EWURA na Wizara ya maji.

Aidha amesema changamoto ya upotevu wa maji unaochangia upotevu wa maduhuli imekuwa ikizungumzwa kwa kipindi kirefu huku Mamlaka zikishindwa kudhibiti suala hilo, hivyo miongozi iliyoandaliwa na EWURA itasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto hiyo na zingine ili kuimarisha utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi na kufikia malengo ya Maendeleo endelevu.

Mbali na hayo pia amezitaka mamlaka za maji nchini kuhakikisha zinajitathmini na kuongeza juhudi Katika kutoa huduma za maji ikiwa ni pamoja na kutekeleza maelekezo yaliyolenga kuimarisha sekta ya maji yanayotolewa na viongozi nchini.

Kaimu MwenyeKiti wa bodi ya wakurugenzi EWURA Fadhil Manongi, Ameeleza kwamba EWURA imetoa kiasi cha shilingi Milioni 150 ili Mamlaka zilizofanya vizuri zitumie fedha hizo kuziungia maji taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo shule za msingi na sekondari pamoja na zahanati zinazonufaika na fedha za uviko 19.

Uko mradi wa maji pale kimbiji ni mfupa ulio mshinda hata JPM.
 
Blah blah za chama dola,60yrs ya kututawala bado wanatupa siasa siasa za maji taka
 
Back
Top Bottom