voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,552
- 11,883
Kwani walioua Elimu ya nchi hii kitaifa ni akina nani zaidi ya Serikali na mawaziri wake?Bila hata kujua kiwango cha elimu ya mkuu wa mkoa wa Dodoma, mara moja naona makosa ya kiutendaji aliyonayo. Kwanza, yaonekana ni mtu asiyejua kuchagua maneno. Pili, hakujua mchakato upi uboreshe kiwango cha elimu mkoani kwake, siyo ufaulu anaotafuta. Elimu inaendeshwa kitaifa na siyo ki-mkoa.
Haiingii akilini kwamba mkuu wa mkoa anataka kuboresha ufaulu wa wanafunzi kwa kupambana na waziri wa elimu, kwa makambi ya elimu. Ili iweje?
Elimu ni mchakato wa miaka 7 kwa shule za msingi, miaka 4 sekondari, n.k. Kama kuna uzembe ktk miaka ya elimu, Mtaka anawezaje kuboresha uzembe huo kwa makambi ya miezi miwili? Yaani sasa hivi aanze, kufika septemba darasa la 7 wafaulu mtihani. Ni elimu gani hiyo?
Sera ya elimu ipo ili kudhibiti mawazo mfu kama haya ya akina Mtaka.
Muacheni Mtaka ajaribu njia mbadala ili tumpime mafanikio yake.