Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,502
- 22,354
Joshua (kushoto) na Martin
Bondia wa Uingereza wa uzito wa juu Antony Joshua anatarajiwa kupambana na Bondia wa Marekani Charles Martin kugombea uzito wa juu wa IBF mjini London.
Pambano hilo la kukata na shoka limetangazwa na meneja wake bwana Eddie Hearn na litafanyikia kwenye ukumbi maarufu wa 02 Arena uliopo mashariki mwa jiji la London tarehe 9 mwezi April.
Joshua (kushoto) na meneja wake Hearn
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Charles Martin kutetea taji lake hilo analolishikilia baada ya kulitwaa mwezi January alipomtwanga bondia Vyacheslav Glazkov mjini Brooklyn nchini Marekani.
02 Arena ni ukumbi na ngome ya Antony Joshua na amekwishashinda mapambano 5 kati ya 15 alochezea hapo.
Hivyo basi tunasubiri mpambano wa nguvu kati ya wakali hawa kwa sasa hapo tarehe 9 April.
Mwaka jana Antony Joshua alishinda mkanda wa uzito wa juu kwa nchini Uingereza baada ya kumpiga Dillian Whyte.