Antonio Guterres: Kuzuia vyanzo vya uvunjifu wa amani ndiyo dawa ya kudumisha amani

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,792
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa mjini Paris Ufanransa wakati wa ufunguzi wa kongamano la kimataifa la Paris kwa ajili ya Amani jana, amesema kuzuia vyanzo vote vinavyosababisha uvunjifu wa amani duniani ndio dawa mujarabu ya kulinda na kudumisha amani ya dunia kuliko kukabili machafuko wakati yameshatokea.

Ameongeza kuwa ingawa ukilinganisha na migogoro mikubwa ya karne zilizopita hali ya sasa inaonekana kuwa ni ya amani zaidi, lakini ukweli ni kwamba “Bado tuko mbali kuwa na ile tunayoiita amani ya kweli, hali halisi ni ya sintofahamu na changamoto kubwa’’

Katika ulingo wa kimataifa Guterres ametaja hatari tano (5) zinazoikabili dunia hivi sasa akisema:

Mosi, Tunaona hatari ya mgawanyiko wa kiuchumi, kiteknolojia na kijiografia.

Pili, Tunapaswa kuangalia katika ngazi ya kitaifa mgawanyiko wa kijamii na tofauti zilizopo.

Tatu, tunashuhudia wimbi la maandamano kote duniani, na kama kila hali ni tofauti basi amesema kuna mambo mawili ambayo yanashabihiana:

  • Kwanza kabisa tunashuhudia ongezeko la kutoaminiana baina ya raia na taasisi za kisiasa na viongozi, usawa wa kijamii uko katika tishio kubwa.
  • Pili, tunashuhudia athari za utandawazi unaohusiana na maendeleo ya kiteknolojia zikiongeza pengo la usawa katika jamii.
Nne, watu wanataabika sana na wanataka kusikilizwa, wana kiu ya kupata usawa. Wanadai kuwa na mfumo wa kijamii na kiuchumi ambao unafanyakazi kwa maslahi ya wote.

Na tano, wanataka haki zao za binadamu na uhuru wa msingi vitekelezwe na kuzingatiwa kwa wote.
 
Haya makongamano huwa yanaleta tija kweli? Zaidi ya kutimiza wajibu tu kwamba kuna kitu au jitihada wanafanya sioni mchango mkubwa wa hizi kelele zao.

Syria imeendelea kupata shida huku watoto, wazee na wamama wakiendelea kupata mateso na shida.

Tumeona yaliyotokea Iraq na Libya, nchi zimeachwa kwenye hali mbaya zaidi kuliko hata hapo awali zilivyokuwa zikiendesha mambo kwa namna zao.

Tatizo la uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi yanaendelea kuikabili dunia kwa kasi kubwa lakini nikiangalia zaidi ya matamko, makongamano na kubadili kauli mbiu sioni jitihada mathubuti zikichukuliwa kukabiliana na hizi changamoto.

UN chombo kikubwa sana kisicho na makali.

Kuna wakati maneno ya Trump yanaukweli kwamba ni club ya watu wanaoenda kula raha na kuishi maisha ya kifahari.
 
Back
Top Bottom