Antoine Fuqua - Director and Producer [Tears of the Sun, Training Day,The Equalizer Etc

I_manyota

Member
Aug 15, 2012
48
44
Unaikumbuka Tears of the Sun na mtaalam Bruce willis, Cole na wakali wengine vipi kuhusu Olympus has follen 🙂🙂, Equalizer je? haya basi huyu hapa mwamba aliyeproducer na ku direct hyo mizigo.

Antoine Fuqua ni mmoja kati wachache wandaaji wa filamu weusi nchini marekani mwenye heshima zake duniani, haya tushuke taratibuuu tumfahamu huyu jamaa ambae wengi tunapenda movie zake pasipokujua kumbe jamaa ndio master mind wa hiyo mizigo yetu pendwa
2613788_Fuqua-250x375.jpg

Mwamba huyo hapo bhana fundi mwenyewe 😃😃 kipisi cha mtu nini fresh.
Basi kwa fasta fasta tupitie hata kahistoria kake, sio kwamba kadogo nope mbaba ana historia ndefu kidogo kwenye hustle za kutoboa maisha kupitia tasnia hii ya utengenezaji wa filamu.
Mbaba bwana kazaliwa huko Pittsburgh, Pennsylvania, U.S. walikomkata mzee trump juzi hapo 😂😂😂 miaka 54 iliyopita.​
  • Kuzaliwa 1966 January 19
  • kazi-Muongoza filamu
  • Watoto 4
haya inatoshaa, sasa tuendelee , Fuqua ana kidamu flani cha sanaa kutoka kwa uncle wake, haya mambo ya sanaa sanaa, kayatoa kwa mjomba ake Harvey Fuqua alikua ni mwanamuziki,mwandishi wa nyimbo mwandaaji na pia alikua mkurugenzi wa kikundi chao cha muziki miaka hiyoo.
Kama ilivyo kwa baadhi ya jamaa alitokea familia choka mbaya enzi apeche alolo, pangu pakavu tia mchuzi namna ilee.
Kabla hajaanza na mambo ya kuandaa filamu aliwahi pia kuandaa video za wasanii wakubwa dunia kama kina ton braxton, Coolio mzee wa Gangsta Paradise, Stevie wonder, nk
Then taratibu akaanza kuingia kwenye filamu huku mdogo mdogo akiendelea na inshu zake za music video hadi pale alipoona sasa niache mambo ya muziki nikae huku, baada ya kuachia filamu ya kwanza aliyoshirikishwa kama co-director iliyoitwa THE REPLACEMENT KILLER mwaka 1998.
Baada ya hapo sasa kilichofuata ni kutoa kitu juu ya kitu na nyingi ya filamu na makala alisimama kote kama director na producer.

BAIT 2000​

TRAINING DAY 2001​

91EbJZH9JWL._AC_SL1500_.jpg


TEARS OF THE SUN​

images (1).jpg


KING ARTHUR 2004 Hii movie ndani yumo mzee baba David Beckham​

408D63EA00000578-0-image-a-272_1495223411882.jpg


SHOOTER 2007​

BROOKLYN'S FINEST 2009​

OLYMPUS HAS FALLEN​

images.jpg

EQUALIZER 1 2​

cff69ac001bf2213ccebbb03d6091eaf.jpg
Danzel Washington & Antoine Fuqua


MAGNIFICENT 7​

91b8fY5RrGL._RI_.jpg

Mizigo iko mingi mingi sana na ya ukweli hutakaa uchoke kuingalia jamaa amefanya documentary na Will Smith inaitwa What's my name?: Muhammad Ali movie kali sanaa. Hoolywood wnamjua vizuri jamaa huwa hakosei kwenye kazi zake toa kitu weka kitu yani. Kwa leo tuishie hapa next time nitakuja na history ya Hollywood upate kufahamu kwanini Hollywood inausishwa sana na maswala ya filamu za marekani kwanini baadhi ya wasanii huwasikiki au wanatoa kazi mbovu, mara Hollywood hawafanyi tena kazi na msanii fulani mambo ni mengi stay tuned.
 

Attachments

  • Fuqua-250x375.jpg
    Fuqua-250x375.jpg
    7 KB · Views: 2
TOKA UDOFO WANGU PRIMARY SCHOOL NILIIPENDA SANA MOVIE YA TEARS OF THE SUN, HAINIISHI HAMU. EQUALIZER NIMEANGALIA MIAKA YA HIVI KARIBUNI TU. ACHA NIMALIZIE ZILIZOBAKI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom