Antivirus mixtape yatinga ndani ya jumba la BBA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Antivirus mixtape yatinga ndani ya jumba la BBA

Discussion in 'Entertainment' started by Brooklyn, Aug 5, 2010.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mixtape maarufu hapa nchini inayokwenda kwa jina la AntiVirus yenye nyimbo zaidi ya nane zilizoimbwa na wasanii mbalimbali wanaojipambanua kama wapambanaji dhidi ya wizi wa kazi za wanamuziki wa kizazi kipya wanaoongozwa na mbunge mtarajiwa Mr. II aka Sugu imetinga rasmi katika jumba la Big Brother Africa (BBA).

  Katika hatua isiyotarajiwa, mshiriki kutoka Tanzania Mwisho Mwampamba aliwaeleza washiriki wenzake maudhui ya albam hiyo na kina nani wamelengwa.

  Alieleza pia namna ambavyo hata yeye alivyotaka kunyonywa na wadosi alipowapelekea movie yake aliyocheza akiwa Nigeria mara baada ya BBA1. Alisema alienda na master kwa mdosi na kwa mshtuko mdosi alimwambia atampa Tsh. 1 mil tu alafu haki zote za kuuza hiyo movie zinakuwa za mhindi huyo.

  Aliendelea kusema, alipokwenda kwa mdosi mwingine (tanzania kuna distributors 2 tu ambao ni mtu na mdogo wake) naye alimwambia atampa kiasi hicho hicho.

  In short ali support sana move ya Mr. II na wenzake ingawa alihofu na kutilia shaka kufanikiwa kwa vita hiyo kwani wasanii hawana ushirikiano.

  Source: BBA All Stars
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,995
  Trophy Points: 280
  SUGU moto Chini hadi BBA
   
 3. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,303
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  hii tape si mchezo yani kuna siri kibao nimezijua.
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Siri zipi umezijua?, ambazo ulikuwa huzijua
   
Loading...