(Anti-Tanesco system) Naachana na TANESCO na bili zao kubwa - JE WEWE? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

(Anti-Tanesco system) Naachana na TANESCO na bili zao kubwa - JE WEWE?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by newmzalendo, Feb 22, 2011.

 1. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Wadau wa JF
  nimeamua kuachana na Tanesco na Bili kubwa za Luku,huduma mbovu ya mgao,usio eleweka,Osterbay umeme haukatiki(nimeona mara 2 mfululizo-u may correct me on this),mgao wa upendeleo.

  Umeweza kununua gari ya milioni 5,umejenga nyumba ya millioni 35,Je utashindwa kufunga umeme milioni 2 wa uhakika bila kero za Tanesco.its time to have an Anti-Tanesco system installed in your house
  Nimeshatengeneza inverter na battery charging system,kwa sasa ninatumia backup inayochajiwa na tanesco.
  Sasa nashughulikia WindMill (kata Upepo) nikishaunga tu kata upepo yangu,nadisconnect Tanesco ,siwataki na siwahitaji Ng'O
  Ninapoishi kuna upepo wa kutosha,kwa wale ambao hamna upepo u can hookup a solar pannel.

  Nataka ni approach local bank kuona uwezekano wa kutoa mikopo ili niwauzie waTz wenye hasira na Tanesco kama mimi.
  How its going to Work:
  Unapata mkopo From the Bank ,eg Exim at a reasonable intrest.The Banks pays for the Anti-Tanesco system,then unaletewa na kufungiwa with a guarantee and service agreement,after a month the Bank wanaanza kukukata fedha kidogo kidogo from your salary or ur account

  kama utapenda kuwa mmoja wapo tafadhali nitumie PM yenye email yako na mji unaotarajia kufunga Anti-Tanesco System

  Nikishafanikiwa nawaandikia Tanesco waje wachukue box lao la LUKU.nawapa talaka ya moja kwa moja.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hayo nimekuwa nayafikiria kila siku kwani kutegemea Tanesco wasio na ushindani ni kupoteza muda tu.
  Kuna uwezekano wa kutumia wind mills za kutengeneza uememe binafsi kwa maeneo fulani. Pia kuna uwezekano mkubwa tu wa kutumia solar energy ambayo unachaji mchana mzima kwenye beteri na usiku unatumia. Umeme huo una uwezo wa kutumia kwa ajili ya radio, aircontion, cooler na taa kwa usiku mzima kutokana na charger ya siku iliyotangulia.

  Watu tumeweza ondokana na tatizo la maji kwa kuchimba visima vya kujitegemea kwa nini tuendelee kuendeshwa na tanesco?

  Nakuunga mkono na hapo umeme binafsi ukishashamiri utaona wameshikishwa adamu kabisa kama ilivyokuwa kampuni ya simu
   
 3. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  wakati Tanzania kuna kampuni moja ya Simu (Posta na Simu) ,kufungiwa line ilikuwa dili kama ilivyo sasa kufungiwa umeme na tanesco,walipoingia Mobitel na Tritel,Adesemi (phonebox) watz tukapata nafuu.

  Nuwa -Dawasco pia sasa cha moto wanakiona kwani watu wanatumia visima binafsi.

  Now its TIME for Tanesco Kuadibishwa.kwani watakosa wateja wengi,hivyo uwezo wa kujiendesha utazidi kupungua,wafanyakazi watapungwa,na watakao baki watakuwa na adabu kama walivyo wa TTCL kwa sasa.

  Ewura pia watakosa visijisent via makato ya LUKU.

  kama unaweza kununua Gari ambalo every day unalipia mafuta,itakuwa bora uzalishe umeme wako ,then later unanunua gari la umeme,(made in China its around 3000 USD)so u kill 2 birds with 1 stone.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hii ni njema sana wengi wakiamua hivi basi tanesco imekula kwao!
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu NM ...wateja wakubwa na ambao tanesco inawategemea ni corporates kama viwanda ... migodi mashirika ya umma n.k ndiyo maana wanadai pesa nyingi sana kwa wateja wadogo wadogo... prepaid customers kwao sio dili na ndio maana they dont care kufanya mgao... hivyo ukitaka kuwakomoa lazima uzalishe umeme wa ku supply kwa cooperate customers kama Geita Gold Mine or so .... hapo ndipo utakapo washitua ...lakini sisi wa luku ...tena watashukuru kweli kweli kuondoa vending business
   
 6. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  mkuu LAT kwa sasa ,Tanesco wako unreliable,wateja wakubwa corporates clients wameshaanza kutafuta their own source of energy, a good example Nemera Industries wapo pugu road(ex Sungura tex)wao wamechota Songas so wana umeme wao,nasikia pia cocacola wao wanatumia songas.
  wateja wadogo ni wengi mmno Tanesco can not just ignore them.kumbuka Tanzania haina viwanda vingi,i dont have the figures labda utupatie kuonyesha kuwa Tanesco hawategemei wateja wadogo.Do u have luku,go and re-read the receipt,compare it in the past 6months utaona price per unit inavyopanda kinyemela.
   
 7. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  electric Car
   
 8. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  View attachment 23675 kama unaweza kununua Gari ambalo every day unalipia mafuta,itakuwa bora uzalishe umeme wako ,then later unanunua gari la umeme,(made in China its around 3000 USD)so u kill 2 birds with 1 stone.

  electric Car
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuna uwezekano wa kuwa na mmoja anayesupply umeme kwa majirani kama nyumba mtaa mmoja, hali hiyo inaweza kuamsha wengi kuanzisha miradi ku kujikimu umeme na papo hapo wanasaidia majirani.
  Wind mills inapunguza sana gharama za umeme.

  Watu wafunzwe namna ya kuwa na akili ya bettery kwa ajili ya kuchaji ili kutumia wakati kwa ratiba maalum kama kuna kuwan na private supply.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Electric power Generator zinapatikana chini ya $ 2000, na hizo zina uwezo wa kusambaza umeme kwa matumizi ya watu binafsi kwa familia kadhaa na pia kuendeshea viwanda vidogo vidogo. Hautua hiyo itawafanya wengi wapumue.
  Tukumbuke huko nyuma tulikuwa na matatizo ya usafiri hadi mzee Ruksa aliporuhusu watu binafsi kutoa huduma za usafiri leo ni historia tu imebaki.
  Uwezo tunao.
   
 11. L

  LAT JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu NM .... suala kubwa na muhimu hapa si kushindana na Tanesco .. kwani tayari uzembe ni wa kwetu sisi watanzania kuwaachia TANESCO kuendelea kuhodhi uzalishaji, usambazaji na ugavi/mauzo ya umeme ..... whether we like or not ... it is because of the policy at hand .... kumbuka netgroup solutions walikuja na kufanya management ya tanesco kwenye ugavi .... walipiga pesa mbaya sana .... kwa magnitude ndogo na ya kawaida ya matumizi ya umeme ndio tunaoathirika na matatizo ya mgao ..... Sijaona mgao Cocacola kwanza factory... sijaona mgao Twiga Cement Factory (SONGAS wanawauzia percent fulani ya umeme wao) n.k ..... hivi haiwezekani watu binafsi wakanunua umeme direct kutoka kwenye vyanzo yaani power generating stations regardless ni ya TANESCO, SONGAS, AGRECO, IPTL, ARTMUS halafu wakatumia infrastructure ya tanesco kusambaza kwa kulipia service line tu .... yes kwanini tununue umeme kwa tanesco na wao hawana ubunifu mkubwa wa ugavi na mauzo...? yes mtu mmoja anaweza kuanzisha biashara kwa kununua certain megawatts kutoka kwenye chanzo akatumia distribution network ya TANESCO na kulipia service charges halafu akafanya vending...?...hi pia itapelekea wadau wengi kujikita kufua umeme wakijua kwamba kuna direct customers wa umeme na hivyo basi vyanzo vya uzalishaji vikaongezeka...... we have to think again

  lingine ..... kwa matumizi madogo madogo ya nishati ya umeme majumbani .... mimi nadhani tunatakiwa tutafute specific area of use au consumption reference point .... nikiangalia vijijini ninaona kabisa mahitaji makubwa katika nyumba /households ni taa (kuwasha taa tena ni muda mfupi wa usiku) ...sitaki kuzungumzia umeme kwa mijini kwa sababu tuna abuse matumizi ya umeme kwani nyumba moja waweza kuta kuna TV tatu zote zinawaka, utakuta kuna garden lights zinawaka usiku kucha, utakuta kuna water fountains zinawashwa.., utakuta majumbani hot water cisterns wakati hali ya hewa inaruhusu kuoga kwa maji ya kawaida n.k ....hivyo basi umeme wa kuwasha taa vijijini kwetu unaweza kupatikana kwa njia nyingi mbadala bila kusubiri bwawa la mtera lijae kwa kudura za mwenyezi mungu na sala zisizo isha ingali tukijua dunia ina tatizo la global warming ..... kuna renewable energy resources nyingi kama upepo na jua..... tusisubiri serikali....tunaweza kuleta hand made technology ndogo ndogo kwa ajili ya kuwasha taa ...hivi kweli kuwasha taa usiku katika nyumba vijijini tunahitaji kusubiri AL Adawi na DOWANS yake wawashe mitambo ndio tuwashe taa .....ha ha haaaa ..... tuamke .... lighting for your life energy is an affordable and yet sustainable means of energy resource ... sun and rain will always replenish

  my take: lets adopt the transfer of technology mechanisms from various successful partners and friends .... kama ni solar panels za kuwasha taa .... kwa nini tusitafute cheap technology tukailipia tukapewa how to do manuals .... tukaanza kuzitengeneza humu humu Tanzania tena zisitengenezwe DSM .... kila makao makuu ya wilaya yawe na center ya kutengenezea hizi panels kwa bei nzuri hand in hand serikali ifanye empowerment kwa kuwapa exemptions wadau watakaoanzaisha hizi biashara kwani itawanufaisha wananchi direct bila serikali kuumiza kichwa
   
 12. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante NM; imefikia wakati wa kuyatazama matatizo kama FURSA (OPPORTUNITY) ambazo tunaweza kuzitumia katika dhana ya uwekezaji na huku tukihudumia jamii inayotuzunguka; kubaki kuendelea kuwalaumu TANESCO, SERIKALI na wengineo haitatusaidia sana. Wakati umefika kwa sisi waTZ kuchukua hatua badala ya kuwasubiri wakina AL ADAWI kuziona hizi FURSA na kutunyonya. Hata nami nilipata wazo la kwenda kufanya majribio ya hizi CRANK BOX kijijini kwetu na nikifanikiwa nitawashawishi wana KIJIJI wenzetu kutumia hizi badala ya kusubiri umeme wa TANESCO; kweli mahitaji makubwa ya umeme kijijini kwa matumizi ya nyumbani ni kuwasha taa na siku hizi kuchaji simu mambo ambayo CRANKBOX inaweza kutekeleza.
   
 13. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  mkuu Wazo la knowledge transfer nimekuwa nalo toka 2009,na nimeanza kulifanyia kazi,i am now institutionalizing these ideas,i have started with an entity called Vision Community Services,lengo ni kutransfer Eco-solutions knowledge.
  kwa mfano,
  Unapofunga wiring,unafanya circuit separation ,i.e Light circuit inakuwa tofauti na appliance circuit ,hivyo unaweza kutumia watts20 panel kwa ajili ya taa tu na kuchaji simu ,and low wattage devices like radio.hivyo umeme ukikatika taa zinakuwa on line bila kuishi na giza la tanesco.
  Elimu ya matumizi ya energy inabidi ifundishwe kuanzia shule za msingi.na secondary iwe optional like Civic or divinity ilivyokuwa.

  Kwa msingi huu tanesco hawatakuwa na umuhimu,ukizingatia watanzania wengi matumizi ya umeme ya nyumbani ni kwa ajili ya
  Taa 6 (usiku for 9hrs) kabla ya kulala unawasha za ndani,ukishalala mnawasha za nje(security lights)
  Tv -moja usually 4hrs per day
  Radio 1-
  wengine hasa wa mijini wanatumia Fridge- so unaongeza pannels or windmill.
   
 14. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,567
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  nimeyapenda mawazo ya wadau wote ktk thread hii.it is high time watu watafute altenative solution.hawa jamaa nimeangalia short na long term plans zao HAKUNA KITU KABISA
   
 15. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Crank box is the best solution.Lini unaenda kijijini?nipe feedbak ya upokeo wa hiyo CrankBOX.

  kuna JF member alitangaza kuuza hizi box,zinawasha taa 3,bei ilikuwa nzuri sana Elfu 15. so kama hazijakuwa subsidized ,inamaana anauza kwa profit,Je zikiwa subsidized zanaweza kuuzwa kijijini kwa shillingi Elfu 10.
  Cha kuzingatia kila kijiji kiteuwe vijana wa5 ,wapewe mafunzo ya kufanya DC wiring ktk nyumba kwa ajili ya Taa na radio/phone charger.then mtu akinunua crank box/solar panel or windmill anaichomeka na ktk point moja ndani ya nyumba ambayo inagawa umeme nyumba nzima.
  Nina Solar boxes kwa bei poa ya 50,000 ziko chache naweza kukupa ukaenda nazo village.
   
 16. L

  LAT JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  simple Toolbox technology kama vile home made solar panels ndiyo itakayoweza kutukwamua especially kwa technology outreach societies kama za vijijini na ukizingatia wengi wa vijijini ni under privileged .... simple products ambazo vijana wanaweza kuwa trained for one week wakajishugulisha kama jua kali na kujiajiri wenyewe huku wakitoa suluhisho la energy for light in their homes without forgetting battery charging for our artificial fore limb aka cellphone and so on

  kuna package za how to build your own solar panel at home ...very interesting .... it contains a downloan version ya how to do manual na CD ya video ya jinsi ya kutengeneza/kuassemble solar pannel...hii ndiyo maana ya transfer of technology..... it is just a matter of translation into swahili language .... halafu tunafundisha vijana jinsi ya kutengeneza sola panels za mpaka 150 watts na ukiweza tengeneza panels 10 ..hii inamaana utakuwa na 1.5 KW ... incredible...kwa vijijini hii inatosha sana .... careful ninajitahidi kufanya online window shopping ya which is the best and affordable package ya home made solar panel (toolbox technology) ili niweze kuinunua ....

  NM ... i will update you on this soon.... it can be something good to start with

  tusisubiri AL Adawi kuja kuleta mitambo yake na baadae kuanza kutusengenya na kutudai fidia na mwisho kuingia nchini na kuzurura zurura huku akikataa kuonesha sura yake
   
 17. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,197
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  i just love JF

  Leo nimepata knowledge kubwa mno. Najipanga kifedha niwe Anti-Tanesco.

  For istance nikiuza gari naweza kununua solar panels na inventer, then next year nijipange tena kununua gari
   
 18. k

  kassamali JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kweli haya ni mawazo mazuri sani watu mmeanzisha topic kama hizi naamini kuna wengine mna uelewa mkubwa na masuala ya umeme nimefuatilia kwa karibu juu ya hii program ya EWURA ya wafuaji wadogo wadogo wa umeme na kuna bei wameziainisha pale kwa mfano

  The proposed Tariff for the year 2011 for the sale of electricity to the Main
  Grid in Tanzania

  Dry Season (August to November) 134.92 TZS/kWh

  Wet Season (January to July, and December)101.19 TZS/kWh

  Je hizi KWh ngapi ni MW 1?
  mfano mtu ana windmill ya MW 1 na anataka kuuza TANESCO je kwa mwezi anaweza kukusanya kiasi gani maana yake pia windmill iko complicated sana na hasa kwenye servises zake nasikia aghali na inahitaji utalaamu

  na je kwa maisha ya sasa hii 101.19 TZS/kWh ni sawa au ni bora kufua umeme na kuwauzia kijiji fulani
   
 19. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Actually unaweza kuuza gari lako ukanunua la gharama nafuu na pia ikabaki pesa ukanunua Solar system/windmill
   
 20. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  GARI YA UMEME,INATEMBEA 180KM PER SINGLE CHARGE.eg FROM MBAGALA TO POSTA NI 15KM NI TRIPU 12[​IMG]


  [​IMG] Click to enlarge image
  Bacis parameter
  Body metal-body
  Dimensions(L*W*H) 2630mm*1430mm*1560mm
  wheel base 1700mm
  Track width(f/r) 1100mm
  Drive type front wheel driving
  Braking system hydraulic disk for 4 wheel
  Mi ground clearance 150mm (full loaded)
  net weight 450kg(without battery)
  Max. speed 55 km/h
  Max. climbing ability (loaded) 30%
  Min turning diameter 3m
  braking distance 5m
  running distance 180km
  charging time <8h
  parking brake hand brake
  speed control pedal control/automatic
  power specification
  Motor 60v AC 4KW
  Electric system 12V DC
  Charger 120V 20A 110V/220V input
  controller 48V
  Battery 6V 240AH*8 lead acid
  Battery type lead-acid free maintenance battery(Gel battery)
  weight of battery 338kg
  battery life Recharging for 800times
  convertor DC 12V
  chassis system
  suspension system 4 wheel independent suspension
  steering system rack and pinion steering gear
  wheel typr (f/r) 145/70R 1269H

  Valid Until 2012/01/18
   
Loading...