Mark pawelk
Senior Member
- Jan 6, 2017
- 103
- 339
OKTOBA 25 2001
" Why do you always want to blame someone in the Middle East? This is a very genious work requiring sophiscated equipments,It's very unlikely to be produced in some cave" (kwanini mnapenda kuwalaumu watu wa nchi za mashariki ya kati'waarabu'? Hii ni kazi ya utaalamu mkubwa inayohitaji vifaa vya teknologia kubwa,si rahisi ikawa imefanyika katika mapango'
Hayo ni maneno ya mkurungezi wa FBI Robert Mueller akiongea kwa ukali huku akigonga meza, Hali hii inawashtua sana waliopo kwenye kikao, Haijawahi kutokea mkurugenzi huyu kuonekana mkali hivi tena mbele ya Rais George Bush pamoja na makamu wake Dick Cheney..
Hasira za mkurugenzi huyu zinatokana na kitendo cha viongozi wengi wa juu wakimhimiza kutoa kauli kua shambulio hili la 'ANTHRAX LETTER ATTACK' ni muendelezo wa mashambulio ya kigaidi yakiongozwa na Al-Qaeda dhidi ya Marekani.. Hii ni kwenye kikao kilichohusisha viongozi mbalimbali wa juu kilichofanyika ikulu ya marekani, Hapa ndipo mkurungezi wa FBI Robert Mueller anashauri kila mtu atulize jazba na wawape muda FBI pamoja na wanasanyansi wafanye uchunguzi na kujua nini hasa chanzo cha shambulio hilo.. Turejee kwenye shammbulio lenyewe..
SEPT 18 2001
Hii ni wiki moja baada ya tukio la kigaidi la kulipuliwa jengo la WTC(world trade centre) jijini New York,Marekani ambalo linasadikika kufanywa na kundi la kigaidi la Al-qaeda... Wakati vyombo vya usalama na nchi nzima ikawa katika hali ya sintofahamu Marekani wanapata tena shambulio lingine la kigaidi
Barua 5 zenye analisi microbiologia za kimeta(anthrax spores LINK) zinatumwa katika ofisi mbalimbali za vyombo vya habari.. Barua hizo zinatumwa kwa ABC news, CBS news, NBC news, NEW YORK post zote za jijini New York pamoja na AMI(American Media Inc) iliyopo Florida..
Wafanyakazi wengi wanaofanya kazi katika vyombo hivi vya habari wanapata maambukizi ya kimeta hali inayozua tafrani katika nchi ya Marekani kwani mara ya mwisho ugonjwa huu ulimuua mtu miaka 26 iliyopita nchini hapo na ulikua umedhibitiwa haswa.. Ugonjwa wa kimeta huwezwa kuzalishwa maabara na kutumika kama silaha, Hivyo marekani wakachukulia tukio hili kama tukio la kigaidi.. (BIOTERRORISM) ambapo vimelea,virusi au sumu za kibaologia huzalishwa kwa makusudi na kuachiwa kama silaha..
Wiki tatu badae barua mbili zinatumwa kwa ma seneta wawili wa chama cha Democratic, seneta Tom Daschle na Patrick Leahy... Barua ya seneta Daschle ilifunguliwa na msaidizi wake ambaye alipata maambukizi ya kimeta huku barua ya seneta Leahly ikirudishwa posta kwasababu ya kukosewa kwa namba ya posta(zip code).. ambapo ilifunguliwa na mfanyakazi wa posta ili kubaini inaenda wapi ambaye nae alipata maambukizi
Barua hizi mbili kwa ma seneta hawa zilikuja kubainika kua analisi microbiologia za kimeta(anthrax spores) zilizotumika zilikua hatari sana zaidi ya zile zilizotumika awali kwenda kwa vyombo vya habari.. watu 22 walipata maambukizi ya kimeta huku watu watano wakipoteza maisha...
madhara ya ugongwa wa kimeta photo credit:wikipedia
FBI WANAANZA UCHUNGUZI
Katika rekodi za FBI hii ni moja ya kesi yenye uzito mkubwa katika historia ya marekani, kesi hii iliyopewa jina la 'AMERITHRAX' ilikua ikifanyiwa kazi na mamia ya mawakala wa FBI. Rekodi inaonyesha mawakala wa FBI walisafiri mabara 6, Wakahoji zaidi ya watu 9000 na wakafanya upekuzi katika majengo 67 ili kubaini ukweli wa shambulio hili. Pia walitangaza zawadi ya dola za kimarekani milioni mbili na nusu kwa mtu yeyote atayekua na taarifa muhimu kuhusu hii kesi.
tangazo la zawadi ya $2.5M photo credit: biography
Zikachukuliwa sampuli kutoka kwenye zile barua na kutumwa katika maabara 16 nchini Marekani mahususi kwa utafiti wa kibaolojia pamoja na nyingine kupelekwa nchini Canada,Sweden na Uingereza. Pia wakafanya uchunguzi wa vituo 600 vya posta kuona kama watakuta kituo chenye analisi microbiologica za kimeta(anthrax spores). Kati ya vituo vyote 600 ni kituo kimoja tu cha Princeton, NEW JERSEY ambacho kilikutwa kina vimelea vya kimeta. Hii iliwafanya FBI kubaini kua barua zile zimetoka katika kituo hiki
Katika kuchukua tahadhari FBI ikishirikiana na kituo cha kuzuia magonjwa nchini Marekani waliamuru kufungwa kwa kituo kilichokua kikifanya utafiti wa kimeta kilichopo Lowa, kituo hiki kilikua mahususi kwa ajili ya wafanya utafiti wote wa kimeta.
a)barua kwa vyombo vya habari
b)barua kwa maseneta photo credit a&b: biography
UCHUNGUZI WA BARUA hizi unaibua maswali mengi, kwanza barua zilizoandikwa kwenda kwa vyombo vya habari viliandikwa bila ya kutumia vituo(punctuations) wakati zile zilizoandikwa kwenda kwa ma seneta ziliandikwa kwa kutumia vituo.
Pili mwandiko uliotumika kuandika barua kwenda kwa vyombo vya habari pamoja na bahasha yake ilikua mkubwa mara mbili zaidi ya uliotumika kuandika barua kwenda kwa maseneta.. pia barua iliyoandikwa kwenda kwa maseneta ilionesha kutoka katika anuani ifuatayo
greenade school,
franklin park new jersey NJ 08852
Walivyofatilia wakakuta New Jersey hakuna anuani wala shule inayoenda kwa jina hilo..
Barua zinaonyesha kama zimetoka kwa mtu wa jihadi, mwarabu au mtu anayetaka kutambulika hivo.. Lakini kwanini katika barua anashauri watakaopokea barua hizo watumie dawa?? TAKE PENICILIN NOW.... Na katika barua kwenda kwa seneta ameweka wazi kua ni kimeta? WE HAVE THE ANTHRAX.. Utata mwingine ni pale barua hizi zilikutwa zimefungwa kwa vifaa maalamu na ustadi mkubwa ili vimelea hivi visiweze kutoka mpaka hapo tu barua ikifunguliwa. utata mwingine ni pale barua zote zikionesha kuandika septemba 11 siku ambayo palitokea shambulio la kigaidi..
WATUHUMIWA waliohusishwa na shambulio hili mwanzo kabisa walikua kikundi cha ki gaidi cha Al-Qaeda, ikumbukwe ni wiki moja tu baada la shambulio la septemba 11. Hivyo ikaonekana kama muendelezo wa mashambulizi ya kikundi hicho, Ila kabla ya kufanya maamuzi walipisha uchunguzi uendelee ili kubaini ukweli, Pia kulikua na uwezekano likawa shambulizi kutoka kwa mtu wa hapo hapo Marekani kutokana na teknolojia na utaalamu uliotumika, waliohusishwa na tukio hili ya kigaidi ni wafuatao...
AL-QAEDA
Uchunguzi unafanyika ili kubaini kama AL-Qaeda wamehusika katika tukio hili, katika uchunguzi huo inabainika kua moja ya wafuasi wa AL-Qaeda Ahmed Al Haznawi aliyehusika katika shambulio la utekaji ndege kisha kuzigongesha katika jengo la WTC anaweza kua mhusika katika tukio hili
Inabainika kua hapo nyuma bwana Al Haznawi alikua na rekodi ya kuhudhuria katika hospitali ya Fort Lauderdale iliyopo Florida akiwa na kidonda kikubwa cheusi mguuni kwake ambacho alidai kua alikipata baada ya kuangukiwa na begi, Hii inawapa mashaka FBI kua huenda Al Haznawi alikua na kimeta
Uchunguzi zaidi unaleta rekodi za hospitali ambazo zinaonyesha wahusika wengine wawili katika tukio la septemba 11 Mohammed Atta na Marwan Al Shehli walihudhuria hospitali kutafuta dawa kwa ajili ya Mohammed Atta ambaye alikua na vidonda na miwasho mikononi mwake, ikumbukwe vijana wote hawa wa AL-Qaeda walikua wakisoma na kuishi Florida, rekodi hizi za hospitali zinaleta uwezekano wa kuhusika kwa hawa AL-Qaeda, Hisia zinakuja pale FBI wanapodhani kua vijana hawa walikua na vimelea hivi vya kimeta na pengine huenda vilianza kuwashambulia wao.
Lakini ajenda zote hizi zinakosa mashiko kwani vijana hawa walifanya tukio septemba 11 na walishafariki, Barua zilianza kutumwa kuanzia septemba 18, je huenda walikua na watu wengine wa ziada kuandeleza matukio??
IRAQ PAMOJA NA SADDAM HUSSEIN
Oktoba 2001 yakaja matokeo mezani kwa FBI yakionyesha kua na kemikali ya 'Bentonite' katika sampuli za vimelea vya kimeta zilizochukuliwa, Kemikali ya Bentonite ilijulikana kutumika na nchi moja pekee duniani katika kutengeneza silaha za kibaolojia duniani, nchi ambayo ni IRAQ, Bentonite ilikua kama utambulishi(trademark) ya mpango wa Saddam Hussein wa kutengeneza silaha za kibaolojia, hakuna nchi nyingine ilikua ikitumia bentonite
Kuwepo kwa bentonite katika sampuli ilidhihirisha wazi kuhusika kwa Saddam Hussein pamoja na Iraq katika shambulio hili, oktoba 29 2001 msemaji wa ikulu ya Marekani akatupilia mbali ajenda hii ni kudai uchunguzi zaidi umebaini sampuli zilikua na 'Silica' pekee yake na wala si bentonite
STEVEN HARTFIL
FBI wakatoa tamko kua huenda likawa shambulio la ndani, Inawezekana kabisa akawa ni mmarekani anayehusika, Steven Hartfil ambaye alikua mtaalamu wa masuala ya virusi(virologist) alipokea barua kutoka Malaysia ambayo iliwapa wasiwasi wafanyakazi wa posta, hivo wakawasiliana na FBI, Barua hii kutoka kwa mpenzi wake Hartfil ilikua na cheki ya benki pamoja na majarida na filamu za ngono, FBI wakafanya ukaguzi wa barua hii na kubaini kua ina vimelea vya kimeta
Haraka FBI pamoja na DOJ(department of justice) wakamtangaza Steven Hartfil kama mtuhumiwa mkuu wa shambulio hili, wakaenda kufanya ukaguzi kwenye nyumba yake lakini hawakupata ushahidi wowote, vyombo vingi vya habari vikamtangaza Hartfil kama mhusika wa hili tukio, Uchunguzi zaidi wa ile barua ukaja kuonyesha kua matokeo ya mara ya kwanza hayakua sahihi, vifaa vilivyotumika vilitoa matokeo yasio sahihi(false positive test)...Hii ilimfanya Hartfil kuwaburuza mahakamani FBI na DOJ pamoja na vyombo mbalimbali vya habari..
Hartfil alikuja kushinda hii kesi na mahakama ikawaamuru FBI na DOJ kumlipa Hartfil dola za kimarekani milioni tano na laki nane($5.8M).. kesi dhidi ya Hartfil na vyombo vya habari iliisha nje ya mahakama kwa wao kukubaliana japokua haikuwekwa wazi ni kiasi gani Hartfil alilipwa
BRUCE EDWARD IVINS
Huyu alikua mfanyakazi wa Marekani kwa miaka 18 katika idara ya kupambana na mashambulizi ya silaha za kibaolojia(bio-defense) lakini kibao kikaja kumwagukia yeye, Yeye alikua moja ya timu ya wanasayansi waliokua wakifatilia kesi hii, Lakini kila mara akileta ripoti ya uchunguzi FBI walikua wakipata mashaka sana,kana kwamba anataka kupindisha ukweli wa shambulizi hili..
FBI wakaamua kupima na kulinganisha sampuli zilizotumika katika shambulio hili dhidi ya sampuli zote zinazopatikana katika maabara zinazohusika na mambo ya silaha za kibaolojia nchini kwake, wakachukua kila sampuli katika kila maabara nchini mwao, matokeo yakaja kua vimelea vilivyotumika katika shambulio hili vimefanana na moja ya sampuli iliyopo katika 'flask RMR-1029'
FBI kuja kuangalia hii sampuli inatoka wapi wakapigwa na butwaa, sampuli hii inatoka katika maabara iliyokua ikiongozwa na Bruce Edward Iwins, ikabidi nguvu zote wazielekezee kwa mtaalamu huyu, wakaanza uchunguzi katika maabara hii iliyokua ikiongozwa na Ivins, uchunguzi ukaonyesha kua Edward Ivins alikua akichukua vifaa pamoja na sampuli mbalimbali na kuondoka nazo nje ya maabara bila kuviandikisha kitu ambacho ni kinyume cha sheria
Alipohojiwa alikua na madhumuni gani kufanya hivyo akawa anatoa maelezo yasiyoeleweka, katika vipindi tofauti Edward Ivins alishakua na matatizo ya akili, Hii ilipelekea FBI kufatlia katika hospitali aliyokua akitibiwa, wakaonana na daktari aliyekua akimtibu Ivins, Ambaye alidai kua Ivins kuna kipindi alimwaambia kua kuna mwanamke anampenda na anapanga kumuua, pia alishamueleza kuhusu kumuua mfanyakazi mwenzake aliyekua akimsumbua, Ivins mara kwa mara alikua akijisifu kua ni mtu ambaye anaweza kutelekeza mauaji kwa akili sana bila ya mtu yoyote kujua
Bruce Ivins photo credit:wikipedia
FBI wakaamua kwenda kusachi nyumba aliyekua akikaa Ivins,walipofika wakamkuta akiwa anatupa kitabu cha 'Godel,Escher Bech' ambacho kilikua kinazungumzia namna mbalimbali ya kutengeneza vimelea, kitabu hiki pia kilizungumzia namna mbalimbali ya kuficha ujumbe kutumia alama za kemikali(chemical abbreviations hidden messages), FBI wakasachi nyumba hawakupata kielelezo cha maana, hivyo wakarudi kuzifanyia uchunguzi barua zile kuona kama kuna ujumbe wowote uliofichwa
09-11-01
THIS IS NEXT
TAKE PENACILIN [sic] NOW
DEATH TO AMERICA
DEATH TO ISRAEL
ALLAH IS GREAT
Katika barua hio utaona herufi kadhaa zikiwa zimekolezwa(bolded).. herufi hizo ambazo ni TTT AAT TAT, Wanasayansi na wataalamu wa mafumbo wakaja na majibu yafuatayo.. alama hizi zilikua ni mfupisho(abbreviation) wa kemikali zifuatazo
TTT= Phenylalanime(inawakilishwa na herufi moja F)
AAT=Aparagine.......(inawakilishwa na herufi moja N)
TAT=Tyrosine.........(inawakilishwa na herufi moja Y)
Wakaja na maneno mawili kama unavyoona hapo juu, PAT na FNY.. Katika kung'amua maana ya maneno hayo,ikabainika kua PAT ni jina na utani la aliyekua rafiki na mfanyakazi mwenzake Iwins, FNY ikiwa na uwezekano wa Fu*k New York. Hii ilitokana na maelezo ya wafanyakazi wenzake ambao walidai kwa muda mrefu Ivins alikua akilichukia jiji la New York na hawakuelewa kwanini, tukumbuke kua karibia barua zote zilitumwa jijini New york. Swala lingine ni kua serikali ilikua na mpango wa kufunga maabara hii inayoongozwa na Ivins hivyo huenda alifanya shambulizi ili umuhimu wao uzidi kuonekana
FBI wakamtangaza rasmi Bruce Edward Ivins kua mtuhumiwa namba moja wa kesi hii, kuna siku Bruce akaenda katika kikao cha kisaikolojia mahali ambapo alikua anatibiwa, akawa na hasira sana, akawaeleza wazi kua anachukizwa na kua mtuhumiwa wa kesi hii, Akasema hawezi kukubali kuja kuhukumiwa kunyongwa, akadai kua kesho yake atawaamua wote waliomkosea ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wenzake, akawaeleza kua ana mpango wa kwenda kuchukua silaha kutoka kwa mtoto wake wa kiume maana FBI wanamuangalia nyumbani kwake muda wote
kabla ya kutelekeza haya na kabla hata ya kesi kupelekwa mahakamani Iwins alikutwa nyumbani kwake akiwa amejiua, FBI badae wakaja kufunga hii kesi na kudai Ivins ndo mhusika wa shambulizi hili, kitendo ambacho kilipingwa na wanasayansi wengi sana, kuna Afisa wa FBI alijitokeza na kudai kua kitendo cha FBI kutopata kielelezo chochote nyumbani mwa Ivins kilishusha hadhi madai yao.. Pia barua za mashambulizi zilitumwa New Jersey siku ambazo rekodi zilionyesha Iwins akiwa kazini
UWEZEKANO LIKAWA SHAMBULIO LA KISIASA
Magwiji wa siasa badae wakaja na mambo manne ambayo yanaweza kufanya shambulio lile kua la kisiasa
a) Barua mbili zilitumwa kwa ma seneta wa chama cha Democratic hivyo endapo wangeuawa, moja kwa moja ingemaanisha chama cha Republic kingekua na ma seneta wengi, na kuna kila uwezekano nafasi hizi zingechukuliwa na ma seneta wa Republic
b) Zaidi ya dola za kimarekani bilioni moja($1B) zilitumika kusafisha majengo dhidhi ya vimelea vya kimeta(anthrax decontamination) hivyo inaweza kua kazi ya watu flani wenye maslahi yao
c) Bajeti ya nchi katika kupambana na silaha za kibaolojia iliongezeka kwa kiasi cha dola za kimarekani bilioni tano na laki sita($5.6B).. hivyo kuhisiwa inaweza kua mpango wa watu flani
d)Hili tukio lilitumika sana kama chachu ya uvamizi wa iraq mwaka 2003
Kesi hii imefungwa na FBI inamtambua Bruce Ivins kama mhusika wa tuki hili japo chama cha wanasayansi Marekani walitoa kauli yao ya mwisho kuashiria Iwins hawezi kua mhusika,kauli ya mwisho ya chama cha wanasanyansi...
"no matter how good a microbiological forensic maybe,they can only,at best, link anthrax to a particular strain or lab, they cannot link it to any individual"
REFERENCE
>FBI released files on the AMERITHRAX case
~Mark Pawelk~