only83
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 5,343
- 2,525
Akihutubia kwenye ibada ya Jumapili kanisani kwake, Mchungaji Antony Lusekelo alimaarufu Mzee wa upako amesema kuwa Tanzania kama nchi inakwenda kuanguka muda si mrefu.
Akiongea kwa uchungu na masikitiko makubwa, Mchungaji Lusekelo amesema ukiona viongozi wakubwa wa nchi wanapata ujasiri wa kuiba mabilioni ya shilingi wakati kuna watu hawana maji, madawati ya shule, huduma za afya tambua Taifa hilo linakwenda kuanguka.
Akaendelea kusema ukiona Twiga wanapakizwa kwenye ndege wakiwa wazima, ukiona Tembo wanauwawa kila siku bila kuchukuliwa hatua ni dalili kuwa Taifa linakwenda kuanguka.
Amesema, Taifa kama China wamejiwekea misingi ya kuhakikisha wanavunja maagano ya umma wanauwawa au kunyongwa.
Kwa mujibu wa Mchungaji Lusekelo, hatua kali dhidi ya majambazi ya mali ya umma zimeiwezesha China kupaa na kuanza kuikalibia Marekani kwa ukaribu kwa nguvu za uchumi.
Source: Channel Ten