Anthony Lusekelo: "Tanzania inakwenda kuanguka muda si mrefu"

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,344
2,000
Akihutubia kwenye ibada ya Jumapili kanisani kwake, Mchungaji Antony Lusekelo alimaarufu Mzee wa upako amesema kuwa Tanzania kama nchi inakwenda kuanguka muda si mrefu.

Akiongea kwa uchungu na masikitiko makubwa, Mchungaji Lusekelo amesema ukiona viongozi wakubwa wa nchi wanapata ujasiri wa kuiba mabilioni ya shilingi wakati kuna watu hawana maji, madawati ya shule, huduma za afya tambua Taifa hilo linakwenda kuanguka.

Akaendelea kusema ukiona Twiga wanapakizwa kwenye ndege wakiwa wazima, ukiona Tembo wanauwawa kila siku bila kuchukuliwa hatua ni dalili kuwa Taifa linakwenda kuanguka.

Amesema, Taifa kama China wamejiwekea misingi ya kuhakikisha wanavunja maagano ya umma wanauwawa au kunyongwa.

Kwa mujibu wa Mchungaji Lusekelo, hatua kali dhidi ya majambazi ya mali ya umma zimeiwezesha China kupaa na kuanza kuikalibia Marekani kwa ukaribu kwa nguvu za uchumi.

Source: Channel Ten
 

samaki2011

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
1,776
0
Ataanguka yeye na familia yake na wapumbavu wenzake! Pamoja na matapeli wenzake!

Ataiacha Tanzania ikiendelea kusonga mbele!
Hatukuamini tena hata ujiapize kwa miungu ya baali na kujikatakata kwa viwembe hatukuamini ng'ooo ndo nyie mliowahi kupinga wizi wa escrow mkaangukia pua
 

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,518
2,000
watabiri wa nyakati hizi hasa wachungaji na wapiga ramli,tabiri zao siku zote huenda sambamba na matukio halisi.hana lolote huyo,kasoma status quo ya nchi ktk wakati huu mgumu wa auto pilot.
 

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,939
2,000
Hatukuamini tena hata ujiapize kwa miungu ya baali na kujikatakata kwa viwembe hatukuamini ng'ooo ndo nyie mliowahi kupinga wizi wa escrow mkaangukia pua
Sijakulazimisha uniamini.
Aliyeangukia pua kwenye Escrow ni Zitto na kamati yake ya kizushi. Nani kakudanganya kuna uwizi kwenye Escrow? Zile ni siasa chafu tu.
 

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,250
Lakinimie nilichosikia kikitoka kinywani mwa LUSEKELO alisema kuwa ANIPENDA TANZANI SANA na KUWA YUKO TAYARI KWA LOLOTE NCHI YAKE ISIANGAMIE.

Nilipenda kauli yake ya kuwa anaipenda KANANI yake TANZANIA.Ndio kusema ata sali usiku na mchana na Taifa letu LITASHINDA.
 

spiritual hero

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
354
0
Ataanguka yeye na familia yake na wapumbavu wenzake! Pamoja na matapeli wenzake!

Ataiacha Tanzania ikiendelea kusonga mbele!
True mkuu. Tanzania haiwezi kuanguka kirahisi wakat kuna UKAWA wako standby kulihuisha taifa. Big up! achana na huyu mchungaj bongofleva
 

TAU 1

JF-Expert Member
Jan 8, 2013
505
500
Huyu sio Mchungaji ni tapeli.

Hafuati maandiko ya bibla yanavyosema!
Kama huyo mchungaji ni tapeli?basi nani aliye bora kwenye ujambazi na utapeli wa mali za nchi? Kama walioinjinia wizi mkubwa ambao haujawahi tokea nchi hii tangu uhuru na mchungaji lusekelo? Kama hujui kusoma basi hata picha? Pole sana MSALANI...
 

rnaluyaga

Senior Member
Jul 6, 2014
139
0
mchungaji alikuwa anaongea na watu wenye akili tena wale wanao ona taswila na msitakabali wa taifa hili,lakini nyie mnaotukana mshukru katiba ya inchi hii ibara ya nane(uhuru wa mawazo) vinginevyo.......
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom