"Anthony Komu subiri jimbo la Uru"

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,395
208
Wachaga na ubaguzi wao! Hii nimeisikia kabla ya uchaguzi, watu wakidai hawatakubali kuwakilishwa na mtu kutoka Uru! Na imekuwa hivyo kweli. Sina uhakika kama matokeo haya ya uchaguzi yametokana na kampeni za aina hiyo maana sijafika Moshi kipindi chote cha kampeni na uchaguzi. Lakini kwa uzoefu wangu wa jinsi hao jamaa wa Uru wanavyodharauliwa na wachaga wenzao, naanza kuamini kuwa kuna ukweli katika kauli waliyokuwa wanamwambia kuwa 'subiri mpate jimbo lenu la Uru'. Kama Pemba na Unguja. Wajomba zangu (precisely wajomba wa babangu) kule Hai wamemchagua Mbowe, nawapongeza, labda kwao hawajachakachuliwa (hakuna factor tofauti na umachame). Kule Moshi vijijini factor ya u-Uru na u-Kibosho ina nguvu kuliko sera. What a shame!
 
komu fisadi wa chadema anayekwapua ruzuku na mbowe. slaa awe mwenyekiti na kaka zitto katibu yule wa mpanda makamu na pateni kiongozi mzuri zanzibari

moshi werevu vunjo wamemchagua shujaa wangu mrema
 
Wakibosho ni wakibosho na Wa Uru ni wauru japo wote ni Wachagga. Mbinu za Cyril Chami ni za kitoto kabisa na ina maana hata ushindi wake ametumia mbinu za kitoto tu kuonyesha jinsi wakibosho walivyo nyuma katika karne hii ya sasa. Wangi wao ni wafanyanyabishara lakini shule ni bure kabisa. Kwa hiyo usishagae hilo. Pili jua Kibosho ni kubwa mno kuliko Uru .
 
Hujui unachokiongea. Mbowe anakuapua ruzuku wapi wakati anajitolea pesa zake kuendesha CHADEMA. Inavoelekea akili zako zimekuruka kama za Mrema huyo unayemsifia make huko ndo kuna purukushani za ruzuku. Na safari hii kashinda Mrema peke yake TLP atalamba posho bungeni na ruzuku yote yake make anajua hana cha kupoteza chama chake kisha kufa.

komu fisadi wa chadema anayekwapua ruzuku na mbowe. slaa awe mwenyekiti na kaka zitto katibu yule wa mpanda makamu na pateni kiongozi mzuri zanzibari

moshi werevu vunjo wamemchagua shujaa wangu mrema
 
Wakibosho ni wakibosho na Wa Uru ni wauru japo wote ni Wachagga. Mbinu za Cyril Chami ni za kitoto kabisa na ina maana hata ushindi wake ametumia mbinu za kitoto tu kuonyesha jinsi wakibosho walivyo nyuma katika karne hii ya sasa. Wangi wao ni wafanyanyabishara lakini shule ni bure kabisa. Kwa hiyo usishagae hilo. Pili jua Kibosho ni kubwa mno kuliko Uru .

Hii imedhihirisha matumizi mabaya ya majority vote, voting for all the wrong reasons! Ubaguzi wa aina hii ni hatari sana. Maana yake ni kuwa hao wauru hata wasiporidhika na mbunge Chami bado hawana uwezo wa kumwondoa kwa kura, na kitakachoendelea kumweka kwenye nafasi hiyo ni imani potofu ya kibaguzi ya wapiga kura wa upande wake. Lakini kuna jamaa hapa ofisini tulikuwa tunajadiliana kabla sijaweka hii thread hapa (yeye kwao ni Kibosho) anasema Chami kafanya makubwa sana kule Kibosho kwa hiyo wanampenda kwa dhati. Sijapata wa kushuhudia kuhusu mambo ambayo Chami ameyafanya kule Uru, pengine itasaidia kuweka balance.
 
Mi naona mnatuboa tu na hayo majadiliano yenu, najua CHADEMA sio ya hivyo, hizo tofauti zenu kazijadilini December mkienda kula X-MAS hapa naona kama sio mahali pake vile au?
 
Mbona haya maneno ya ukabila mnayotoa hayaendani kabisa na hali halisi iliyokuwa jimboni moshi mjini? Hakukuwa na ukabila wowote, hakukuwa na uuru wala ukibosho pale, Komu mwenyewe alijiharibia kwa kuleta mambo ya ubabe na vurugu katika kampeni, nasikitika Komu ndiye aliyetukkosesa Chadema lile jimbo, alishindwa kwa kiasi kikubwa kutetea sera za Chadema jimboni mwake
 
Hii imedhihirisha matumizi mabaya ya majority vote, voting for all the wrong reasons! Ubaguzi wa aina hii ni hatari sana. Maana yake ni kuwa hao wauru hata wasiporidhika na mbunge Chami bado hawana uwezo wa kumwondoa kwa kura, na kitakachoendelea kumweka kwenye nafasi hiyo ni imani potofu ya kibaguzi ya wapiga kura wa upande wake. Lakini kuna jamaa hapa ofisini tulikuwa tunajadiliana kabla sijaweka hii thread hapa (yeye kwao ni Kibosho) anasema Chami kafanya makubwa sana kule Kibosho kwa hiyo wanampenda kwa dhati. Sijapata wa kushuhudia kuhusu mambo ambayo Chami ameyafanya kule Uru, pengine itasaidia kuweka balance.

Mhhh nahofia mjadala kama huu ukiachiwa kuendelea hatutakuwa na Chadema kama ilivyo hapo 2015. Nafikiri kwa majimbo iliyoyapata Chadema imezidi kujipambanua kuwa si chama cha KICHAGA kwa maana ya kanda ya Moshi na Arusha, na hii hali imewasuta wale wote walopaza sauti na kusema Chadema inanuka ukabila. Leo hii Chadema ina wabunge kona zote za Tanzania, Toka Mbeya hadi Kilimamjaro, Dar hadi Kigoma na mwanza. Kwa mijadala kama hii ya Ukibosho na Uuru haitusaidii ni lazima tuisitishe kabisa kwa manufaa ya chama chetu.
 
Mbona haya maneno ya ukabila mnayotoa hayaendani kabisa na hali halisi iliyokuwa jimboni moshi mjini? Hakukuwa na ukabila wowote, hakukuwa na uuru wala ukibosho pale, Komu mwenyewe alijiharibia kwa kuleta mambo ya ubabe na vurugu katika kampeni, nasikitika Komu ndiye aliyetukkosesa Chadema lile jimbo, alishindwa kwa kiasi kikubwa kutetea sera za Chadema jimboni mwake
Ni Moshi vijijini
 
Mhhh nahofia mjadala kama huu ukiachiwa kuendelea hatutakuwa na Chadema kama ilivyo hapo 2015. Nafikiri kwa majimbo iliyoyapata Chadema imezidi kujipambanua kuwa si chama cha KICHAGA kwa maana ya kanda ya Moshi na Arusha, na hii hali imewasuta wale wote walopaza sauti na kusema Chadema inanuka ukabila. Leo hii Chadema ina wabunge kona zote za Tanzania, Toka Mbeya hadi Kilimamjaro, Dar hadi Kigoma na mwanza. Kwa mijadala kama hii ya Ukibosho na Uuru haitusaidii ni lazima tuisitishe kabisa kwa manufaa ya chama chetu.
Ni kweli unachosema, CHADEMA ni chama cha kitaifa, na uchaguzi wa mwaka huu ni ushahidi. Kinachozungumzwa hapa si tatizo la CHADEMA, ni tatizo la hawa wajomba zangu wachaga kubaguana kwa hoja zisizo na tija. Hawa jamaa wanabaguana hivyo kila mahali, kwenye CCM, vyama vingine, kanisani popote lazima mtu aulizwe kwanza ni mchaga wa wapi kabla ya chochote kufuata, na jibu lake ndilo linaloamua kiwango cha kukubalika kwake. Naomba nieleweke, sizungumzii tatizo la CHADEMA hapa.
 
Me naona hakuna ukabila wala ubaguzi...pia hakuna kampeni za kibabe zilizoendeshwa na komu...huku moshi vijijini watu wanampenda komu..mf:ni mwaka 2005 wamama wa kibosho walimkinga komu na vurugu wakati wa kampeni....na kuongeza me nilickia matokeo ya awali ktk vituo vya kupigia kura na kulikuwa na dalili ya komu kushinda.....me nadhani mbinu iliyotumiwa na hawa SISIEM ni ile ya uchakachuaji tu kama kule Ukonga na sehemu nyingine nyingi........hapo hakuna ukabila.
 
komu fisadi wa chadema anayekwapua ruzuku na mbowe. slaa awe mwenyekiti na kaka zitto katibu yule wa mpanda makamu na pateni kiongozi mzuri zanzibari

moshi werevu vunjo wamemchagua shujaa wangu mrema

Hapo kwenye nyekundu umechemsha!!
 
wakuu mbona hii post inakizana na moja iyokuwa hapa jamvini kuwa mh komu kachakachuliwa?Au ndo mbinu za kutusahaulisha,tusahau kujadili kuchakachuliwa tuongelee ushabiki wa kikanda?
Binafsi si amini kama pana ubaguzi wakiwango hicho unless m2 ataje ushahidi usio na mashaka.
NAWAKILISHA.
 
eeeeh napita mimi ila chami yupo vizuri ngawaiya alipewa mwisho wa siku akatapeli wa2
 
Chami amefukuzwa kazi yeye na Ekerege kwa kashfa ya rushwa.Wachaga bora ufukuzwe kazi kwa kuiba kuliko kupokea vijisenti
 
Back
Top Bottom