Wachaga na ubaguzi wao! Hii nimeisikia kabla ya uchaguzi, watu wakidai hawatakubali kuwakilishwa na mtu kutoka Uru! Na imekuwa hivyo kweli. Sina uhakika kama matokeo haya ya uchaguzi yametokana na kampeni za aina hiyo maana sijafika Moshi kipindi chote cha kampeni na uchaguzi. Lakini kwa uzoefu wangu wa jinsi hao jamaa wa Uru wanavyodharauliwa na wachaga wenzao, naanza kuamini kuwa kuna ukweli katika kauli waliyokuwa wanamwambia kuwa 'subiri mpate jimbo lenu la Uru'. Kama Pemba na Unguja. Wajomba zangu (precisely wajomba wa babangu) kule Hai wamemchagua Mbowe, nawapongeza, labda kwao hawajachakachuliwa (hakuna factor tofauti na umachame). Kule Moshi vijijini factor ya u-Uru na u-Kibosho ina nguvu kuliko sera. What a shame!