Anthony Komu, (CHADEMA): Kususia uchaguzi si sahihi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana ukikosea unajisahihisha

Jamaa ana akili kuliko mwenyekiti wake.

CHADEMA mpeni KOMU uenyekiti tafadhari.

Ila kususia kwa uchaguzi kuna habari za chini ya kapeti kwamba jamaa wamekombaa ruzuku kwenye akaunti.
 
Komu anataka kurudi ccm na taarifa hizi zipo siku nyingi, kwanza tangu amekuwa mbunge wa Moshi vijijini hajawahi kuonekana jimboni kwake kabisa! hata kushukuru hajawahi na anajua hatakiwi kabisa hata kwa dawa! pambaf zake aende tu hatutaki mizigo.
Baada ya kuongea ukweli ndio unataka kumchafua? Kubalini kuambiwa ukweli ili chama kisonge mbele
 
Sii ni ninyi chichim mmemwambia aandike hivyo Kom haoni yaliyotokea unacheza mchezo ambao Refa ni wao lainisman ni wao uwanja ni wao polisi ni wao hiyo haki utaipatia wapi we Kom.
 
Yaani sasa hivi CCM wataachwa watupie madogo yao yoooote majukwaani huku CHADEMA na vyama vingine wamejikunyata pembeni kama yatima. This is a very wrong move. Kununanuna na kususa ni tabia ya ajabu sana, hata wanawake walishashtuka.
 
..ni kweli kabisa...kususia uchaguzi ni ujinga na ukondoo wa hali ya juu....yani wameamua kuwapa ccm ubunge wa chee....inasikitisha mno....alafu watakuja 2020 wasemeje kwenye uchaguzi???...yani badala ya kupambana na ccm kwenye kampeni alafu walinde kura wao wanasuasa???..hii inawasaidiaje.???yani wanawanyima wananchi haki yao kuwachagua alafu wategemee nini??...huu upinzani tz Una walakini....wamejaa ubinafsi mno viongozi wa upinzani...ndio maana hata suala la kuungana kwao ni gumu mno kila wakati....
 
Chadema hata lama hakuna fedha changisheni. Tutswachangia ili muende tu hata ccm wakiiba lakini wahenye.
 
Sipingi mtazamo wa Komu ni haki yake kikatiba kutoa maoni yake. Ila akatafute wapiga kura wake walioko tayari kugeuzwa vilema ili yeye apate cheo. Kwa kuanzia atoe pesa za kutibiwa hao wote waliopata majeraha kwenye unyama wa uchaguzi.
Kauli yako inaashiria ukimpinga mwenyekiti lazima ukumbane na janga baya!
 
UVCCM mmepanic sana baada ya ukawa kugomea uchaguzi mnasema ukawa waingie kwenye uchaguzi wapambane ? Hivi una akili wewe wapambane na Police na NEC na CCM ,bora hata basi wangekua wanapambana afu mnaheshimu kura za wananchi, tatzo CCM mpaka mmeagiza wakurugenzi wasitangaze wapinzani wakishinda, so usifananishe mfalme daudi na upuuzi wa CCM
Kwa hiyo Komu ni Uvccm?
 
Kauli yako inaashiria ukimpinga mwenyekiti lazima ukumbane na janga baya!

Acha Komu hata Mbowe sasa hivi hapeleki mtu kupiga kura ya amani. Akitaka aandae hela za matibabu na sanda, vinginevyo agawe silaha tuende kwenye uchaguzi.
 
Comrade Komu,uko sahihi 100%. Ukianguka uchaguzi huu,unabaini mapungufu,unajipanga kwa ujao.
 
NI KOSA KUBWA LA KIUFUNDI KUSUSIA UCHAGUZI.

Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.

Katu hutakiwi kususia uchaguzi katika mazingira kama haya. Badala yake unatakiwa kushiriki tena kuliko ulivyoshiriki huko nyuma.

Nenda kwa watu. Waeleze. Waambie hayo yaliyokufanya ususie. Waeleze hayo matatizo unayopitia sasa. Washitaki kwa wananchi hao unaosema wanakiuka miiko ya demokrasia na sheria.

Kwanini ususie uchaguzi. Je utasusia mpaka lini, utasusia huu wa marudio tu, au hata ule wa 2020, au hata zaidi ya hapo. Mpango wa kususia ukomo wake ni lini.

Unasema hushiriki kwasababu uchaguzi wa madiwani ulivurugwa hivyo unahitaji ;
a) Mjadala kuhusu kilichotokea.
b) Marekebisho ya sheria za uchaguzi.
c ) Marudio ya uchaguzi kata ulipovurugwa
d ) Ikiwezekana na katiba mpya, nk, nk

Unasema haya mpaka yatekelezwe ndio ushiriki uchaguzi. Niambie sasa, unaona dalili zozote kwa haya kutekelezwa kwa siku za hivi karibuni. Kama hakuna dalili una mpango gani na chaguzi zijazo na hatima ya chama chako.

Kama mgomo huu utaendelea basi ndio mwisho wa Chadema. Nilidhani kwakuwa mikutano ya siasa imezuiwa basi chaguzi hizi ni nafasi ya pekee na adhimu ya kuhuisha uhai wa chama. Ni nafasi pekee ya kupulizia roho kwenye kifua cha chama ili kiondoke katika ufu.Badala yake mnasusa ! ?.

Tizama hapa, msiige muungano wa NASA kenya. Tofauti yenu na hawa ni kuwa hawa hawakususia uchaguzi tu bali pia walisusia shughuli za kiuchumi.

Waliamrisha wafuasi wao kususia huduma zote zinazotolewa na makampuni yenye uhusiano na muungano wa Jubilee. Ninyi hili hamliwezi kwakuwa ushawishi wenu kwa wafuasi wenu haujafika kiwango hiki.

Ni juzi tu kampuni ya Safaricom yenye uhusiano mkubwa na Jubilee imeitisha press ikiomba maridhiano ya siasa kwakuwa mapato yameshuka isivyo kawaida.

Na makampuni mengi yanalalamika na kutokana na hilo tayari kuna tetesi za mazungumzo ya maridhiano kuanza. Huku ndio kususia. Sio unasusia halafu unabaki kutizama siasa kwenye taarifa za habari. My friend, you are finished.

Kususia kwa mtindo wenu ni wazo la kipuuzi kabisa kuliko mawazo yote ya kiharakati na kisiasa ambayo mmewahi kuyabuni takribani kwa miongo miwili. Na sababu i-wazi. Upande wenu hakuna athari chanya yoyote inayotokana na kususia zaidi ya kuiimarisha CCM. Chama hususa ili kifaidike na sio kifaidishe chama hasimu.

Sikilizeni, hebu acheni utoto. Shirikini chaguzi na hayo mnayolalamikia nendeni mkawaeleze watu huko wanakusubirini.

Sikilizeni tena, hayo mnayoyasubiri yafanyike eti ndio muanze kushiriki uchaguzi nakuhakikishieni hakuna wa kuyafanya kwasasa. Nyie wenyewe mnajua kabisa. Na kwa tafsiri hii maana yake mmeacha siasa kabisa kipindi hiki. Na kama mnaacha siasa CDM inageuka kuwa NGO ya haki za binadamu.

Yes, tofauti kubwa ya NGO za haki za binadamu na chama cha siasa ni chaguzi. Chama hushiriki na NGO haziruhusiwi kushiriki kuwa na mgombea. Ila mengine yote ya kupigania utawala wa sheria, utawala bora,hali ya uchumi, haki za kiraia nk wote hushiriki. Basi msiwe NGO.

Na kama msimamo wenu utakuwa huu all over, basi mwisho wa CHADEMA uliokuwa ukisubiriwa ni huu.
 
Naunga mkono hoja Mkuu. Chadema watafakari kwa kina kuhusu hili na wabadili mwelekeo haraka sana vinginevyo uamuzi huo ni sawa na kujichimbia kaburi.

Ameongea jambo sahihi sana. Hiyo susasusa yao haitawaongezea chochote kile na watanzania ndiyo hawa kama wanavyojulikana, ni watu wa kupelekwa na upepo na matukio siyo watu wa misimamo.
Halafu wanaposusa next plan yao ni ipi? CHADEMA na UKAWA wamebugi vibaya sana. Sijui walijufungia kufanya nini kwenye hiyo kamati kuu.
Wenye influence na effects ndiyo huwa wanasusa tena dhidi ya upande unaojali, lakini si katika mazingira haya. Hii ni vita.

Kingine siioni siku hizi ile CHADEMA iliyokua ikitoa shutuma au malalamiko huku ikinukuu na kufanya marejeo kwenye vifungu vya Katiba. CHADEMA ya sasa si ya watu wa kusoma maandishi, CHADEMA ya sasa inakaa vikao ikilipana posho halafu inakuja na matamko ya hovyo yanayowapa mzigo walaji wa taarifa ili kuzitafutia maumbo mazuri ili yalete maana.
 
You can't enter a boxing competition with your hands tied. Abandoning mid election is a very valid protest against obvious election misconduct in earlier ward elections
 
CHADEMA haishiriki uchaguzi kwa sababu pesa ya ruzuki inalipa madeni ya uchaguzi mkui kwa Mbowe na nyingine inalipa fadhila kwa Lowassa kwa kuleta wabunge wengi CDM. Baada ya malipo hayo kinachobaki ........
 
Ameongea jambo sahihi sana. Hiyo susasusa yao haitawaongezea chochote kile na watanzania ndiyo hawa kama wanavyojulikana, ni watu wa kupelekwa na upepo na matukio siyo watu wa misimamo.
Halafu wanaposusa next plan yao ni ipi? CHADEMA na UKAWA wamebugi vibaya sana. Sijui walijufungia kufanya nini kwenye hiyo kamati kuu.
Wenye influence na effects ndiyo huwa wanasusa tena dhidi ya upande unaojali, lakini si katika mazingira haya. Hii ni vita.

Kingine siioni siku hizi ile CHADEMA iliyokua ikitoa shutuma au malalamiko huku ikinukuu na kufanya marejeo kwenye vifungu vya Katiba. CHADEMA ya sasa si ya watu wa kusoma maandishi, CHADEMA ya sasa inakaa vikao ikilipana posho halafu inakuja na matamko ya hovyo yanayowapa mzigo walaji wa taarifa ili kuzitafutia maumbo mazuri ili yalete maana.
Umeongea point sana,hasa aya ya mwisho.
 
Kwanza naomba ieleweke kwa wana ccm kwamba yale sio maamizi ya Mbowe , inawezekana kabisa hata mbowe alitaka kushiriki lakini kamati kuu ilimpinga na kuja na common solution ya kutoshiriki uchaguzi huu mdogo. Sasa nyie wanaccm mnaosema komu kapingana na Mbowe mna ajenda zenu za siri. Komu anapingana na mawazo ya kamati kuu.
Kupingana kupo kwenye taasisi ila lazima mwisho wa siku kukubaliana mawazo ya wengi , inawezekana kabisa ndani ya kamati kuu wapo waliotaka kushiriki ila wapo pia waliokataa, sasa kama waliokataa walishinda huna budi kuwaunga mkono. Sasa unatoka nje na kuanza kuropoka oooh sijui nini, huo sio uongozi.

Katika maisha yako mambo mangapi wenzako walikupinga na ukakubali mawazo yao na mambo yakaenda. Je ulilazimisha wazo lako tu ndo litimizwe? Tuheshimu mawazo ya wengine , tuheshimu mawazo ya kamati kuu, tuheshimu watu waliojela, walioteseka , walioumizwa , waliopoteza Mali zao na waliopoteza maisha kwa sababu ya kupigania haki kipindi cha uchaguzi wa madiwani.
Yeye komu yangemkuta yaliowakuta wabunge wa kilombero na wanachama wao au meya wa Iringa asinge ropoka ujinga nje ya vikao vya ndani
Hujui kitu. Unaongozwa na hisia tu
 
Back
Top Bottom