Anthony Komu, (CHADEMA): Kususia uchaguzi si sahihi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana ukikosea unajisahihisha

'It's possible for a smart or clever person to deceive, confuse or cheat people most of the time but not God even for once. We need to be careful because we shall meet with reality one day. Mh. Mbunge nakubaliana na wazo lake tusiwe wajinga kwenye nyakati za kutaka kunyamazishana.
Mkuu na wewe umeanza kumpinga mwenyekiti wa maisha Mbowe???!!!
 
Huyu KOMU labda ana silaha za moto na jeshi
ili waweze kupambana na upande wa pili.
 
Tumejifunza nini uchaguzi wa Zanzibar!!?

Hata kama macho hatuoni...ubongo wa mbele hatuna!?
 
Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu ametoa msimamo unaotofautiana na ule uliotolewa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuhusu ushiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani.

Kauli ya UKAWA ipo hapa: UKAWA na CHAUMMA wasema hawatashiriki uchaguzi mdogo ujao hadi kasoro zilizojitokeza uchaguzi uliopita zitatuliwe

Komu akizungumza na mwandishi wetu kuhusu uamuzi huo wa Ukawa alisema uamuzi ni halali kwa kuwa umepitia vikao halali, lakini unaweza kujadiliwa.

“Usahihi ni kitu kingine. Hatuko sahihi kususia uchaguzi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana unaonyesha wapi unakosea na kujisahihisha,” alisema mkurugenzi huyo wa fedha wa zamani Chadema.

“Hata hizo kata 43 hatukuonewa kote ndiyo maana tulishinda kata moja tuliyojipanga vizuri, kikubwa tunapaswa kujenga uwezo wetu na kupambana… kama tutasusia je, tumejipangaje kuhakikisha hicho tunachokipigania tutakipata?” alihoji.

Mbunge huyo alisema uamuzi huo unazua maswali mengi kwani CCM itapita katika majimbo yote bila kupingwa... “Watapata jukwaa la kueleza mambo yao sisi hatutapata, lakini je, kama huu hatutashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa mwaka 2020 tutashiriki au la, haya ndiyo maswali yanayohitaji majibu.”

Rejea Kauli ya NEC juu Uchaguzi huo; NEC: Chama cha Siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe! Tume haiko kushawishi chama kushiriki

Chanzo; Mwananchi
Kwani unapotaka kuhama chama ni lazima Azungumze na waandishi wa Habari Ndiyo Maana nasema hivi Vyama vianaendeshwa km (Pressure Groups not political parties) kila mtu ni msemaji wa chama n.k
 
Moja kati ya maajabu ya vikao na maazimio ya chadema ni pale walipokaa kikao na kuja na azimio la operation "ukuta"na "kata funua"halafu unaenda polisi kuomba kibali cha kufanya maandamano yanayoitwa kata funua hata Uingereza hupewi hicho kibali
 
[HASHTAG]#Habari[/HASHTAG]: Mbunge wa Moshi Vijijini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Anthony Komu ametoa msimamo wake unaotofautiana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuhusu kususia uchaguzi wa majimbo matatu unaotarajiwa kufanyika mwakani. Mbowe alisema kuwa kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haitaahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika januari 13 mwakani ili kushiriki majadiliano, hawatashiriki uchaguzi huo, lakini Komu amesema kuwa kufanya hivyo ni kosa kubwa ambalo linaweza kuwaathiri katika chaguzi zijazo.

[HASHTAG]#Myatake[/HASHTAG]
Naungana na Antony Komu.

-Anayetupinga Atuambie Baada ya Ukawa Kususia Uchaguzi Faida gani itapatikana?
579a8b2fe65972cbc8d3090df093317c.jpg
 
komu kahoji mambo ya msingi. uchaguzi wa mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 nao mtasusa?! mbowe yupo tayari kupoteza ruzuku kwa kususa 2020? tricky!
 
Chadema wamesusia vitu vingi lakini hakuna hata kimoja kilichofanikiwa,kazi ya chama cha siasa ni kuleta Sera mbadala,sasa kama upinzani hamshiriki uchaguzi na kazi kubwa ya chama cha siasa ni kushika dola utashikaje dola bila kushiriki uchaguzi???? Zenji walisusia maccm yakapita kiulani
 
Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu ametoa msimamo unaotofautiana na ule uliotolewa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuhusu ushiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani.

Kauli ya UKAWA ipo hapa: UKAWA na CHAUMMA wasema hawatashiriki uchaguzi mdogo ujao hadi kasoro zilizojitokeza uchaguzi uliopita zitatuliwe

Komu akizungumza na mwandishi wetu kuhusu uamuzi huo wa Ukawa alisema uamuzi ni halali kwa kuwa umepitia vikao halali, lakini unaweza kujadiliwa.

“Usahihi ni kitu kingine. Hatuko sahihi kususia uchaguzi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana unaonyesha wapi unakosea na kujisahihisha,” alisema mkurugenzi huyo wa fedha wa zamani Chadema.

“Hata hizo kata 43 hatukuonewa kote ndiyo maana tulishinda kata moja tuliyojipanga vizuri, kikubwa tunapaswa kujenga uwezo wetu na kupambana… kama tutasusia je, tumejipangaje kuhakikisha hicho tunachokipigania tutakipata?” alihoji.

Mbunge huyo alisema uamuzi huo unazua maswali mengi kwani CCM itapita katika majimbo yote bila kupingwa... “Watapata jukwaa la kueleza mambo yao sisi hatutapata, lakini je, kama huu hatutashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa mwaka 2020 tutashiriki au la, haya ndiyo maswali yanayohitaji majibu.”

Rejea Kauli ya NEC juu Uchaguzi huo; NEC: Chama cha Siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe! Tume haiko kushawishi chama kushiriki

Chanzo; Mwananchi
Ili watanzania wasio na hatia wabaki salama bora CHADEMA wasishiriki chaguzi hizo uongozi na madaraka si kitu kuliko uhai wa mtu waachwe tu wajipishe na washinde ili roho za watu zisije walilia, kuna watanzania wamelemaa kwa ajili ya uchaguzi mdogo tu wa juzi na kuna wengine wamezikwa kisa uchaguzi wa madiwan yanini hayo yote?? Waachwe wawe huru ili roho za watanzania zenye mawazo tofauti na chama tawala zibaki salama
 
Chadema wamesusia vitu vingi lakini hakuna hata kimoja kilichofanikiwa,kazi ya chama cha siasa ni kuleta Sera mbadala,sasa kama upinzani hamshiriki uchaguzi na kazi kubwa ya chama cha siasa ni kushika dola utashikaje dola bila kushiriki uchaguzi???? Zenji walisusia maccm yakapita kiulani
Tatizo kushiriki kwao uchaguzi kutaleta maafa na majeraha maana hali ilikiwa yeye mtutu wa bunduki hutumika sasa salama ya watanzania wwnye msimamo tofauti na chama tawala iko wapi ? Inamaana bora kuendelea na uchaguzi ambao taswira inaonesha kabisa kuwa kuna kumwaga damu!? Hapana aisee ili watanzania wasidhurike bora ccm waachwe tu waendelee na uchaguzi huu wakati upinzani wakijipanga namna sahihi ya kuchukua hatua ingawa nao wamekuwa wazito kuchukua hatua kazi yao kulalama tu mitandaoni
 
Suseni bana , kwanza itaokoa fedha za uma, namtafuta zitto nae agome tukaapishe wagombea wetu.
 
Ameongea jambo sahihi sana. Hiyo susasusa yao haitawaongezea chochote kile na watanzania ndiyo hawa kama wanavyojulikana, ni watu wa kupelekwa na upepo na matukio siyo watu wa misimamo.
Halafu wanaposusa next plan yao ni ipi? CJADEMA na UKAWA wamebugi vibaya sana. Sijui walijufungia kufanya nini kwenye hiyo kamati kuu.
Wenye influence na effects ndiyo huwa wanasusa tena dhidi ya upande unaojali, lakini si katika mazingira haya. Hii ni vita.

Kingine siioni siku hizi ile CHADEMA iliyokua ikitoa shutuma au malalamiko huku ikinukuu na kufanya marejeo kwenye vifungu vya Katiba. CHADEMA ya sasa si ya watu wa kusoma maandishi, CHADEMA ya sasa inakaa vikao ikilipana posho halafu inakuja na matamko ya hovyo yanayowapa mzigo walaji wa taarifa ili kuzitafutia maumbo mazuri ili yalete maana.
1. Mbowe.
2.John Mrema
3. Reginald Munisi
Hawa ndio think tank ya Chama. Hawana hela. Uchaguzi umekuja kama surprise na hawana means yoyote ya kupata hela.

Wanasingizia demokrasia. Hakuna uchaguzi ambao haukuwa na vurugu. Iringa Mwangosi aliuawa, Morogoro Ally Zona, Igunga Mbwana Masoud na wengine, CCM wao waliumiziwa Tesha, Arumeru Mbwambo.

Haka kakikundi Kanataka kula hela tu ila kuumia hapana! Wanachama na viongozi wa ngazi za chini wana wajibu wa kuwahoji.

Nimekuwa nikisema Mwenyekiti anadanganywa, anatishwa, anafitinishwa na kulishwa majungu. Shauri yake akikumbuka shuka kumekucha.
 
Mbowe na siasa togwa. " ukitaka mambo yako yakunyokee ingia CCM" - Mr. Zero.
 
Kwanza naomba ieleweke kwa wana ccm kwamba yale sio maamizi ya Mbowe , inawezekana kabisa hata mbowe alitaka kushiriki lakini kamati kuu ilimpinga na kuja na common solution ya kutoshiriki uchaguzi huu mdogo. Sasa nyie wanaccm mnaosema komu kapingana na Mbowe mna ajenda zenu za siri. Komu anapingana na mawazo ya kamati kuu.
Kupingana kupo kwenye taasisi ila lazima mwisho wa siku kukubaliana mawazo ya wengi , inawezekana kabisa ndani ya kamati kuu wapo waliotaka kushiriki ila wapo pia waliokataa, sasa kama waliokataa walishinda huna budi kuwaunga mkono. Sasa unatoka nje na kuanza kuropoka oooh sijui nini, huo sio uongozi.

Katika maisha yako mambo mangapi wenzako walikupinga na ukakubali mawazo yao na mambo yakaenda. Je ulilazimisha wazo lako tu ndo litimizwe? Tuheshimu mawazo ya wengine , tuheshimu mawazo ya kamati kuu, tuheshimu watu waliojela, walioteseka , walioumizwa , waliopoteza Mali zao na waliopoteza maisha kwa sababu ya kupigania haki kipindi cha uchaguzi wa madiwani.
Yeye komu yangemkuta yaliowakuta wabunge wa kilombero na wanachama wao au meya wa Iringa asinge ropoka ujinga nje ya vikao vya ndani
 
Komu anataka kurudi ccm na taarifa hizi zipo siku nyingi, kwanza tangu amekuwa mbunge wa Moshi vijijini hajawahi kuonekana jimboni kwake kabisa! hata kushukuru hajawahi na anajua hatakiwi kabisa hata kwa dawa! pambaf zake aende tu hatutaki mizigo.
 
No free and fair electoral commission no election than dramma from the actors. Period

Hakuna uchaguzi na wapinzani wasishiriki dhambi hii anymore if no free and fair electoral commission, kwani kilichotokea siku za nyuma inatosha kabisaaa.

Wawaache ccm watawale milele kama wazanivyo na watakavyo.
 
mimi pia napingana na chadema kususia chaguzi...
twende kwenye chaguzi kama wakileta fujo na sisi tuwape fujo... wakiona tunawaka hapo ndio watakubali tuongee na ha[po ndio tutawapa malalamiko yetu na wayatekeleze
uko tayari kukaa mbele kabisa kupambaa na polisi?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom