Anthony Komu, (CHADEMA): Kususia uchaguzi si sahihi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana ukikosea unajisahihisha

Nashukuru kumbe kuna wabunge wanaojitambua CHADEMA, achelewi kuitwa msaliti kwa kusimamia ukweli.Huyu Mbowe ndo anaizika CHADEMA hivi hivi mnajiona ebu wanachama wake mjiongeze.
 
Woga ni dhambi, Ufunuo 21:8....waingie wapambane...hakuna mwoga aliyewahi kuwa shujaa....Mfalme Daudi hakuogopa ukubwa wa Goliath na wasifu wake alioupata kwa Sauli bali yeye aliamini kuwa ujasiri wa kumtegemea Mungu ndio ushindi, naye akashinda.sasa UKAWA wanasema walianza na Mungu na watamaliza na Mungu...iweje waogope...wanamdhalilisha Mungu, acheni woga maana ni dhambi...Vaeni ujasiri katika kumtegemea Mungu, mtamuangusha Goliath bila hivyo hamtafanikiwa kabisa...mwishio hamtakubali kwa wananchi.

UVCCM mmepanic sana baada ya ukawa kugomea uchaguzi mnasema ukawa waingie kwenye uchaguzi wapambane ? Hivi una akili wewe wapambane na Police na NEC na CCM ,bora hata basi wangekua wanapambana afu mnaheshimu kura za wananchi, tatzo CCM mpaka mmeagiza wakurugenzi wasitangaze wapinzani wakishinda, so usifananishe mfalme daudi na upuuzi wa CCM
 
Ameongea jambo sahihi sana. Hiyo susasusa yao haitawaongezea chochote kile na watanzania ndiyo hawa kama wanavyojulikana, ni watu wa kupelekwa na upepo na matukio siyo watu wa misimamo.
Halafu wanaposusa next plan yao ni ipi? CJADEMA na UKAWA wamebugi vibaya sana. Sijui walijufungia kufanya nini kwenye hiyo kamati kuu.
Wenye influence na effects ndiyo huwa wanasusa tena dhidi ya upande unaojali, lakini si katika mazingira haya. Hii ni vita.

Kingine siioni siku hizi ile CHADEMA iliyokua ikitoa shutuma au malalamiko huku ikinukuu na kufanya marejeo kwenye vifungu vya Katiba. CHADEMA ya sasa si ya watu wa kusoma maandishi, CHADEMA ya sasa inakaa vikao ikilipana posho halafu inakuja na matamko ya hovyo yanayowapa mzigo walaji wa taarifa ili kuzitafutia maumbo mazuri ili yalete maana.
Naunga mkono hoja. Mbowe kapoteza mwelekeo kabisa, naona anataka kurudi rasmi kufanya biashara zake. Akiache chama kwa watu watakaoendana na siasa za sasa za Tanzania (ambazo ni za kijima kwa mujibu wa siasa za kimataifa).
 
Ni sahihi kabisa Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani kuomba busara kwa Tume; ametimiza wajibu wake na kwa hilo tunampa Big UP!

Ila kwa kuwa Tume imejitoa ufahamu na kusema kama UKAWA wanaona walionewa waende mahakamani huku akigoma hata kupata chembe ya ushahidi kwamba kanuni / taratibu za uchaguzi zilikiukwa waziwazi na kwa makusudi kabisa - Basi wandugu hatuna namna - TWENDENI KAZINI KUKAPAMBANE.

Maana huu hautakuwa uchaguzi bali itakuwa Gharika, Tunakwenda kucheza mchezo ambao hauna refa wala kamisaa.
 
Nawaandikia wapinzani, yaani vyama vyote vya upinzani hapa Tanzania vikiongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Nawasihi kuwa wasithubutu kususia uchaguzi wowote utakaosimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC). Nasema kwa uwazi na uthabiti kuwa kususia uchaguzi ni kujimaliza kabisa. Hatupendi iwe hivyo!

Dunia nzima, hakuna mahali ambapo vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi na uchaguzi husika kutofanyika. Inafahamika kuwa ni kazi pevu, dunia nzima, vyama vya upinzani kupambana uchaguzini na hata siasani na chama tawala. Sababu kuu ni mbili. Mosi, chama tawala ndicho kinachounda Serikali. Hivyo, vyombo vya dola 'huwa karibu' na mtawala.

Pili, chama tawala hakipangi wala kupenda kutoka madarakani. Hufanya kila njia ya kisiasa kubakia madarakani. Siasa, ingawa mimi si mwanasiasa, ni pamoja na mbinu, ubunifu na kuthubutu. Siasa ni mapambano ya kupambania kuongoza Serikali. Harakati zake, tangu zianze hamsini kweusi, hazijawahi kuisha. Harakati za kisiasa za kimapambano hazisusiwi. Huendelezwa.

Wapinzani wapambane kadiri ya uwanja na nafasi iliyopo. Kama mikutano imekatazwa, tumieni media kufikisha ujumbe wenu. Wananchi wakielewa mnachokisimamia watawasaidia kusimamia hoja zenu. Mabadiliko yote ya kisheria na kimfumo yatakuwa rahisi kupatikana. Hakuna ubishi mkubwa kuwa mfumo mzima wa uchaguzi wa Tanzania, ikiwemo Tume ya Uchaguzi, una dosari.

Kwa mfano, uchaguzi ngazi ya Majimbo na Kata kusimamiwa na wateule wa Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama tawala ni dosari kubwa. Ushindi kwa wapinzani, katika mazingira hayo, ni kama ngamia kupenya kwenye tundu ya sindano. Wapinzani husambaratishwa hata kwa mapingamizi na vigisu za kuchelewa kurejeshwa kwa fomu za wagombea.Hatahivyo, wapinzani hushinda.

Hakika, kuna hoja za kidemokrasia za kuzifanyia kazi katika kufanya siasa na wakati wa uchaguzi. Lakini, kususia zi njia sahihi. Njia itakiwayo ni kuendeleza mapambano uchaguzini huku changamoto zikibebwa na kuelezwa kila uchao kwa namna mbalimbali. Hatimaye, mambo yatakuwa na nafuu. Lakini, kwa nchi nyingi za dunia hii, upinzani haukuwahi kucheza fair game na chama tawala. Ingawa wapo wapinzani walioibuka washindi.
 
Mnataka wangapi waumizwe au wafe ndio mjue Tanzania hakuna uchaguzi ni vita.
FB_IMG_1513042210692.jpg
 
Ameongea jambo sahihi sana. Hiyo susasusa yao haitawaongezea chochote kile na watanzania ndiyo hawa kama wanavyojulikana, ni watu wa kupelekwa na upepo na matukio siyo watu wa misimamo.
Halafu wanaposusa next plan yao ni ipi? CJADEMA na UKAWA wamebugi vibaya sana. Sijui walijufungia kufanya nini kwenye hiyo kamati kuu.
Wenye influence na effects ndiyo huwa wanasusa tena dhidi ya upande unaojali, lakini si katika mazingira haya. Hii ni vita.

Kingine siioni siku hizi ile CHADEMA iliyokua ikitoa shutuma au malalamiko huku ikinukuu na kufanya marejeo kwenye vifungu vya Katiba. CHADEMA ya sasa si ya watu wa kusoma maandishi, CHADEMA ya sasa inakaa vikao ikilipana posho halafu inakuja na matamko ya hovyo yanayowapa mzigo walaji wa taarifa ili kuzitafutia maumbo mazuri ili yalete maana.

Anajulikana hana muda mrefu anaenda kumuunga mkono Sizonje nani asiyejua
 
Nawaandikia wapinzani, yaani vyama vyote vya upinzani hapa Tanzania vikiongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Nawasihi kuwa wasithubutu kususia uchaguzi wowote utakaosimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC). Nasema kwa uwazi na uthabiti kuwa kususia uchaguzi ni kujimaliza kabisa. Hatupendi iwe hivyo!

Dunia nzima, hakuna mahali ambapo vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi na uchaguzi husika kutofanyika. Inafahamika kuwa ni kazi pevu, dunia nzima, vyama vya upinzani kupambana uchaguzini na hata siasani na chama tawala. Sababu kuu ni mbili. Mosi, chama tawala ndicho kinachounda Serikali. Hivyo, vyombo vya dola 'huwa karibu' na mtawala.

Pili, chama tawala hakipangi wala kupenda kutoka madarakani. Hufanya kila njia ya kisiasa kubakia madarakani. Siasa, ingawa mimi si mwanasiasa, ni pamoja na mbinu, ubunifu na kuthubutu. Siasa ni mapambano ya kupambania kuongoza Serikali. Harakati zake, tangu zianze hamsini kweusi, hazijawahi kuisha. Harakati za kisiasa za kimapambano hazisusiwi. Huendelezwa.

Wapinzani wapambane kadiri ya uwanja na nafasi iliyopo. Kama mikutano imekatazwa, tumieni media kufikisha ujumbe wenu. Wananchi wakielewa mnachokisimamia watawasaidia kusimamia hoja zenu. Mabadiliko yote ya kisheria na kimfumo yatakuwa rahisi kupatikana. Hakuna ubishi mkubwa kuwa mfumo mzima wa uchaguzi wa Tanzania, ikiwemo Tume ya Uchaguzi, una dosari.

Kwa mfano, uchaguzi ngazi ya Majimbo na Kata kusimamiwa na wateule wa Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama tawala ni dosari kubwa. Ushindi kwa wapinzani, katika mazingira hayo, ni kama ngamia kupenya kwenye tundu ya sindano. Wapinzani husambaratishwa hata kwa mapingamizi na vigisu za kuchelewa kurejeshwa kwa fomu za wagombea.Hatahivyo, wapinzani hushinda.

Hakika, kuna hoja za kidemokrasia za kuzifanyia kazi katika kufanya siasa na wakati wa uchaguzi. Lakini, kususia zi njia sahihi. Njia itakiwayo ni kuendeleza mapambano uchaguzini huku changamoto zikibebwa na kuelezwa kila uchao kwa namna mbalimbali. Hatimaye, mambo yatakuwa na nafuu. Lakini, kwa nchi nyingi za dunia hii, upinzani haukuwahi kucheza fair game na chama tawala. Ingawa wapo wapinzani walioibuka washindi.
Hadi leo watu bado wako hospitali wanauguza vidonda wengine wamevunjika miguu utakuwa na busara kuingia uchaguzi mwingine? ili uongeze majeruhi au?

Haiingii akilini wewe unaenda kwenye kampeni wakati kuna wafuasi wengine huko Maswa bado wako mahabusu kwa sababu ile ile na polisi au NEC don't care about it.

Au mnataka kuumiza wengine kama hawa....busara ni muhimu.

diwan.jpg
FB_IMG_1513042210692.jpg
 
He has a point, waswahili wanasema ww ukisusa wenzio twala, mbowe na wenzie waache kulialia cha msingi ni kubadili tactics za mapambano sio kwenda kuhubiri amani uwanja Wa vita ndomana wanakufa mapema kama sterling wa picha la kihindi.
 
Kunguru Mjanja Hakuna cha maswali hapo. Uamuzi uliochukuliwa ni mzuri sana kwa mtu ambaye anaona mbali. Vyama hivi viko tayari kushiriki uchaguzi kama dosari zilizooneka zinarekebishwa. Kwa nini tume inakataa kurekebisha dosari hizo.

Tume inafahamu kwamba uchaguzi ukifanyika kwa huru na hadi ccm inaondoka mchana kweupe hilo halina ubishi.

Waambie wafanye kama mzalendo brother makala kule mbeya.Pamoja na kuwa mwenyekiti wa kamati ya usalama alihakikisha uchaguzi unakuwa huru na wahaki ndio maana katikati ya kundi kubwa la CCM chama cha cdm kilipata diwani.
 
mimi pia napingana na chadema kususia chaguzi...
twende kwenye chaguzi kama wakileta fujo na sisi tuwape fujo... wakiona tunawaka hapo ndio watakubali tuongee na ha[po ndio tutawapa malalamiko yetu na wayatekeleze
 
Back
Top Bottom