Anthony Komu, (CHADEMA): Kususia uchaguzi si sahihi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana ukikosea unajisahihisha

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,927
Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu ametoa msimamo unaotofautiana na ule uliotolewa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuhusu ushiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani.

Kauli ya UKAWA ipo hapa: UKAWA na CHAUMMA wasema hawatashiriki uchaguzi mdogo ujao hadi kasoro zilizojitokeza uchaguzi uliopita zitatuliwe

Komu akizungumza na mwandishi wetu kuhusu uamuzi huo wa Ukawa alisema uamuzi ni halali kwa kuwa umepitia vikao halali, lakini unaweza kujadiliwa.

“Usahihi ni kitu kingine. Hatuko sahihi kususia uchaguzi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana unaonyesha wapi unakosea na kujisahihisha,” alisema mkurugenzi huyo wa fedha wa zamani Chadema.

“Hata hizo kata 43 hatukuonewa kote ndiyo maana tulishinda kata moja tuliyojipanga vizuri, kikubwa tunapaswa kujenga uwezo wetu na kupambana… kama tutasusia je, tumejipangaje kuhakikisha hicho tunachokipigania tutakipata?” alihoji.

Mbunge huyo alisema uamuzi huo unazua maswali mengi kwani CCM itapita katika majimbo yote bila kupingwa... “Watapata jukwaa la kueleza mambo yao sisi hatutapata, lakini je, kama huu hatutashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa mwaka 2020 tutashiriki au la, haya ndiyo maswali yanayohitaji majibu.”

Rejea Kauli ya NEC juu Uchaguzi huo; NEC: Chama cha Siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe! Tume haiko kushawishi chama kushiriki

Chanzo; Mwananchi
 
Ameongea jambo sahihi sana. Hiyo susasusa yao haitawaongezea chochote kile na watanzania ndiyo hawa kama wanavyojulikana, ni watu wa kupelekwa na upepo na matukio siyo watu wa misimamo.
Halafu wanaposusa next plan yao ni ipi? CHADEMA na UKAWA wamebugi vibaya sana. Sijui walijufungia kufanya nini kwenye hiyo kamati kuu.
Wenye influence na effects ndiyo huwa wanasusa tena dhidi ya upande unaojali, lakini si katika mazingira haya. Hii ni vita.

Kingine siioni siku hizi ile CHADEMA iliyokua ikitoa shutuma au malalamiko huku ikinukuu na kufanya marejeo kwenye vifungu vya Katiba. CHADEMA ya sasa si ya watu wa kusoma maandishi, CHADEMA ya sasa inakaa vikao ikilipana posho halafu inakuja na matamko ya hovyo yanayowapa mzigo walaji wa taarifa ili kuzitafutia maumbo mazuri ili yalete maana.
 
Anthony Komu yupo sahihi kabisa huwezi kugomea uchaguzi kwa faida ya CCM.
Inatakiwa jumuia za kimataifa wapate nafasi ya wao kushuhudia kama Demokrasia ya kweli ipo Tanzania.

Ni matumaini yangu International Observer watakuwepo kwenye uchaguzi ujao. Ni vyama vya wapinzani kuweka tofauti zao pembeni na kuweka mgombea mmoja
 
Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu ametoa msimamo unaotofautiana na ule uliotolewa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuhusu ushiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani.

Ukawa wamesema kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) haitaahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Januari 13 mwakani ili kuruhusu majadiliano, hawatashiriki uchaguzi huo. Lakini Komu amesema kufanya hivyo ni kosa kubwa linaloweza kuwaathiri katika chaguzi zijazo.

Viongozi wa Ukawa unaoundwa na Chadema, Chauma, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF waliitaka Nec kuahirisha uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido, Songea Mjini na ule wa kata sita ili wadau wapate nafasi ya kujadili kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo kwenye kata 43 vinginevyo hawatashiriki.

Viongozi wa Ukawa; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Mwenyekiti wa Baraza Kuu la CUF, Julius Mtatiro; Kaimu Katibu wa Chauma, Eugene Kabendera na Katibu Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Danda Juju walitoa msimamo huo juzi lakini jana Komu akizungumza na mwandishi wetu kuhusu uamuzi huo wa Ukawa alisema uamuzi ni halali kwa kuwa umepitia vikao halali, lakini unaweza kujadiliwa.

“Usahihi ni kitu kingine. Hatuko sahihi kususia uchaguzi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana unaonyesha wapi unakosea na kujisahihisha,” alisema mkurugenzi huyo wa fedha wa zamani Chadema.

“Hata hizo kata 43 hatukuonewa kote ndiyo maana tulishinda kata moja tuliyojipanga vizuri, kikubwa tunapaswa kujenga uwezo wetu na kupambana… kama tutasusia je, tumejipangaje kuhakikisha hicho tunachokipigania tutakipata?” alihoji.

Mbunge huyo alisema uamuzi huo unazua maswali mengi kwani CCM itapita katika majimbo yote bila kupingwa... “Watapata jukwaa la kueleza mambo yao sisi hatutapata, lakini je, kama huu hatutashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa mwaka 2020 tutashiriki au la, haya ndiyo maswali yanayohitaji majibu.”

Juzi, Mbowe alisema kulikuwa na kasoro nyingi kwenye uchaguzi wa kata 43 ambazo zinahitaji kurekebishwa, lakini mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima katika taarifa yake aliyoitoa jana alisema chama cha siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe.

“Ikitokea vyama vikasusa vyote kushiriki kwenye uchaguzi hapo ndipo unaweza kuahirishwa kwa kuwa hakutakuwa na mgombea,” alisema Kailima.
 
Mbowe wala hawazii demokrasia ,yeye anawazia gharama(mbesa)zitakazo tumika kwenye uchaguzi ambao anahisi hawawezi shinda. Na hapo ndipo akili yake ilipoishia.
Kifupi mbowe hapaswi kubaki kwenye nafas ile ,uwezo wake wote umeshakwisha.
 
Gamba ww ndo unatekeleza agizo la sizonje kujibu mitandaoni ,nenda lumumba kawadanganye uko
 
Haya maccm ukisusia ndo furaha yao mimi naona wapambane tu.

Maccm yenyewe wanaomba hata waendelee kuwa madarakani maisha sasa kususia kwako ndo furaha kwao.

Kususia uchaguzi ilihali tume ya uchaguzi tumeona majibu yao kwamba ili waahilishe uchaguzi ni mpaka vyama vyote viache kushiliki hata kikiwa chama kimoja wenyewe wataandaa uchaguzi!
 
'It's possible for a smart or clever person to deceive, confuse or cheat people most of the time but not God even for once. We need to be careful because we shall meet with reality one day. Mh. Mbunge nakubaliana na wazo lake tusiwe wajinga kwenye nyakati za kutaka kunyamazishana.
 
Mbowe wala hawazii demokrasia ,yeye anawazia gharama(mbesa)zitakazo tumika kwenye uchaguzi ambao anahisi hawawezi shinda. Na hapo ndipo akili yake ilipoishia.
Kifupi mbowe hapaswi kubaki kwenye nafas ile ,uwezo wake wote umeshakwisha.
Wee mbowe humpendi kwa Sababu haongeki ndo maana unamshambulia kiuchumi aonekane anakula ruzuku toka msajiliCCM Mbona humsemi lipumba mrema mbatia cheyo nk the other long time serving chairmen
 
Sipingi mtazamo wa Komu ni haki yake kikatiba kutoa maoni yake. Ila akatafute wapiga kura wake walioko tayari kugeuzwa vilema ili yeye apate cheo. Kwa kuanzia atoe pesa za kutibiwa hao wote waliopata majeraha kwenye unyama wa uchaguzi.
 
Woga ni dhambi, Ufunuo 21:8....waingie wapambane...hakuna mwoga aliyewahi kuwa shujaa....Mfalme Daudi hakuogopa ukubwa wa Goliath na wasifu wake alioupata kwa Sauli bali yeye aliamini kuwa ujasiri wa kumtegemea Mungu ndio ushindi, naye akashinda.sasa UKAWA wanasema walianza na Mungu na watamaliza na Mungu...iweje waogope...wanamdhalilisha Mungu, acheni woga maana ni dhambi...Vaeni ujasiri katika kumtegemea Mungu, mtamuangusha Goliath bila hivyo hamtafanikiwa kabisa...mwishio hamtakubali kwa wananchi.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom