screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,792
- 15,693
Baada ya kuwa nje ya ulingo kwa mwaka mzima, hatimaye bingwa wa ndondi wa uzito wa juu duniani anayeshikilia mikanda ya WBA, WBO na IBF anatarajiwa kurudi tena ulingoni jumamosi hii. Sikuhiyo atakuwa anatetea ubingwa wake dhidi ya mbulgaria Kubrat Pulev ambaye IBF walimrate kama no1 Challenger hivyo pambano hilo ni 'IBF mandatory'.
Pambano hilo kwa AJ ni la kwanza baada ya lile la marudiano dhidi ya Mmexico Andy Ruiz lililofanyika Saudi Arabia mwishoni mwa mwaka jana na kufanikiwa kuirejesha mikanda yake. Rekodi zao ni kama zinavyoonekana pichani, wote wakiwa wamepoteza mara moja; AJ akipoteza dhidi ya Andy Ruiz na Pulev akipoteza dhidi ya W.Klistchko.