Anthony Diallo aomba radhi kwa waliomuelewa vibaya kauli yake ya 'Viongozi waliopita walikuwa na Matatizo ya Akili'

Kijogoodi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,363
2,372
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, bwana Anthony Diallo amewaomba radhi watanzania kwa kauli zake alizozitoa kuwa viongozi wa Serikali waliopita walikuwa na mafaili mirembe.

========

Diallo: Mimi nadhani ufafanuzi unatosha, nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya, kuna kunielewa nilivyomaanisha lakini kuna kunielewa vibaya mtu mwingine akaona nimeleta ukakasi, hiyo ni nature ya binadamu inaweza kutokea kwamba naweza kuelewa kidogo au tofauti na aliyesema.

Mtu anaetafsiri uelewa ni yule anayesikiliza kulingana na principle ya communications, mara nyingi inatokea mtu anaweza akakuelewa vibaya, katika muktadha wa aina hiyo mimi sina shida ya kusema wanisamehe kwasababu nimewapa uelewa ambao sivyo walivyotarajia

Kuhusu akaunti ya mtandao ni Akaunti feki, hiyo post nimeiona sio mimi.

=======

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi ‘kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake.

Dkt. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha.

Ni baada ya jana Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021, kuzungumza masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika utawala wa awamu ya tano akigusia suala la nchi kuongozwa kwa matamko.

Dkt. Diallo aliyewahi kuwa waziri, alizungumza hayo katika kipindi cha Ajenda, kinachorushwa na kituo chake cha televisheni cha Star TV, jijini Mwanza.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata maoni yake juu ya nchi kuongozwa kwa matamko bila kufuata Katiba na sheria, Dk. Diallo alisema, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya mtu kabla ya kupewa dhamana ya kuongoza.

Mimi nafikiri tuwe waangalifu tu katika kuchagua tuwe tuna ‘track record’ kwani huko nyuma tuliwahi kuchagua watu walikwisha kwenda hospitali za vichaa ‘milembe’ harafu unamwachia aongoze nchi, kwa hiyo tuwe makini,” alisema.

Kauli hiyo ilizua mjadala na leo Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, akizungumza na waandishi wa habari amesema “nilifanya kosa kwa kutolea mfano wa wakati uliopita badala ya wakati ujao kuwa tusipokuwa waangalifu tunaweza kuchagua viongozi wenye matatizo ya akili.”

Na sijasema mtu kuwa aliyekuwa na tatizo ila nilikosea tu kwenye maelezo. Nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya kwani wapo waliotafasiri wanavyojua wao,” amesema Dk. Diallo.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini amsema “mimi nadhani tuwe waangalifu sana hasa wana CCM, tumeanza kuingiliwa sana.”

Dkt. Diallo amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kutoa matamko kabla ya kumsikiliza au kumuuliza alikuwa ana maanisha nini.

“Unakuta ni kiongozi wa chama anatoa tamko na kunituhumu kama vile nimefanya kosa, bila hata kuniuliza. Lazima tuwe waangalifu sana wana CCM,” amesema Dkt. Diallo.

Miongoni mwa viongozi waliomshtumu ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi alisema, viongozi walioaminiwa na “chama chetu, na wanakaa katika vikao vya maamuzi, tunawaomba wawe na nidhamu na chama hiki.”

“Chama hiki ni kikubwa kuliko mtu, kwa hiyo mwenyekiti na katibu mkuu wetu, niwaombe sisi kama UVCCM, kauli ile imetuudhi sana, mwenyekiti wa CCM anapozungumza hivyo hapaswi kuungwa mkono.”

Kihongosi aliongeza kwa kusema “kama yeye aliona wanapaswa kwenda milembe hapa anafanya nini, kama ni vikao vya maamuzi yeye ni miongoni na kauli zile kama sisi vijana zinatuvunja moyo.”

Mwanahalisi

Zaidi, soma: Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo ameomba radhi ‘kiaina’ baada ya kauli yake kuzua mjadala ndani na nje ya chama chake.

Dk. Diallo amesema, ametafasiriwa vibaya na baadhi ya watu huku akiwataka wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuwa makini kwani wapo wasiowatakia mema wanatumia mwanya huo kuwachonganisha.

Ni baada ya jana Jumamosi, tarehe 10 Julai 2021, kuzungumza masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika utawala wa awamu ya tano akigusia suala la nchi kuongozwa kwa matamko.

Dk. Diallo aliyewahi kuwa waziri, alizungumza hayo katika kipindi cha Ajenda, kinachorushwa na kituo chake cha televisheni cha Star TV, jijini Mwanza.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata maoni yake juu ya nchi kuongozwa kwa matamko bila kufuata Katiba na sheria, Dk. Diallo alisema, kuna umuhimu wa kuangalia historia ya mtu kabla ya kupewa dhamana ya kuongoza.

“Mimi nafikiri tuwe waangalifu tu katika kuchagua tuwe tuna ‘track record’ kwani huko nyuma tuliwahi kuchagua watu walikwisha kwenda hospitali za vichaa ‘milembe’ harafu unamwachia aongoze nchi, kwa hiyo tuwe makini,” alisema.

Kauli hiyo ilizua mjadala na leo Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, akizungumza na waandishi wa habari amesema “nilifanya kosa kwa kutolea mfano wa wakati uliopita badala ya wakati ujao kuwa tusipokuwa waangalifu tunaweza kuchagua viongozi wenye matatizo ya akili.”

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi

“Na sijasema mtu kuwa aliyekuwa na tatizo ila nilikosea tu kwenye maelezo. Nawataka radhi wale ambao walinielewa vibaya kwani wapo waliotafasiri wanavyojua wao,” amesema Dk. Diallo.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini amsema “mimi nadhani tuwe waangalifu sana hasa wana CCM, tumeanza kuingiliwa sana.”

Dk. Diallo amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kutoa matamko kabla ya kumsikiliza au kumuuliza alikuwa ana maanisha nini.

“Unakuta ni kiongozi wa chama anatoa tamko na kunituhumu kama vile nimefanya kosa, bila hata kuniuliza. Lazima tuwe waangalifu sana wana CCM,” amesema Dk. Diallo.

Miongoni mwa viongozi waliomshtumu ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi alisema, viongozi walioaminiwa na “chama chetu, na wanakaa katika vikao vya maamuzi, tunawaomba wawe na nidhamu na chama hiki.”

“Chama hiki ni kikubwa kuliko mtu, kwa hiyo mwenyekiti na katibu mkuu wetu, niwaombe sisi kama UVCCM, kauli ile imetuudhi sana, mwenyekiti wa CCM anapozungumza hivyo hapaswi kuungwa mkono.”

Kihongosi aliongeza kwa kusema “kama yeye aliona wanapaswa kwenda milembe hapa anafanya nini, kama ni vikao vya maamuzi yeye ni miongoni na kauli zile kama sisi vijana zinatuvunja moyo.”

Chanzo: Mwanahalisi

---
Japokuwa ameomba msamaha, Dkt. Diallo asisamehewe na apewe adhabu kubwa ili iwe fundisho.

Amejua kuwa alifanya fyongo na kuongea pumba. Ili iwe fundisho kwa wanafiki kama Diallo apewe adhabu kali na kutimuliwa kabisa.
 
Baada ya kusema ukweli kuhusu awamu iliyopita jinsi ilivyonyanyasa watu wakiwemo wana-CCM wenyewe, hali hio imewachukiza sana wana CCM ambao walikua wanufaika wa unyanyasaji huo hali iliyopelekea Dr Diallo kuikana kauli yake muda mfupi uliopia.

Tumsamehe tu hakuna binadamu asiyekosea. Hata Magu mwenyewe aliwasamehe watu waliokuwa wanamsema vibaya kwa kejeli alipokua hai kina Nape na January, Makamba Sr, japo wenyewe walikua kwenye plan B.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom