Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Sio sitaki, bali lazima nishangae, vipi wewe hushangai?,
Watu tumeonyeshwa video Musiba amefanya Press Conference Dodoma jana mchana, mara jana hiyo hiyo anakuja kuhudhuria kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakati yeye sio mjumbe!, halafu miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho, kuna mjumbe mmoja anaripoti kwa Ngurumo!,haya hayakushangazi?!.

P.
Source of info can either be formal OR informal....
 
Duh!.
Ngurumo, Ngurumo, Ngurumo...
Hii kali...
Kwanza kwaheri

kisha karibu

Hii ya kwako Ngurumo kali!, yaani wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es Salaam wanaripoti kwako Ngurumo!...
bora umekimbia! maana...

Hata hivyo, kwenye tasnia ya media, hakuna kitu kama MBM, kilichopo ni waandishi wasio ma mipaka, Journalists San Frontiers
P
Amekuacha mbali maana mengi anayoandika yanatokea vile vile,kiatu kina siri nyingi
 
Huyu jamaa anatuonaje eti, kesi ya kubumba wakati audio na video za mbowe akitamka yale zipo na full text!!
Akaenda kuchukua smg na kuwagawia wafuasi wake ili wapambane na polisi? Kuna muda muwe mnatumia akili
 
"haya yote yana mwisho wake" hata hao wanaoteswa/kukandamizwa wana Mungu wao, ni suala la muda tuu, Mungu wao atawatetea
 
Utulishe matango ya shambani kwako sasa.
Very unfortunately, mimi sina shamba la matango, ukiona nimeleta news humu, ujue ama nilikuwepo, ama from first hand informant who was there. Hizi kupata second hand news, unaweza kabisa kulishwa matango pori.
P
 
Very unfortunately, mimi sina shamba la matango, ukiona nimeleta news humu, ujue ama nilikuwepo, ama from first hand informant who was there. Hizi kupata second hand news, unaweza kabisa kulishwa matango pori.
P
p nafikiri Ngurumo nimwandishi mwenzetu mimi na wewe tunalijua hilo tusikazanie si kweli maana anajua madhara yake
 
Very unfortunately, mimi sina shamba la matango, ukiona nimeleta news humu, ujue ama nilikuwepo, ama from first hand informant who was there. Hizi kupata second hand news, unaweza kabisa kulishwa matango pori.
Mkuu kama una taarifa sahihi zimwage ili tulinganishe na matango pori; lakini Bashite na Magu wanaliangamiza taaifa tukiona
 
Inamaana amezipata hizi taarifa akiwa huko ugaibuni? Kama ni hivyo sasa nihatari,nani amemfikishia taarifa za kikao hicho? Kwa kifupi kuna uvujaji mwingi sana wa taarifa kama ni hivyo,haiwezekani mtu yuko ugaibuni akaqeza kudukua siri za vikao hapa kwetuu
Kwani Mange anapata wapi taarifa nyeti ,!!?. Somewhere somehow system not safe. Hata Lema kasema hakuna kinachofanyika na serikali mahali popote au wakati wowote kisichowafikia.
 
Mmmh hii habari ya uongo kabisa

Hii habari ni ya hisia potofu tu haina uhalisia wowote. Hakuna ukweli hata kidogo

Kumbe Ngurumo muongo hivi ? Aiseee
 
Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda, alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.
Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito.

Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Makonda) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.

1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni "majasusi wa Chadema!"

2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.

3. Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na "uchawi."

4. Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.

5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe. Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.

Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!

MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?
b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?
c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?
d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi…. nitawavunja miguu?”
e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?
f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?
h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?

Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.

Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)
Njoo usemee huku sio unakimbia halafu unatuletea porojo za uzushi,wanaume hawakimbii ,ukiambiwa unaleta chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao,utaona umeonewa au ndio nawe unataka uonekana mtu wa muhimu,kumbe ni zero.
 
Nakosa jinsi ya kuandika wether alioandika Ngurumo ni uongo ama Kweli, hali ya nchi ni mbaya. Wazalendo tukubali kusimama tu hawa mbwa wawili lazima tuwaangushe. Hata kwa macho tunaona, alichosema kinasadifu tuyaonayo
 
Uko maporini ulikokimbilia kutakua kuna baridi kubwa sana, unapata ugonjwa wa akili mgando na mawazo poofu
 
Alah! Zawadi ya ukweli ni risasi nyingi eeh! Mbona mmejawa na roho za kikatili kuliko shetani? Kwani mkimjibu kwa njia aliyoitumia hatopata majibu? Ccm kumbukeni hamna hati miliki ya maisha ya wengine kwani uhai wake siyo mali yenu!

Umewahi mno kujibu bila kusoma na kunielewa....

Mimi siyo CCM, sijawahi kuwa wala hata kujaribu kuipenda tu !!

Nisome unielewe, inawezekana tuko pamoja
 
Ngurumo alichobakiza ni kusajiliwa MODERN TAARAB,

Maana kwa uongo huu na propaganda za miaka ya 1940s anazileta Leo

Yaani ngurumo ana taarifa za kiinterejensia ambazo hata kipilimba na Magufuli hana

Hawa wana siasa sijui huwa wanatuoanaje Watanzania?
Taarifa sahihi ni zipi? Ukiweza kuthibitisha kuwa Makonda hakuwa kikaoni muda huo tajwa saa tisa alasiri na ukatuonesha mahali alipokuwa bila chembe ya shaka tutakuamini, ukishindwa tuache kwanza tuamini ya Ngurumo mpaka utulete ushahidi wako.
 
Mkuu Mwanahabari Huru, hoja yangu sio credibility ya Ngurumo, bali informants wake ndio imemlisha matango pori kwa kumtupia fupa lenye sumu, na yeye akaingia mazima!.

p
Infomer wa Ngurumo ni wengi pia hata Heri Kisanduku makapero pia hutoa siri za Naibu Rais Maliyamungu idd Amin Bashite kwenye michepuko na huko ndipo siri husambaa pia ingawa wewe umejipendekeza kwa kuogopa Ujio wa Nissan nyeupe huko kwako mbagala
 
Very unfortunately, mimi sina shamba la matango, ukiona nimeleta news humu, ujue ama nilikuwepo, ama from first hand informant who was there. Hizi kupata second hand news, unaweza kabisa kulishwa matango pori.
P
Hata wewe mbona umelishwa matango feki kwa kudanganywa kuwa Ngurumo hana vyanzo vya Uhakika, wakati Ngurumo ana jopo kubwa la vyombo vya Dola vinavyompatia taarifa zote na pia kuna mpambe toka kwenye kikundi cha uhalifu cha Maliyamungu Bashite humpelekea taarifa zote.
 
Mwanahabari Huru, unajua madhara ya kutoa habari kama hiyo, au hujui? Ukikamatwa kuthibitisha nawe utasema haki na uhuru wako umeingiliwa?

Nimekidharau na kila bandiko lako nitalisoma kwa jicho la tatu.

UPUUZI NA UJINGA. MTU MZIMA HOVYO,
Acha vitisho we bua, unajifanya anajiweza, tena wewe kwako tunapajua endelea kutuudhi tutaanza na wewe.
 
Kuna ushahidi Musiba alihudhuria? Kama ni kweli alihudhuria, shutuma alizozitooa hadharani anawajibika kudhibitisha. Na kwenye kikao cha ulinzi na usalama, ni sehemu sahihi ya yeye kuitwa kuthibisha hayo mazito aliyoyasema kwa kuwa yanagusa usalama wa Taifa.
Hii nchi ina usalama wa taifa au wa ccm??
 
Back
Top Bottom