Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Kuna Evarist Chahali pia...yuko Uingereza, Mange yuko USA baby, Ngurumo finland.....kiufupi ukitaka kuikosoa serkali uhame nchiiiii hahahahahahahaah. cc Miguna
 
Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda, alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.
Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito.

Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Makonda) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.

1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni "majasusi wa Chadema!"

2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.

3. Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na "uchawi."

4. Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.

5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe. Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.

Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!

MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?
b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?
c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?
d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi…. nitawavunja miguu?”
e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?
f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?
h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?

Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.

Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)

Africa tuna taratibu nyingi sana ila moja ya taratibu ambayo imewekwa wakti wa kula ni kwamba ukiwa unakula usiongee, hii ni falsafa ndefu sana ambayo imewekwa kama lugha ya kielelezo cha heshima ila maana yake ni kubwa, wapo walioielewa, wapo wanaoilewa, wapo wasioielewa na wapo ambao wataielewa,
1. Mtu ambaye kwa namna moja au nyingine ananufaika na huu mfumo kazi yake itakuwa ni kupinga mambo yote anayoyaiona yanaikosoa serikali
2. Mtu ambaye ni mvivu wa kufikiria kwa undani atakuwa wa kwanza kutetea huu mfumo,
3. hii inafafanana kidogo na nao.2 Mtu ambaye elimu yake ni ndogo sana, au hakwenda kabisa, uwezo wake wa kuanalyse mambo kwa undani basi atakuwa wa kwanza kupinga.
4. Mtu ambaye ni mwepesi wa kuridhika, mtu ambaye hana exposure yaani hajui wengine wamefika wapi na speed walioyonayo ni ipi kwenye masuala mtambuka kama afya, miundo mbinu, nishati, uchumi kwa ujumla basi mtu huyu atakuwa wa kwanza kupinga sababu uelewa wake uko ndani ya box la Nchi hii.

Lakini niwaambie enyi watu, kuna mambo yanatakea na yanahuzinisha na kukatisha tama sana, ammbo ambayo kizazi cha 1975 na kuendelea hatukuwahi kuyashuhudia kabisa, tumelewa kwa upendo mkubwa, amani ilikuwa imetamalaki, tumelelewa katika misingi ya kukosoana na kujenga, tukiamini hakuna mkamilifu ndani ya dunia, tumekuwa tukiamini katika umoja, tumekuwa tukishuhudia makabuli mengi sana karibu yetu yaliyobeba fikra za ukabila na udini, fikira za ubwanyenye na ubabe, fikra za udictator na ukabaila, tumekuwa tukizungukwa na maneno ya kutiana matumaini hasa nyakati zote zie shida au raha,

kwa sasa nchi yetu imeingiliwa na mdudu, nchi yetu si mahali tena pa amani, tumeanza kuandikwa vibaya kwenye magazeti makubwa sana ndunia, tumeanza kushukiwa na mataifa mengi sana kuhusu ukiukwaji wa haki za bianadamu, tunaona mihimili ya mahakama ikisiginwa, bunge linasiginwa, madaraka ya usalama yanakasimiwa na mtu mmoja, tunaona watu wenye fikra tofauti na wakubwa wanavyonyanyaswa na kuonewa, watu wanasahahu kwamba, madaraka ni ya muda, watu wanasahahu kwamba umiliki wa hii nchi uko katika usawa kwa kila mwanachi, kinachotutengenisha ni madaraka na nafasi tulizonazo. Watu wanashindwa kuelewa kwamba kwa hai ilivyo kwa sasa, tutasubiri sana kuhusu wawekezaji kwani moja ya misingi mikubwa ya uwekezaji kwa wale tunaowaita Foreign Direct investors wanaangalia mambo makuu kama 3-4 ambayo yanatoweka kwa kasi kubwa sana katika nchi yetu,

1. Utawala wa sheria-hapa kwetu ni kizungumkuti, neno la mtu ndo sheria
2. Uwazi na ukweli-Hii nadhani mnakumbuka hata nchi yetu imejitoa kabisa kwenye huu ushirika (Think deep, think critically)
3. Utawala bora-hapa kuna shida kubwa sana
4. uwajibikaji-wote ni mashahidi hapa.

Ukikosa hizi Pillars za kiuchumi anza kuhesabu maumivu, na kama wawekezaji hawaji anayeumia ni wewe na mimi, hii nchi haina capacity ya ku absorb demand ya ajira iliyopo, tunashangilia na kupiga makelele lakini tunasahahu kwamba tuna matatizo makubwa sana ila kwa sababu ya akili zetu zilizofungwa hatuwezi kuyaona haya, Think of birth rate vs death rate, tukadiriwa kwa sasa kuwa 55mil na kati ya hawa over 30% ni watu ambao wako regarded kama productive people,

It might be possible Ngurumo ana mtu/watu wanompa hizi taarifa, refere to Mbowe's saga, ameanza kuelezea huu mpango wiki mbili au tatu kabla na imekuwa, suala la DAB kukasimiwa madaraka na mkuu ya usalama wa nchi ya kusadikika ni jambo ambalo limesemwa sana na watu wengi, jambo hili unaweza kulipigia mstari kwa sababu matukio yanayofanywa kwanza si ya kisomi, ni matukio yenye kukosa uweledi wa kimafunzo yenye ustadi wa kiusalama, wanaosoma mnaweza mkawafatilia MOSSAD makona namna matukio yanavyotekelezwa. Hii ni hatari kwa taifa kwani kwa kila kukicha watu wanazidi kuingiwa na hofu na kujenga hasira na vyombo vya kiusalama, hofu ya sisi kwa sisi. kisaikolojia tunaamini watu wanabadirika kulingana na mda nahali inayowazunguka, tusione watu hawa wamenyemaza ipo siku wataongea yaliyo mioyoni mwao. Masuala ya uchumi nathari zake ila naamini through spill over effect, through multipler effect na systemic risk, haya mambo yataanza kuibuka na kuonekana kwenye maisha ya watu siku za usoni.
 
Kuna Evarist Chahali pia...yuko Uingereza, Mange yuko USA baby, Ngurumo finland.....kiufupi ukitaka kuikosoa serkali uhame nchiiiii hahahahahahahaah. cc Miguna
Ukiwa Tanzania ujue Heri Kisanduku makapero atakuja na Nissan nyeupe kukupiga Risasi ni bora kukosoa ukiwa mbali kabsa.
 
Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda, alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.
Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito.

Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Makonda) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.

1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni "majasusi wa Chadema!"

2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.

3. Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na "uchawi."

4. Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.

5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe. Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.

Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!

MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?
b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?
c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?
d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi…. nitawavunja miguu?”
e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?
f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?
h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?

Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.

Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)
Safi sana Ngurumo......nlimiss sn makala zako na wenzako mwanahalisi gazeti langu pekee lkn kwa kuwa kwako nje ya nchi naamini ntapata hbr zaidi ya pengine ungekuwa nchini....ukiungana na DADA WA TAIFA MANGE na KAKA WA TAIFA RAIS LISSU na tukipata wengine kadhaa km nyie nchi itaenda kupata ukombozi halic kutoka kwa wadharimu ccm
 
Wenye akili tumeshamshtukia zaidi, anajenga mazingira ya kupata hifadhi ya kudumu ya ukimbizi kwa kuichokoza serikali kwa kuandika habari za uzushi.
Ni wazi akiandika habari za kizushi, serikali itamtafuta na yeye atatumia hilo gepu kudai anatafutwa, ila wa nchi za magharibi sio wajinga kama anavyodhani.
When a dog is let out to Jamii forums. This is what we call Vocal Diarrhea. Asbert Ngurumo does not take advice from you.
 
Africa tuna taratibu nyingi sana ila moja ya taratibu ambayo imewekwa wakti wa kula ni kwamba ukiwa unakula usiongee, hii ni falsafa ndefu sana ambayo imewekwa kama lugha ya kielelezo cha heshima ila maana yake ni kubwa, wapo walioielewa, wapo wanaoilewa, wapo wasioielewa na wapo ambao wataielewa,
1. Mtu ambaye kwa namna moja au nyingine ananufaika na huu mfumo kazi yake itakuwa ni kupinga mambo yote anayoyaiona yanaikosoa serikali
2. Mtu ambaye ni mvivu wa kufikiria kwa undani atakuwa wa kwanza kutetea huu mfumo,
3. hii inafafanana kidogo na nao.2 Mtu ambaye elimu yake ni ndogo sana, au hakwenda kabisa, uwezo wake wa kuanalyse mambo kwa undani basi atakuwa wa kwanza kupinga.
4. Mtu ambaye ni mwepesi wa kuridhika, mtu ambaye hana exposure yaani hajui wengine wamefika wapi na speed walioyonayo ni ipi kwenye masuala mtambuka kama afya, miundo mbinu, nishati, uchumi kwa ujumla basi mtu huyu atakuwa wa kwanza kupinga sababu uelewa wake uko ndani ya box la Nchi hii.

Lakini niwaambie enyi watu, kuna mambo yanatakea na yanahuzinisha na kukatisha tama sana, ammbo ambayo kizazi cha 1975 na kuendelea hatukuwahi kuyashuhudia kabisa, tumelewa kwa upendo mkubwa, amani ilikuwa imetamalaki, tumelelewa katika misingi ya kukosoana na kujenga, tukiamini hakuna mkamilifu ndani ya dunia, tumekuwa tukiamini katika umoja, tumekuwa tukishuhudia makabuli mengi sana karibu yetu yaliyobeba fikra za ukabila na udini, fikira za ubwanyenye na ubabe, fikra za udictator na ukabaila, tumekuwa tukizungukwa na maneno ya kutiana matumaini hasa nyakati zote zie shida au raha,

kwa sasa nchi yetu imeingiliwa na mdudu, nchi yetu si mahali tena pa amani, tumeanza kuandikwa vibaya kwenye magazeti makubwa sana ndunia, tumeanza kushukiwa na mataifa mengi sana kuhusu ukiukwaji wa haki za bianadamu, tunaona mihimili ya mahakama ikisiginwa, bunge linasiginwa, madaraka ya usalama yanakasimiwa na mtu mmoja, tunaona watu wenye fikra tofauti na wakubwa wanavyonyanyaswa na kuonewa, watu wanasahahu kwamba, madaraka ni ya muda, watu wanasahahu kwamba umiliki wa hii nchi uko katika usawa kwa kila mwanachi, kinachotutengenisha ni madaraka na nafasi tulizonazo. Watu wanashindwa kuelewa kwamba kwa hai ilivyo kwa sasa, tutasubiri sana kuhusu wawekezaji kwani moja ya misingi mikubwa ya uwekezaji wale tunaowaita Foreign Durect investors wanaangalia mambo makuu kama 3-4.
1. Utawala wa sheria-hapa kwetu ni kizungumkuti, neon la mtu ndo sheria
2. Uwazi na ukweli-Hii nadhani mnakumbuka hata nchi yetu imejitoa kabisa kwenye huu ushirika (Think deep, think critically)
3. Utawala bora-hapa kuna shida kubwa sana
4. uwajibikaji-wote ni mashahidi hapa.

ukikosa hizi Pillars za kiuchumi anza kuhesabu maunmivu, na kama wawekezaji hawaji anayeumia ni wewe na mimi, hii nchi haina capacity ya ku absorb demand ya ajira iliyopo, tunashangilia na kupiga makelele laini tunasahahu kwamba tuna matatizo makubwa sana ila kwa sababu ya akili zetu klufungwa hatuwezi kuyaona haya,

Ngurumo it might be possible ana mtu/watu wanompa hizi taarifa, refere to Mbowe's saga, ameanza kuelezea huu mpango wiki mbili au tatu kabla na imekuwa, suala la DAB kukasimiwa madaraka na mkuu ya usalama wa nchi ya kusadikika ni jambo ambalo limesemwa sana na watu wengi, nia hii unaweza kulipigia mstari kwa sababu matukio yanayofanywa kwanza si ya kisomi, ni matukio yenye kukosa uweledi wa kimafunzo yenye ustadi wa kiusalama, wanaosoma mnaweza mkawafatilia MOSSAD makona namna matukio yanavyotekelewa. Hii ni hatari kwa taifa kwani kwa kila kukicha watu wanazidi kuingiwa na hofa na kujenga hasira na vyombo vya kiusalama. kisaikolojia tunaamini watu wanabadirika kulingana na mda, tusione watu hawa wamenyemaza ipo siku. Masuala ya uchumi nathari zake ila naamini through spill over effect, through multipler effect na systemic risk, haya mambo yataanza kuibuka na kuonekana kwenye maisha ya watu siku za usoni.
Dah, mkuu umepigilia msumali wa inchi 6! Sidhani kama watu wamekusoma maana sijaona 'like ' bado.

Vv
 
hata wale wanaoamini Uzushi na propaganda za Msiba ni wale CCM wajinga wajinga watupu waliopungukiwa na fahamu lakini watanzania wengi wanaojielewa wanajua CCM ni hatari kwa Demokrasia ya Tanzania na kila ubaya wa CCM dhidi ya chadema unakuwa wazi kwa sababu Mungu hapendi kinachofanywa na CCM dhidi ya chadema na upinzani kwa ujumla.
 
Inamaana amezipata hizi taarifa akiwa huko ugaibuni? Kama ni hivyo sasa nihatari,nani amemfikishia taarifa za kikao hicho? Kwa kifupi kuna uvujaji mwingi sana wa taarifa kama ni hivyo,haiwezekani mtu yuko ugaibuni akaqeza kudukua siri za vikao hapa kwetuu
Wewe hujui dunia iliko, ndio maana mna underestimate watz. Kikukweli mnaongoza kizee zee tuu.
 
THANK YOU! ubarikiwe sana. Nadhani vidole vya mwenzetu kisu cha ngariba viliteleza. Tuna genge la wahuni ndani ya Ikulu, wezi, mafisadi na wauaji ambao wako tayari kufanya lolote lile ili kung’ang’ania madarakani.

Upinzani wana hali ngumu au WATANZANIA TUNA HALI NGUMU?
 
THANK YOU! ubarikiwe sana. Nadhani vidole vya mwenzetu kisu cha ngariba viliteleza. Tuna genge la wahuni ndani ya Ikulu, wezi, mafisadi na wauaji ambao wako tayari kufanya lolote lile ili kung’ang’ania madarakani.
Wanatumia pesa za Umma pesa za walipa kodi tena wengi wanaolipa kodi si wanachama wa CCM pia wengine hawana vyama lakini cha ajabu wanaenda Hazina BOT wanachukua pesa kienyeji na kuzitumia kuua upinzani ni Dhambi kubwa na Ufisadi wa kutisha kutumia pesa za Umma kwa mambo ya hovyo hovyo kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi, kuwafunga jela Wapinzani na unyama mwingi, Mungu hapendi ndiyo maana kaamua kufunua kila kitu kwa njia za ajabu ni muujiza kwani kila Mtanzania sasa anajua kiini cha ubaya na kinara wa Sumu za ubaya na uadui wa CCM ni Maliyamungu idd Amin Bashite ambaye ni Naibu Rais na mshauri mkuu wa Mtukufu malaika toka chato.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kila kinachofichwa kitawekwa hadharani
Kinachopangwa gizani kitawekwa hadharani
Na hii habari ni ya kweli kabisa
Magufuli na makonda ni watu hatari katika taifa letu
 
Vyombo vya Dola wengi hawapendezwi na Udikteta unaoendelea sasa ndiyo maana hutoa siri zote kwa chadema:
 
Hawa watu wamejaa uovu wa kutisha dhidi ya Watanzania. Sasa sababu za dhalimu Bashite kukingiwa kifua na Mkuu wa kitengo cha watu wasiojulikana nje nje na huyu ndiye mratibu wa shambulizi kali la kutaka kumuua Lissu the Great.

Mwenyezi Mungu inusuru nchi yetu na hili genge la wauaji.

Kila kinachofichwa kitawekwa hadharani
Kinachopangwa gizani kitawekwa hadharani
Na hii habari ni ya kweli kabisa
Magufuli na makonda ni watu hatari katika taifa letu
 
Hahahaha, hahahahahaaaa hiyo mwandishi wa habari MBM ulifundishwa chuo gani? Kuna Journalists San Frontiers, sasa hiyo, Ngurumo kweli
Lakini tumemuelewa kwa kiswahili alichotumia (tafsiri isiyo rasmi) na hilo ndo la msingi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mwanahabari Huru, unajua madhara ya kutoa habari kama hiyo, au hujui? Ukikamatwa kuthibitisha nawe utasema haki na uhuru wako umeingiliwa?

Nimekidharau na kila bandiko lako nitalisoma kwa jicho la tatu.

UPUUZI NA UJINGA. MTU MZIMA HOVYO,
unajua kanunu ya uwandishi au unapepesa macho tu?
 
Back
Top Bottom