singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
ANSBERT NGURUMO, kwa takribani miaka yote kumi ya utawala wa wa Kikwete, alitumia kalamu yake kumuuliza Rais Kikwete alichokuwa akikita maswali magumu, aliuliza maswali hayo bial kuchoka kwa muda wote huo hakuna kumbukumbu kama aliwahi kujibiwa.
Mwaka 2005, katika mchakato wa uteuzi wa CCM wa kumtafuta mteule wake ambapo Kikwete aliibuka kidedea, Ngurumo alikuwa katika kambi ya Malecela, waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais mstaafu.
Kwa bahati mbaya jina la Malecela lilitupwa mwanzoni kabisa katika mchakato huo kitendo hicho hakikumfurahisha Ngurumo ndipo akaamua kuwa mpinzani wa CCM
Mwaka 2010, Chadema ilipomsimamisha Dk. Wilboard Slaa ambaye kwa kidogo alikuwa mgombea urais kutoka upinzani mwenye muonekano wa uzalendo wa uadilifu wa kweli.
Hapo ndipo Ngurumo akapata pa kupumulia, akaingia front kumuunga mkono Dk. Slaa kabla ya kupata bahati ya kuwa miongoni mwa watu watano muhimu wa kubeba mikoba ya mgombea huyo wa urais katika kipindi chote hicho akifanywa kuwa mratibu na mshauri.
Kila Mtanzania mwenye kuitakia afya njema nchi yake angeweza kuungana na Dk. Slaa kutokana kilele cha ufisadi ambacho nchi ilikuwa imefikia chini ya uongoiizi wa Rais Kikwete, mafisadi wakitamba kifua mbele bila ya kuguswa wakati walikuwa wakifahamika na vitendo vyao vikijulikana
Binafsi nawachukia mafisadi na vitendo vyao kwa nchi hii kama ambavyo niliamini Kama Ngurumo na Dk. Slaa wanavyowachukia mafisadi pamoja na vitendo vyao vya kifisadi.
Mwaka 2010 niliamini asalimia zote kwamba ndoa ya Ans Ngurumo na Dk Slaa ilitokana na msimamo wa kuwachukia mafisadi wananchi hii pamoja na vitendo vya kifisadi, hivyo basi iliwahitaji wanyonge hao waunganishe nguvu zao pamoja na wanyonge wengine dhidi ya nguvu ya mafisadi.
Kumbe nilikosea kuamini hivyo kwa Ngurumo ila kwa Dk Slaa nilikuwa sahihi. Kilichowaunganisha mwaka 2010 haukuwa ukombozi wa nchi dhidi ya mafisadi, kumbe Ans Ngurumo alikuwa anatazama mbli zaidi, maslahi binfsi zaidi ya kiuchumi na kisasa.
Kwa nini nilikosea, Baadhi ya maswali ya Ngurumo kwa Kikwete yalihusu, kwa nini kiongozi huyo alikiuka miiko nya mwalimu Nyerere kwa kumteua Lowassa kuwa waziri mkuu wake?
Na hata mwaka 2008 Rais Kikwete alipolazimika kuvunja baraza la mawaziri na kumfukuza Lowassa kutokana na kashfa ya ufisadi wa richimond, Bado Ngurumo liendelea kusisitiza kwa rais kikwete enzi hizo kwamba mzimu wa Mwl. Nyerere hautamuacha salama kwa kuendelea kumkumbatia fisadi Lowassa ndani ya chama chake cha CCM.
Kwa msimamo huo wa wa Ngurumo wengi wetu tulidhania baada ya Dk.Slaa kusutwa na nafsi yake hivyo kufanya uamuzi mzito wa kuachana na Chadema, baada ya uongozi kufanya kosa kubwa la kiufundi la kukabidhi chama kwa lowassa na kumfanya kuwa mgombea urais, Ngurumo naye angeonyesha uzalendo wake wa kuunga mkono hatua hiyo ya Dk. Slaa.
Leo hii kwa neema za Mungu, ndani ya CCM amepatikana DK. Magufuli aliyedhamiria kupambana na uchafu wake wote ndani ya serikali na taasisi zake, Kina Ngurumo hawa wa kumdhikhaki na kumkejeli?
Eti anadiriki kusema hana dhamira hiyo na wala hakuwa chaguo la watanzania, bali Lowassa ambaye yeye NGurumo alikuwa akimsakama Kikwete usiku na mchana akimtaka kumfunga jela kwa ufisadi ndio huyo huyo leo anasema kuwa ndio chaguo la watanzania?
Huyu Ngurumo hakuwahi kumwamini Kikwete kama kama president material na sasa anandika upuuzi ule ule kama hamuamini Dk. Magufuli kama president material.
Yeye alimuamini Mwalimu NYerere akamuamini Malecela na akamwamini Lowassa wakati Mwalimu aliwakataa wote Malecela na Lowasa, tena miaka takribani kumi akitumia kalamu yake kutuaminisha kuwa fisadi leo anatwambia Lowassa ndiye president material na alikuwa chagua la watanzania na angekuwa rais bora kuliko Dk. Magufuli?
Mwisho kaka yangu ANSBERT NGURUMO kweli njaa mbaya lakini usitoe njaa tumboni na kupeleka kichwani utaaribu kichwa.