Ansbert Ngurumo anauliza: Maamuzi magumu? Mbona tuko gizani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ansbert Ngurumo anauliza: Maamuzi magumu? Mbona tuko gizani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by M-mbabe, Jul 3, 2011.

 1. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,993
  Likes Received: 3,742
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Ansbert Ngurumo

  MIAKA mitano iliyopita, Rais Jakaya Kikwete aliandika historia kwa kukiri hadharani kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa kimeshinda uchaguzi kwa mapato haramu.

  Ilikuwa hivi. Baada ya miezi minne tu madarakani katika awamu yake ya kwanza, Rais Kikwete alikutana na 'wafadhili' wa CCM), jijini Dar es Salaam, walioisaidia kupata pesa za kampeni mwaka 2005.

  Katika kuzungumza nao, Kikwete alisisitiza mambo mawili. Kwanza, aliwaomba wana CCM wasilewe ushindi walioupata mwaka 2005, badala yake wajiandae kwa uchaguzi mkuu unaofuata.

  Pili, aliwaasa wanachama wenzake waanze kutafakari namna ya kupata MAPATO HALALI kwa ajili ya kampeni. Hili ndilo lilizua maswali, hasa kwa kuwa lilitoka kinywani mwake baada ya chama kushinda kwa nguvu kubwa ya pesa, huku kikiwa kinashutumiwa kusaidiwa na matajiri kadhaa wanaojihusisha na wizi na ujambazi.

  Tunapowapima leo, tunagundua kwamba yote mawili yamewashinda. CCM ilibweteka, ikajidai itatawala milele, ikabaki kuimba ushindi wa kishindo wa mwaka 2005.

  Mwenendo na matokeo ya kura katika uchaguzi wa mwaka 2010, vimeonyesha kwamba CCM haitatawala milele. Na baadhi ya wachambuzi wa siasa wanasema kuwa huu ndio umekuwa uchaguzi wa mwisho wa CCM kuwaburuza wananchi.

  Dalili zote zinaonyesha kuwa kisipojisuka vema, miaka minne ijayo kitakuwa kimefika kule viliko vyama vingine vya ukombozi barani Afrika. Mapumzikoni. Kitakuwa kinajiandaa upya katika harakati za kujaribu kurejea madarakani.

  Lakini hili la pili ndilo limechangia pia katika kuishusha CCM mbele ya umma, na kuwafanya viongozi wake waonekane watu wasioaminika, wenye maneno yasiyofanana na matendo yao; wasio na uwezo wa kutumia kodi zetu kutuletea kile walichotuahidi.

  Wakati ule, kuna Watanzania hawakumwelewa Rais Kikwete. Lakini baada ya mapambano ya ufisadi kuanika matukio ya wizi wa EPA na mengine yaliyofanana nayo, leo kila mtu anaelewa vema maana ya kauli ya Rais Kikwete.

  Kumbe alikuwa anajua kwamba kampeni zake zilifanikishwa na pesa chafu. Hakutaka litokee tena. Lakini ameshindwa kulizuia.

  Maana katika uchaguzi wa mwaka jana (2010), CCM ilipokea michango kutoka kule kule, na hata kutumia baadhi ya ndege zinazomilikiwa na watu wale wale wanaotiliwa shaka.

  Aliishia kutamka tu kwamba anakusudia kutunga sheria ya kuzuia wafanyabiashara kuwa wanasiasa, akaishia kuwaomba wafanyabiashara wa aina ile ile wafanikishe kampeni zake.

  Kwanini nimekumbuka mambo haya leo? Wiki hii tumekumbushwa dhana ya maamuzi magumu ambayo serikali imekuwa inashindwa kuchukua.

  Bahati mbaya, kila mara wapinzani walipokuwa wanazungumza kauli ya kuitaka serikali kuchukua maamuzi magumu, walikuwa wakizomewa na wabunge wa CCM.

  Zamu hii kauli ile ile imezungumzwa na mwana-CCM mwenzao, kigogo na mwasisi wa serikali ya awamu ya nne, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

  Ameitaka serikali iache kuogopa, ichukue maamuzi na ikubali sifa au lawama kwa uamuzi wake.

  Nilimsikiliza na kumuona Lowassa akitoa hotuba yake bungeni. Wabunge wengi wa CCM, isipokuwa Samuel Sitta, walikuwa wakimshangilia badala ya kumzomea. Maana yake ni kwamba walikubaliana na kauli yake – ile ile wanayoizomea kila inapozungumzwa na wapinzani!

  Lakini kikubwa zaidi ni majibu yaliyotolewa na serikali. Ni majibu ya kejeli. Hayaonyeshi umakini. Yanaendekeza uchovu na ubabaishaji ule ule ulioifikisha hapa ilipo.

  Serikali, kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilipuuza kauli ya Lowassa na kusisitiza kwamba katika miaka 50 ya historia ya Tanzania huru, hakuna serikali iliyofanya maamuzi magumu kama serikali ya awamu ya nne.

  Akataja miradi waliyotekeleza: ujenzi wa shule za kata, umaliziaji wa barabara zilizoachwa na Rais Benjamin Mkapa, ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, kuvunja Baraza la Mawaziri mwaka 2008 na mengine machache.

  Katika yote haya, sikuona uamuzi wowote mgumu uliotolewa. Ujenzi wa shule za kata nchi nzima ni uamuzi wa kisera ulioanzishwa na Lowassa mwenyewe, lakini haukuwa umefanyiwa maadalizi ya kina. Si uamuzi mgumu kuanzisha shule nyingi zisizo na walimu, vitabu, maabara, mabweni na vifaa vingine muhimu.

  Hata kama ungekuwa uamuzi mgumu, matokeo ya mitihani ya taifa katika shule hizo, hayaonyeshi kama ni jambo la kujivunia kuingiza watoto kwenye shule wakakaa miaka minne bila kuelimika, wakapoteza mwelekeo wa maisha yao kitaaluma.

  Badala ya shule za kata, bora wangeanzisha vyuo vichache vya ufundi katika kila wilaya, kwa maandalizi ya kuwapatia wanafunzi stadi za maisha ambazo ni bora kuliko kidato cha nne kisicho na cheti au chenye alama zisizoweza kumsaidia mtoto kuendelea na masomo ya juu.

  Kumalizia barabara zilizoanzishwa na Rais Mkapa, tena nyingi kwa kiwango kisichoridhisha, si uamuzi mgumu. Ni wajibu wa serikali. Chuo Kikuu cha Dodoma ni fahari ya taifa, kama ukubwa wa majengo, na wingi wa wanafunzu vitaendana na uwezo na nia ya serikali kukijali na kukiwezesha kufyatua wasomi weledi wanaoendana na mahitaji ya karne ya 21.

  Na bado huu si muujiza, wala si uamuzi mgumu. Ni wajibu wa serikali. Ni njia mojawapo ya kutumia kodi za wananchi kwa ajili ya kuendeleza watu wake.

  Kama serikali inataka kujitapa kwa maamuzi magumu, mbona taifa liko gizani? Kama inataka kujitapa kwa maamuzi magumu, mbona iliwaogopa mafisadi wa EPA, hata ikawabembeleza warudishe pesa ili isiwashitaki? Kama inataka kujitapa kwa maamuzi magumu mbona ilikiri kwamba Kagoda hawakamatiki?

  Kama serikali inataka kujitapa kwa maamuzi magumu mbona ilishindwa kumtia mbaroni aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Balali? Mbona ilijidai haijui alikokimbilia? Mbona ilijidai haijui alikodaiwa kuugulia? Mbona ilishindwa kumfuata kokote aliko na kumrejesha ili awe shahidi katika kesi ya wizi wa EPA?

  Kama serikali inajitapa kwa maamuzi magumu, mbona taifa linakabiliwa na njaa?

  Siamini kwamba haya ninayojadili ndiyo maamuzi magumu aliyokuwa amekusudia Lowassa bungeni, lakini ni wazi kwamba Lowassa ametupatia fursa ya nyongeza kuibana serikali ifanye maamuzi magumu. Na kama hayo iliyofanya ndiyo inaita maamuzi magumu, basi hatuna serikali!

  Kuvunja Baraza la Mawaziri si uamuzi mgumu. Kwa kawaida, anayeunda baraza hilo ndiye ana wajibu wa kulivunja. Lakini Rais Kikwete hajavunja Baraza la Mawaziri. Ilikuwa lazima livunjike baada ya Lowassa kujiuzulu.

  Kama rais angetaka heshima ya kuvunja Baraza la Mawaziri, angemfukuza kazi Lowassa. Alishindwa kumfukuza Waziri Mkuu, hadi Spika wa Bunge wa wakati huo, Samuel Sitta na Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, walipomsaidia “kumshauri Lowassa apime na kutafakari hatima yake kisiasa.”

  Kwa hiyo, kimantiki, haukuwa uamuzi wa serikali, bali wa Bunge. Maana kama serikali ingekuwa na uwezo wa kufanya maamuzi hayo, isingeliacha Bunge liifikishe mahali pa kuivua nguo na kuidhalilisha.

  Ingekuwa heri kama Pinda angepuuza kabisa hoja hii, kuliko kuthubutu kuijibu kwa kutoa kauli inayozidi kushusha heshima ya serikali mbele ya umma. Lakini kama tunakubaliana kwamba haya aliyotaja ndiyo maamuzi magumu ya serikali ya awamu ya nne, basi serikali haijaanza kazi!

  Maamuzi magumu yangeturudisha kule kule alikoanzia rais mwaka 2006, kusafisha mifumo ya chama tawala na serikali na kujijengea uhalali wa kutawala kwa heshima na ridhaa ya wananchi. Wamelazimisha ushindi mwaka jana, na sasa wanatawala kwa kulazimisha. Je, na huu tuuite uamuzi mgumu?
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Asante mwandishi ngurumo huyu Pinda anafikiri anahutubia chekechea!!kukaa kwake ikulu miaka 30 haikumsaidia hata kupata busara na kufikiria zaidi ya wanaomzunguka kweli!!ameshndwa kuchota busara na uwezo wa JKN,AHM,BWM kweli???huyu hata ubalozi wa nyumba kumi hafai kabisa!!
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Kwa hali ilivyo mm nashau watz tutulie tukia hiki chama kijfie haraka iwezekanavyo maana tukiendelea kutoa ushauri tunachelewesha kifo cha haki cha ccm!
   
 4. J

  Jombi Jombii Senior Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK ni mtu hatari kwa Taifa hili.Anasamehe wezi kabla ya kupelekwa mahakamani na kuwaomba Majambazi wa EPA warudishe pesa badala ya kuwafilisi na kuwafungulia kesi za kuhujumu uchumi?2015 na ifike ili jina lipotee kabisa kwenye uso wa TZ
   
 5. F

  Fareed JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Serikali ya Jakaya Kikwete haijawahi kufanya maamuzi magumu yoyote. Kwanza mgao unaoendelea lawama zinaenda moja kwa moja kwa Kikwete kwani katika kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano (2005-2010) serikali yake imeongeza 145MW tu kwenye gridi ya taifa. Angefanya maamuzi magumu kwa kuongeza 1,000MW kwenye gridi ya taifa kwa miaka 5 iliyopita sasa Tanzania ingekuwa na umeme wa ziada. Wala si kazi ngumu, angejiwekea lengo la kuongeza 200MW tu kwa mwaka kwenye gridi ya taifa.

  Edward Lowassa, waziri mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kuhusika na kashda ya ufisadi ya Richmond, hana moral authority ya kumnyooshea kidole mtu na kudai ameshindwa kazi au hawezi kufanya maamuzi magumu. Kwanza Lowassa alikuwa waziri mkuu kwa miaka 3 kati ya 5 ya awamu ya kwanza ya Kikwete hivyo matatizo mengi ya awamu ya kwanza yeye pia anahusika.

  Lowassa ndio aliliingiza taifa kwenye janga hili la umeme kwa kuliingiza taifa kwenye mgogoro wa Richmond/Dowans. Pia ametumia nafasi zake za uongozi serikalini kupata utajiri mkubwa sana. Lowassa amechafuka sana kwa tuhuma za ufisadi, hivyo kitendo cha wabunge wa CCM kumshangilia kinaonesha jinsi CCM kilivyopoteza mwelekeo na sasa chama hiki kinaunga mkono viongozi kama Lowassa ambao ni wachafu sana kwa tuhuma za rushwa.
   
 6. M

  Mtanzania Huru Member

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lowassa ni sumu kubwa kwenye siasa ya Tanzania. Mtu yoyote anayetukuza maneno yake au kumuunga mkono fisadi huyu ni msaliti kwa taifa hili la Julius Nyerere aliyemgundua Lowassa tangu zamani kuwa hafai kuwa kiongozi wa nchi yetu. Lowassa na genge lake la mafisadi -- Rostam Aziz na Andrew Chenge -- ni hatari sana kwa usalama wa Tanzania.

  Ni upumbavu mkubwa kwa watu kuendelea kumsifia na kumjadili Lowassa kama vile Tanzania haina viongozi mahiri ambao hawajachafuka na tuhuma za ufisadi kwenye vyama vikubwa vya siasa nchini CCM (Samuel Sitta, Harisson Mwakyembe, Bernard Membe, Asha-Rose Migiro, John Magufuli) na CHADEMA (Dk. Willibrod Slaa, Tundu Lissu, John Mnyika, Kitila Mkumbo, etc)
   
 7. s

  sikiolakufa JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Maamuzi magumu? Mbona tuko gizani?
  [​IMG]

  Ansbert Ngurumo​
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  MIAKA mitano iliyopita, Rais Jakaya Kikwete aliandika historia kwa kukiri hadharani kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa kimeshinda uchaguzi kwa mapato haramu.
  Ilikuwa hivi. Baada ya miezi minne tu madarakani katika awamu yake ya kwanza, Rais Kikwete alikutana na 'wafadhili' wa CCM), jijini Dar es Salaam, walioisaidia kupata pesa za kampeni mwaka 2005.
  Katika kuzungumza nao, Kikwete alisisitiza mambo mawili. Kwanza, aliwaomba wana CCM wasilewe ushindi walioupata mwaka 2005, badala yake wajiandae kwa uchaguzi mkuu unaofuata.
  Pili, aliwaasa wanachama wenzake waanze kutafakari namna ya kupata MAPATO HALALI kwa ajili ya kampeni. Hili ndilo lilizua maswali, hasa kwa kuwa lilitoka kinywani mwake baada ya chama kushinda kwa nguvu kubwa ya pesa, huku kikiwa kinashutumiwa kusaidiwa na matajiri kadhaa wanaojihusisha na wizi na ujambazi.
  Tunapowapima leo, tunagundua kwamba yote mawili yamewashinda. CCM ilibweteka, ikajidai itatawala milele, ikabaki kuimba ushindi wa kishindo wa mwaka 2005.
  Mwenendo na matokeo ya kura katika uchaguzi wa mwaka 2010, vimeonyesha kwamba CCM haitatawala milele. Na baadhi ya wachambuzi wa siasa wanasema kuwa huu ndio umekuwa uchaguzi wa mwisho wa CCM kuwaburuza wananchi.
  Dalili zote zinaonyesha kuwa kisipojisuka vema, miaka minne ijayo kitakuwa kimefika kule viliko vyama vingine vya ukombozi barani Afrika. Mapumzikoni. Kitakuwa kinajiandaa upya katika harakati za kujaribu kurejea madarakani.
  Lakini hili la pili ndilo limechangia pia katika kuishusha CCM mbele ya umma, na kuwafanya viongozi wake waonekane watu wasioaminika, wenye maneno yasiyofanana na matendo yao; wasio na uwezo wa kutumia kodi zetu kutuletea kile walichotuahidi.
  Wakati ule, kuna Watanzania hawakumwelewa Rais Kikwete. Lakini baada ya mapambano ya ufisadi kuanika matukio ya wizi wa EPA na mengine yaliyofanana nayo, leo kila mtu anaelewa vema maana ya kauli ya Rais Kikwete.
  Kumbe alikuwa anajua kwamba kampeni zake zilifanikishwa na pesa chafu. Hakutaka litokee tena. Lakini ameshindwa kulizuia.
  Maana katika uchaguzi wa mwaka jana (2010), CCM ilipokea michango kutoka kule kule, na hata kutumia baadhi ya ndege zinazomilikiwa na watu wale wale wanaotiliwa shaka.
  Aliishia kutamka tu kwamba anakusudia kutunga sheria ya kuzuia wafanyabiashara kuwa wanasiasa, akaishia kuwaomba wafanyabiashara wa aina ile ile wafanikishe kampeni zake.
  Kwanini nimekumbuka mambo haya leo? Wiki hii tumekumbushwa dhana ya maamuzi magumu ambayo serikali imekuwa inashindwa kuchukua.
  Bahati mbaya, kila mara wapinzani walipokuwa wanazungumza kauli ya kuitaka serikali kuchukua maamuzi magumu, walikuwa wakizomewa na wabunge wa CCM.
  Zamu hii kauli ile ile imezungumzwa na mwana-CCM mwenzao, kigogo na mwasisi wa serikali ya awamu ya nne, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.
  Ameitaka serikali iache kuogopa, ichukue maamuzi na ikubali sifa au lawama kwa uamuzi wake.
  Nilimsikiliza na kumuona Lowassa akitoa hotuba yake bungeni. Wabunge wengi wa CCM, isipokuwa Samuel Sitta, walikuwa wakimshangilia badala ya kumzomea. Maana yake ni kwamba walikubaliana na kauli yake – ile ile wanayoizomea kila inapozungumzwa na wapinzani!
  Lakini kikubwa zaidi ni majibu yaliyotolewa na serikali. Ni majibu ya kejeli. Hayaonyeshi umakini. Yanaendekeza uchovu na ubabaishaji ule ule ulioifikisha hapa ilipo.
  Serikali, kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilipuuza kauli ya Lowassa na kusisitiza kwamba katika miaka 50 ya historia ya Tanzania huru, hakuna serikali iliyofanya maamuzi magumu kama serikali ya awamu ya nne.
  Akataja miradi waliyotekeleza: ujenzi wa shule za kata, umaliziaji wa barabara zilizoachwa na Rais Benjamin Mkapa, ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, kuvunja Baraza la Mawaziri mwaka 2008 na mengine machache.
  Katika yote haya, sikuona uamuzi wowote mgumu uliotolewa. Ujenzi wa shule za kata nchi nzima ni uamuzi wa kisera ulioanzishwa na Lowassa mwenyewe, lakini haukuwa umefanyiwa maadalizi ya kina. Si uamuzi mgumu kuanzisha shule nyingi zisizo na walimu, vitabu, maabara, mabweni na vifaa vingine muhimu.
  Hata kama ungekuwa uamuzi mgumu, matokeo ya mitihani ya taifa katika shule hizo, hayaonyeshi kama ni jambo la kujivunia kuingiza watoto kwenye shule wakakaa miaka minne bila kuelimika, wakapoteza mwelekeo wa maisha yao kitaaluma.
  Badala ya shule za kata, bora wangeanzisha vyuo vichache vya ufundi katika kila wilaya, kwa maandalizi ya kuwapatia wanafunzi stadi za maisha ambazo ni bora kuliko kidato cha nne kisicho na cheti au chenye alama zisizoweza kumsaidia mtoto kuendelea na masomo ya juu.
  Kumalizia barabara zilizoanzishwa na Rais Mkapa, tena nyingi kwa kiwango kisichoridhisha, si uamuzi mgumu. Ni wajibu wa serikali. Chuo Kikuu cha Dodoma ni fahari ya taifa, kama ukubwa wa majengo, na wingi wa wanafunzu vitaendana na uwezo na nia ya serikali kukijali na kukiwezesha kufyatua wasomi weledi wanaoendana na mahitaji ya karne ya 21.
  Na bado huu si muujiza, wala si uamuzi mgumu. Ni wajibu wa serikali. Ni njia mojawapo ya kutumia kodi za wananchi kwa ajili ya kuendeleza watu wake.
  Kama serikali inataka kujitapa kwa maamuzi magumu, mbona taifa liko gizani? Kama inataka kujitapa kwa maamuzi magumu, mbona iliwaogopa mafisadi wa EPA, hata ikawabembeleza warudishe pesa ili isiwashitaki? Kama inataka kujitapa kwa maamuzi magumu mbona ilikiri kwamba Kagoda hawakamatiki?
  Kama serikali inataka kujitapa kwa maamuzi magumu mbona ilishindwa kumtia mbaroni aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Balali? Mbona ilijidai haijui alikokimbilia? Mbona ilijidai haijui alikodaiwa kuugulia? Mbona ilishindwa kumfuata kokote aliko na kumrejesha ili awe shahidi katika kesi ya wizi wa EPA?
  Kama serikali inajitapa kwa maamuzi magumu, mbona taifa linakabiliwa na njaa?
  Siamini kwamba haya ninayojadili ndiyo maamuzi magumu aliyokuwa amekusudia Lowassa bungeni, lakini ni wazi kwamba Lowassa ametupatia fursa ya nyongeza kuibana serikali ifanye maamuzi magumu. Na kama hayo iliyofanya ndiyo inaita maamuzi magumu, basi hatuna serikali!
  Kuvunja Baraza la Mawaziri si uamuzi mgumu. Kwa kawaida, anayeunda baraza hilo ndiye ana wajibu wa kulivunja. Lakini Rais Kikwete hajavunja Baraza la Mawaziri. Ilikuwa lazima livunjike baada ya Lowassa kujiuzulu.
  Kama rais angetaka heshima ya kuvunja Baraza la Mawaziri, angemfukuza kazi Lowassa. Alishindwa kumfukuza Waziri Mkuu, hadi Spika wa Bunge wa wakati huo, Samuel Sitta na Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, walipomsaidia “kumshauri Lowassa apime na kutafakari hatima yake kisiasa.”
  Kwa hiyo, kimantiki, haukuwa uamuzi wa serikali, bali wa Bunge. Maana kama serikali ingekuwa na uwezo wa kufanya maamuzi hayo, isingeliacha Bunge liifikishe mahali pa kuivua nguo na kuidhalilisha.
  Ingekuwa heri kama Pinda angepuuza kabisa hoja hii, kuliko kuthubutu kuijibu kwa kutoa kauli inayozidi kushusha heshima ya serikali mbele ya umma. Lakini kama tunakubaliana kwamba haya aliyotaja ndiyo maamuzi magumu ya serikali ya awamu ya nne, basi serikali haijaanza kazi!
  Maamuzi magumu yangeturudisha kule kule alikoanzia rais mwaka 2006, kusafisha mifumo ya chama tawala na serikali na kujijengea uhalali wa kutawala kwa heshima na ridhaa ya wananchi. Wamelazimisha ushindi mwaka jana, na sasa wanatawala kwa kulazimisha. Je, na huu tuuite uamuzi mgumu?
  ​

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 8. Bernard Rwebangira

  Bernard Rwebangira R I P

  #8
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maamuzi magumu ni kwenda kuwaonyesha wabunge "sinema" ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya na ushaidi badala ya kuwakamata na kuwapeleka panapostahili, wait a minute! last week kulikuwa na opereshen kamata mateja, isijekuwa ndo picha litalooneshwa! wacha tusubiri tuone.
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nilishanga sana niliposikia kuwa kuanzishwa kwa UDOM ni maamuzi magumu.an ni magumu kuliko awamu zote?????mmmh
  mimi ntayataja maamuz magumu sana ya awamu ya kwanza

  1.AZIMIO LA ARUSHA NI MAAMUZ MAGUMU SANA,NA HAKUNA SERIKA ITAKAYOWEZA KUFANYA HIVO
  2.Ujenzi wa reli ya TAZARA(AFRICA'S FREEDOM RAILWAY)
  3.KUJENGA VIWANDA ILHALI NCH IKIWA NA GRADUANDS WASIOZID 50 NI MAAMUZ MAGUM,PINDA ACHA POROJO BWANAAA
   
 10. C

  Campana JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi shule za kata imejenga serikali au tumejenga sisi wananchi kwa pesa zetu n nguvu zetu? Serikali ilitakiwa ituletee waalimu, haijafanya hivyo. Huo uamizi aliousema Pinda uko wapi?
   
 11. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Maamuzi magumu ni ya pinda kukoloma bungeni dhidi ya wapinzani.
  Na viongozi kujitokeza kunywa kikombe cha babu.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Maneno ya pinda ni sahihi kabisa kwa vile anayatoa kama Kada wa CCM. Ningeshangaa kama maneno hayo yangetoka mdomoni mwa mtu ambaye hayuko affiliated na CCM.
   
 13. S

  SAMMYT Member

  #13
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa wabunge na wawakilishi wetu wanajua hasa core responsibility yao? maana naona wanaishia kulinda zaidi maslahi ya vyama vyao badala ya kufikisha ujumbe wanapewa na waliowachagua. Nchi ikiendeleza sana siasa haifiki popote
   
 14. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Kwenye nyekundu hapo, tuambie Lowasa alistaafu lini? Unasema Sita hakushangilia, Mwakyembe je? Ole Sendeka je? Manyanya je?

  Ubaya wake Gazeti la Tanzania Daima mmeshaingia kwenye Mchezo wa kumchafua Sita. Rejea Makala ya Absolom Kibanda yenye maneno kama Sita hafai hata kuongoza Familia yake.

  Maoni yangu
  CCM= Chama cha Magamba=Lowasa=Sitta= Kikwete

  MBIO ZA URAISI ZINAWASUMBUA HAO. TUTASIKIA KAULI NYINGI TOKA KWA LOWASA ZA KUFANYA TUMUAMINI. HAMANA AATAKAYEMUAMINI LOWASA WALA SITA WALA AWAYE YOYOTE TOKA CCM

  Magazeti yote isipokuwa Raia Mwema na Magazeti ya IPPM MEDIA YANAONYESHA KILA DALILI YAMENUNULIWA. KITU KIDOGO TU AKISEMA LOWASA, UKURASA MZIMA UNAMPAMBA

  HATUDANGANYIKI, LIKE CCM MAGAMBA MAGUMU LIKE LOWASA LIKE SITA
   
 15. W

  Warofo Member

  #15
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Nakuunga mkono, MWANAHALISI na Tanzania Daima ni miongoni mwa mwagazeti ambayo wamiliki/wahariri wake wamenunuliwa na Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge kuwalinda mafisadi hawa na kuwashambulia maadui wa mafisadi hawa -- Sitta, Nape, Mwakyembe, Membe, Kikwete, etc.

  Eti Lowassa waziri mkuu mstaafu? Pumbaf, huyu ni waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond. Kamwe historia hii haitafutika na itamtafuna mpaka mwisho kwenye mbio zake za sakafuni za kusaka urais 2015.
   
 16. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Watanzania wamefanya UAMUZI MGUMU NA WA HATARI SANA kukubali kuongozwa na Chama Cha Magamba. Nan anabisha?
   
 17. m

  mtimbaru Member

  #17
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  EL ni captain wa jeshi mstaafu na amewahi kuwa katibu wa ccm mkoa wa shinyanga na mkurugenzi wa AICC na mfahamu vizuri. huyu EL ana karama ya uongozi na ni mchapa kazi,kilichomchafua ni utajiri wa kupindukia ambao hayati Mwl Nyerere ana ushahidi,hii ni dosari inayomtafuna na kingine ni kashfa ya RICHMOND. Kwa hiyo rafiki yangu EL urais 2015 usijidanganye acha kabisa, nchi ina watu wengi wasafi wenye uwezo wa kuongoza.
   
 18. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
 19. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  udoma kama shule za kata tu, tofauti yake ina majengo mazuri. Lecturers wa udom baadhi yao wana degree moja, tutafika kweli?
   
 20. E

  EL+RA=UFISADI Member

  #20
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mhariri Mkuu wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, yuko kwenye payroll ya Edward Lowassa. Hili jambo linafahamika sana. Hata mmiliki wa Tanzania Daima, Freeman Mbowe wa CHADEMA, anajua hili lakini hachukui hatua yoyote kwa kuwa Mbowe na Lowassa ni marafiki. Kama mnabisha, jiulizeni ni lini Mbowe amemnyooshea kidole Lowassa hadharani au kuzungumzia kashfa ya Richmond na kumuita Lowassa fisadi?

  Tulidhani kuwa Ansbert Ngurumo ni mtu mwenye msimamo, kumbe na yeye sasa kawekwa mfukoni Lowassa! Eti anamuita Lowassa waziri mkuu mstaafu, huyu ni waziri mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi. Hata akaogeshwe maji ya baharini, Lowassa hatakati ng'o kwa tuhuma nzito za ufisadi na kujilimbikizia mali kwa kutumia ofisi za umma.

  Kwa kutumia nafasi zake kama mkurugenzi wa AICC, waziri na waziri mkuu, Lowassa tayari amekuwa bilionea. Je akipata Urais anaoutaka kwa gharama yoyote ili kwa kushirikiana na fisadi mwenzake Rostam Aziz, Lowassa si atakuwa mwizi mkubwa kama Sani Abacha au Mobutu Seseseko!!
   
Loading...