Mtoto wa Mkulima
JF-Expert Member
- Joined
- Apr 12, 2007
- Messages
- 688
- Points
- 0
Habari zaidi tutawaletea kwa mujibu wa BBc. Stay turned
Hii Rwanda nduguyangu, wakati yale yakitokea Koffi Annan alikuwa kule same is happening in Kenya....Mungu bariki Afrika!!Hivi hii si Rwanda inanukia hiiii???????
What a coincidence! Kifo hiki ni vigumu kukitenganisha na machafuko yanayoendelea nchini Kenya kwa sasa.Kulipiza kisasi???
Naskia ni mauaji wa wivu wa mapenzi- huyu askari pia ameua askari mwingine wa kile ktk gari la mbunge- ambaye alikuwepo ktk gari na inasemekana ni mpenzi wake!
Mambo ya mapenzi- ila inatokea wakati huu wa machafuko ya kisiasa!
Mie pia nimeipata hio nyeti na bado nafuatiliza na sources zangu huko Kenya.Jamaa ni mbunge wa Ainamoi mitaa ya Eldoret.Sasa kasheshe ipo maana hapo nd'o panapotokea wale Kalenjin Warriors walioanzisha tifu la kuwaua wakikuyu baada ya Kibaki kuiba kura. Sasa niambie watafanzani vile mtu wao kauliwa?A'fu kumbuka vidole bado vipo kwenye serikali ya Kibaki kuhusu kifo cha yule mbunge wa kwanza.Mbunge Mwingine wa ODM ameuawa.
Bila shaka hili si Taifa tena.
Hamna cha kukubali wala nini.Haya maji yashavuliwa nguo na lazima yakogwe tu!Hata Raila akikubali,unadhani walalahoi watakubali?Si watamwambia tu asogee kando aje mtu mwengine kama vile Ruto.Hii kitu si ya Raila bali wakenya wote wameamua na Raila akigeuza kibano watamwambia achukue namba.Wajaluo wake wenyewe washamuambia.Bongo tukae mkao wa kupokea wakimbizi tu!Mie nafikiri kuna mkono wa kibaki ili Odinga akubali matokeo na mambo yasonge mbele
Kazi ipo kwa hawa watani wetu wa jadi hata sijui itakuaje. Serikali isiowezi kuhakikisha usalama kwa raia wake haina mamlaka ya kutawala nchi.Ni mtazamo tu.Hii sasa noma...
well said bro.AU na UN wasipochukua hatua za dharura na za mapema sana naona hali ya Kenya inaweza kuwa kama ile iliyotokea Rwanda 1994. Viongozi wa EAC na Afrika kwa ujumla liangalieni hili kwa upana na kwa makini zaidi, tuache kushabikia uroho wa madaraka kwa damu ya raia wasio na hatia, hii ni hatari sio kwa Kenya pekee bali kwa nchi zote majirani, Afrika na Dunia kwa ujumla.