Anne Makinda na Definition yake ya Ufisadi

Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,556
7,318
Wadau wa JF, Habari za weekend!

Naomba mnijuze mjuao: Jana Jumamosi nimesoma gazeti la mwananchi; topic inayosema Sita Avunja Ukimya ambamo Mheshimiwa Spika, Anne Makinda, amenukuliwa akisema: "...Kwanza sijui kama kuna mafisadi kwa kuwa fisadi ni mwanamume anayeiba mke wa mtu". Huyu mama mheshimiwa alikuwa na maana gani? je hii ndo maana mpya ya neno fisadi? Je ni kweli kuwa hajui kuwa kuna mafisadi?

Si ni huyu huyu aliyewahi kusema: “Inashangaza kusikia na kuona kikundi cha Watanzania wachache wakifanya kazi ya kuwasafisha mafisadi wakati wanatambua kuwa ufisadi unaangamiza taifa zima. Mimi nawataka Watanzania waendelee kulivalia njuga suala hilo ikiwa ni pamoja na kuliombea taifa kwa Mungu ili aweze kuteketeza shetani ufisadi,”

Si huyu huyu aliyewahi kusema: “Kwanza ningependa kuwapongeza wananchi wangu wa Njombe pamoja na Watanzania wengine wote ambao mmekuwa mkifuatilia vikao vya Bunge...Bunge la sasa halijalala kwani wenyewe ni mashahidi na mmekuwa mkishuhudia wabunge wanavyofichua ufiasadi,” (TZ Daima July 7). Yangu macho, Yaani mama ameshasahau kuwa yeye mwenyewe ameshawahi kuonyeshwa kukerwa na ufisadi an mafisadi. Mimi naona mama katumwa.

Wadau mnisaidie, huyu mama na hii definitionn yake mpya ya ufisadi ni vipi?

Sasa naanza kuamini kuwa mafisadi wamemtuma!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom