Anne Makinda enough is enough tumechoka na Bunge lako la hovyo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anne Makinda enough is enough tumechoka na Bunge lako la hovyo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mazoko, Jul 29, 2011.

 1. Mazoko

  Mazoko JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 676
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nasema wazi Anne Makinda hana la kujivunia na pengine hata wanahistoria hawana la kuandika juu ya mwanasiasa huyo ambaye ni dhahiri sasa nyota yake inazidi kufifia kila sekunde.
  Yanayoendelea na yatakayoendelea kutoka Bungeni ni ushahidi wa wazi wa udhaifu wa spika Makinda, Job Ndugai, Jenista Mhagama na Simbachamwene ambao kwa nyakati tofauti wameonyesha dhahiri kuwa sasa wameshindwa kazi.
  Sitaki kuibua malumbano yasiyo na tija bali nataka niweke wazi kuwa tatizo si wapinzani bali udhaifu wa Makinda na wasaidizi wake.
  Ni mwehu gani leo hii hakumbuki mikiki ya Dr Slaa wakati wa spika Sitta? je yalitokea haya tunayoyaona sasa? je nikisema Sitta “KAMFUNIKA” Makinda nitakuwa naongopa? NARUDIA TENA tatizo ni Makinda na wasaidizi wake!
  Tangu awali wenye kuona mbali walitoa angalizo kuwa spika aliyechaguliwa kwa kigezo cha jinsia “HAFAI” na leo hii wote tu mashahidi kuwa sasa “MAKINDA ANAWABEBA WALIOMBEBA” amelivuruga Bunge na kweli limevuruga .
  Kawafanya wapinzani kuwa na roho ya “KUPAMBANA” dhidi yake na wasaidizi wake na kwa bahati mbaya hana uwezo wa kulitatua hili si yeye wala “wasaidizi wake”
  Watanzania hawapaswi kushangaa “eti wabunge wanataka kupigana” nini cha ajabu? au Deo Filikunjombe kutaka “kupigwa makofi?” lipi la ajabu? Lema, Msigwa na Lissu kutolewa nje ya Bunge? nini cha ajabu? pendekezo la wabunge kupimwa akili? haya yote hayana budi kutokea, hebu jaribu kufikiria haya yasipotokea watanzania mtaamini vipi kuwa “HII NI NCHI LEGELEGE?”


  Mungu Ibariki Tanzania, Amin
   
 2. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Juzi alikuwa London na WIGI zake
   
 3. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Unasema kweli. Lakini ujue kuwa huyu ameletwa na watu kwa masilahi yao. Unategemea nini?
   
Loading...