Anne Makinda aifanya CCM kukiri kuanza kushindwa, kwa ku-surrender vita ya propoganda bungeni

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Ukiachilia mbali coverage kubwa waliyo-enjoy CCM kwa kutumia Radio Tanzania, kisha TBC, hata lile jina WANAMTANDAO lililoibuka mwaka 2005 ni kutokana na lile kundi la CCM kuweza kutumia vizuri propoganda kwa njia kutumia network devices yaani mitandano kama simu, SMS, email, fax nk.

Hadi Kikwete anaingia madarakani CCM walifaulu vizuri vita ya vyombo vya habari. Kumbuka hata JK alipotimiza siku 100 ndani ya Ikulu ziliandikwa articles nyingi kuhusu yaliyofanyika ndani ya siku hizo.

Leo dakika chache zilizopita kulikuwa na kuomba miongozo mingi pale Bungeni. Spika Anne Makinda imebidi aseme kuwa miongozo imekuwa ni mingi na inakula ovyo muda wa bunge. Lakini akaeleza kuwa waomba miongozo wengi ni wapinzani.

Hadi hapo sikuona tatiz kwa hoja ya spika maana hata kama ni wapinzani bado wana haki ya kuomba mwongozo hata kama ni mara 100 kwa siku.

Hoja ninayowasilisha hapa ni kauli ya Spika kwa vyombo vya habari. Anne Makinda amekiri kwamba vyombo vya habari vimekuwa havimtendei haki yeye Spika na wasaidizi wake kuhusu suala la miongozo. Kwamba vyombo vya habari badala ya kujikita kwenye kanuni wao wanakazana kuandika kwamba Spika anawaonea wapinzani.

Ukiachana na ukweli au uongo wa kauli hii, kinachoonekana ni kwamba sasa mlalamikaji kuhusu vyombo vya habari amebadilika. Zamani mlalamikaji alikuwa ni vyama vya upinzani. Kwamba vyombo vya habari vimekuwa vikiipendelea CCM na taasisi zake na viongozi wake.

Leo, Spika ni mwana CCM. Malalamiko ya Spika kwa vyombo vya habari si suala dogo. Hebu tuangalia magazeti nane yafuatayo:

1:
UHURU
2: DAILY NEWS
3: SUNDAY NEWS
4: JAMBO LEO
5: HABARI LEO
6: TAZAMA TANZANIA
7: RAI
8: MTANZANIA​


Hivi kweli mama yetu Anne Makinda anapolaumu vyombo vya habari, moyoni mwake kweli kunaweza kukawa na kimoja kati ya hivyo nane hapo juu? Sijui mwenzangu unasemaje lakini mimi sidhani kabisa kama ni kati ya hivyo. Hapo sijaweka Radion na TV kama vile TBC, Clouds na vingine vyote vyenye similar allegiance.


Hii maana yake ni nini? Lugha ya malalamiko siku zote ni phsychology ya kutambua anguko lako. Kwamba uwezo wa kushindana umekwisha sasa umebaki uwezo wa kulalamika na kulaumu.

Hapa maana yake ni kwamba vyombo ambavyo ni watetezi wa CCM ni wazi kwamba vimeelekea kushindwa vita ya propoganda vilivyoi-enjoy kwa miaka mingi.


Vyombo vya habari vimekuwa silaha ya CCM kwa miaka kadhaa. Sasa, wao wenyewe wanakiri kuishindwa silaha hiyo.

Maana nyingine ni kwamba chombo cha ushindi kimoja baada ya kingine cha cCM vinaanza kutekwa na wapinzani. Sijui hali itakuwaje kufikia 2015.

Jadili.
 
Kwani anadhani watanzania hatuwaoni jinsi wanavyokandamiza vyama vya upinzani? Akitukana upinzani ni kosa akitukana ccm sawa tena wanashangilia km watoto, nadhani km hataki tuone aanze na kuifungia TBCCM isionyeshe bunge live pengine ndipo akilalamika tutamkubalia
 
Kwani anadhani watanzania hatuwaoni jinsi wanavyokandamiza vyama vya upinzani? Akitukana upinzani ni kosa akitukana ccm sawa tena wanashangilia km watoto, nadhani km hataki tuone aanze na kuifungia TBCCM isionyeshe bunge live pengine ndipo akilalamika tutamkubalia

Hakuna mbunge wa CCM anayetaka bunge lionekane kwenye TV. Hili walilazimika wafuate desturi ya mabunge duniani kwamba ni lazima parliament session iwe live on air.
 
Hizi ni zama tunazotembea na TV na PC kwenye mifuko ya mashati yetu. Hizi si zama za waziri mkuu kusema liwalo na liwe. Makinda anapaswa kufahamu vema kuwa propaganda haina nafasi tena kwenye kizazi hiki.
 
Worse enough..kawatukana kwamba wanaandika upuuzi. Ingekuwa nchi zingine ambako media ina nguvu leo ndio ungekuwa mwisho wake wa kuwa spika huyu bi kiroboto.
Lakini kwa makanjanja wetu hawa haina shida life goes on!!
 
Worse enough..kawatukana kwamba wanaandika upuuzi. Ingekuwa nchi zingine ambako media ina nguvu leo ndio ungekuwa mwisho wake wa kuwa spika huyu bi kiroboto.
Lakini kwa makanjanja wetu hawa haina shida life goes on!!

uh,,,,,wagome????kwan wanajua umuim wa taaluma zao???
 
Hakuna mbunge wa CCM anayetaka bunge lionekane kwenye TV. Hili walilazimika wafuate desturi ya mabunge duniani kwamba ni lazima parliament session iwe live on air.
Nakubaliana na wewe mkuu,kwanza wanakera halafu kuna Tbc radio hivi ni kwa niniradio wasirushe bunge muda wote kwa sababu wenye access na tv ni wachache siku hizi kuna simu zina redio so ukiwa na earfone unapata taarifa na mambo yanavyoenda sasa wanajaribu kutuzuia tusipate mjadala LIVE ili tusiwasikie wanavyofanya ubabe wao,hata kama tutaibia ibia tu tatawajua wanachokifanya......
 
wayafanyayo twaona wazi hapo ndo shida kwani walitaka yaonekane na wabunge tu. Wanaolala, wanaozomea, wanaotoroka, wanapongeza wote wapo wazi. siku hizi karibu tutajua hata kuwa kile kiti ni cha nani hata kama hayupo, atafute njia nyingine ya kulalamika. hata sasa twajua ni wakati akiwepo nani mijadala itaenda sawa kati ya Makinda, Ndugai, Mhagama ama Zungu
 
siku hiyo mi nilikuwa naangalia runinga, hoja zote za miongozo , zilikuwa za wapinzani, na nilivyona mimi, hoja kama ya mkosamali kutaka spika amwamuru mbunge kyiseri chambiri kufuta maneno ya wabunge vijana hawajui nchi ilikotoka kwa kudharau mchango na maendeleo , lilikuwa jambo la msingi mno.sababu linapingana na katiba ambayo inatambua wabunge kuanzia umri wa mika 21.Kwahiyo badala ya kutoa mwongozo wa kumwamru kyiseri chambiri anatamka spika hafundishwi kufanya kazi yake>sasa hapo nani ambaye navunja kanuni, wabunge wa upinzani au yeye spika?hapa kuna haja kiongozi wa upinzani bungeni kuandika barua ya kuwatendea haki wapinzani kikanuni, vinginevyo wasiwe na imani naye.
 
huyu alishashindwa kuongoza bunge muda mrefu tu yaani yupo yupo tu...na mtu aliye mbumbumbu na hewa kichwani huwa anatumia mbinu za makinda ..akiombwwa miongoza anakuwa mkali ,kushusu taarifa anakuwa mkali ..dawa yake ni kuchana mistari tu hata akikataza unaendelea tu mpaka umalize
 
Back
Top Bottom