Anne Makinda achachamaa na takrima kwa wabunge..................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anne Makinda achachamaa na takrima kwa wabunge.....................

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 23, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,234
  Trophy Points: 280
  Makinda: Nitawaondoa wabunge watakaopokea takrima, posho mbili Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 21:11

  Sadick Mtulya
  SPIKA wa Bunge, Anna Makinda, amesema atawaondoa kwenye Kamati za Kudumu za Bunge, wabunge watakaobainika kupokea posho mara mbili kutoka taasisi au mashirika ya umma.

  Pia, Makinda alieleza msimamo wake kuwa, ni kutowavumilia na kuwachukulia hatua za nidhamu wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge, watakaopokea takrima kwenye ziara zao.

  Alitoa onyo hilo jana wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, alipokuwa akifungua semina ya mafunzo kwa wabunge wa kamati za Bunge zinazosimamia mapato na matumizi ya fedha za umma.

  Semina hiyo inayozihusisha Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali ( PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeratibiwa na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Spika alisema itakuwa kosa kubwa kwa wabunge kupokea posho mara mbili au takrima wanapofanya ziara kukagua uendeshaji mashirika mbalimbali na idara za serikali na kwamba, hatua hiyo inazorotesha utendaji wa kamati.

  "Kitendo cha kupokea posho mara mbili au takrima kinaathiri kwa kiwango kikubwa usimamizi na ukaguzi wa mashirika haya, maana wabunge wakipokea posho za Bunge na zile zinazotolewa na mashirika yanayokaguliwa hushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo,” alisema Makinda na kuongeza:

  “Katika hili wabunge watakaobainika nitawachukulia hatua za nidhamu ikiwamo kuwatoa kwenye kamati zao.’’

  Alisema atatumia Kanuni za Bunge zinazozuia wabunge kupokea takrima yoyote wanapotembea mashirika wakati tayari ziara zao zinakuwa zimelipwa na Bunge.

  Alisema licha ya wabunge kukumbwa na vishawishi vingi, ofisi yake itajitahidi kwa kadri itakavyowezekana kuboresha maslahi ya wabunge awamu kwa awamu ili kuwaondoa kwenye hali hiyo.

  “Nafahamu kwamba posho zenu hazitoshelezi, lakini naomba kwa sasa mkubaliane na hali halisi kwa kuzingatia mazingira halisi ya wakati huu,’’ alisema.

  Awali, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, alisema kamati ya PAC, LAAC na POAC zinakabiliwa na changamoto mbalimbali na kwamba, ili ofisi yake ifanye kazi kwa ukamilifu anategemea ufanisi wa kamati hizo.

  “Baadhi ya changamoto za kamati hizi ni muda wa kutosha kufanya kazi za ukaguzi, wataalamu wa kutosha kuziwezesha kufanya utafiti wa kina kufuatilia utendaji wa serikali na taasisi zake, licha ya ukosefu wa fedha na vitendea kazi vya kutosha kuziwezesha kutimiza majukumu ipasavyo,’’ alisema Utouh.

  Hata hivyo, Utouh alisema kamati za Bunge, Bunge lenyewe na ofisi ya CAG, vinahitaji uhuru wa fedha na utendaji ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,234
  Trophy Points: 280
  Wabunge wanaoendekeza posho kukiona
  Imeandikwa na Namsembaeli Mduma, Bagamoyo; Tarehe: 23rd February 2011 @ 07:19 Imesomwa na watu: 26; Jumla ya maoni: 0  KATIKA jitihada za kulinda heshima ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuhakikisha kuwa linatekeleza majukumu yake kwa umakini bila kutanguliza maslahi binafsi ya wabunge, Spika Anne Makinda ametangaza kuwaondoa kwenye kamati za usimamizi wa fedha, wabunge watakaobainika kuomba au kupokea posho na takrima kutoka kwa wanaowakagua kwa kuwa zitawanyima uhuru wa kufichua ubadhirifu watakaobaini.

  Vilevile, amesisitiza kuendeleza vita dhidi ya wajumbe wa kamati za Hesabu za Serikali (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) watakaothibitika kuwa ‘mizigo' kwa kamati hizo, kwa kuendekeza utoro vikaoni au kutokuwa na msaada wowote kwa kamati na watakaotumia nafasi zao kibabe na kuwatendea kinyume wanaowakagua, kwa sababu watakuwa ni watovu wa nidhamu na wavunja sheria.

  Akifungua mafunzo ya siku nne maalumu kwa ajili ya wajumbe wa kamati hizo kuhusu masuala ya usimamizi wa hesabu za umma yaliyoratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT) kwa udhamini wa Benki ya Dunia (WB) mjini hapa jana, Spika alisema uzoefu wake wa miaka minane akiwa mjumbe wa kamati za Bunge za fedha za umma na baadaye Mwenyekiti, unamfanya atilie mkazo umuhimu wa nidhamu kwa wabunge.

  Alisema: "Endapo nidhamu yenu itakuwa chini, hamtatekeleza wajibu wenu ipasavyo na wala hamtahofia kuomba posho mbili na kupokea takrima kutoka kwa mnaowakagua.

  "Ni lazima mkatae kupokea fedha hizo na mkubaliane na hali halisi ya maisha kwa kufanya kazi zenu za ukaguzi wa mapato na matumizi ya hesabu bila kutanguliza maslahi binafsi. Nidhamu iwe silaha yenu ya kwanza, bila nidhamu mtaaibika na kuliaibisha Bunge zima".

  Makinda alisema anafahamu kuwa posho za wabunge hazitoshi, lakini hiyo haimaanishi kuwa wawe ombaomba wa posho nyingine kutoka kwa wanaowakagua wala takrima, kwa kuwa watalazimika kuficha maovu ya watakaowalipa posho hizo na hivyo kushindwa kufanya kazi waliyotumwa na wananchi.

  "Tunashughulikia tatizo la posho zenu ndogo, ninawaomba sana mwepuke kulishushia Bunge letu heshima kwa kutanguliza maslahi yenu binafsi badala ya yale ya umma, sitahofu kuwaondoa wote watakaobainika kujihusisha na uvunjaji wa nidhamu kwa kuombaomba na kupokea posho hizo na nitawaondoa bila kujali tulichowekeza kwao katika mafunzo tunayowapa kila mara.

  Makinda alisema, ingawa kutobadilisha wanakamati kila mara kunabana matumizi, haitakuwa na maana kama watakuwa wanaficha ubadhirifu au kuendekeza utovu wa nidhamu.

  "Na wale watakaokuwa wasindikizaji na mzigo kwa wenzao nao nitawaondoa, nataka wanakamati muwe wachapakazi wenye kujali muda, kuhudhuria vikao vyote na kuokoa fedha za umma zisitumike vibaya, jipangeni kwa uchache wenu mtembelee miradi yote nyeti na si kuishia kukagua vitabu pekee.

  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, aliahidi kushirikiana nao kwa karibu na kufanya kazi zake kwa uhuru, huku akiuweka bayana ubadhirifu wowote atakaobaini.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,234
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Makinda alisema anafahamu kuwa posho za wabunge hazitoshilakini hiyo haimaanishi kuwa wawe ombaomba wa posho nyingine kutoka kwa wanaowakagua wala takrimakwa kuwa watalazimika kuficha maovu ya watakaowalipa posho hizo na hivyo kushindwa kufanya kazi waliyotumwa na wananchi

  "Tunashughulikia tatizo la posho zenu ndogo, ninawaomba sana mwepuke kulishushia Bunge letu heshima kwa kutanguliza maslahi yenu binafsi badala ya yale ya umma, sitahofu kuwaondoa wote watakaobainika kujihusisha na uvunjaji wa nidhamu kwa kuombaomba na kupokea posho hizo na nitawaondoa bila kujali tulichowekeza kwao katika mafunzo tunayowapa kila mara. 
  Hivi huyu Makinda yupo dunia ipi.........................anatakiwa katika tathmini yake aunganishe na mishahara minono ya wabunge huku akilinganisha na kipato kidogo cha raia ili kufikia katika hitimisho la ya kuwa posho za wabunge hazitoshi....................
   
Loading...