Anne Kilango: Wanataka kuniua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anne Kilango: Wanataka kuniua

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Jun 15, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  VITA vya kuwania ubunge Jimbo la Same Mashariki vimechukua sura mpya baada ya mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango-Malecela kudai mpinzani wake anataka kumaliza maisha yake na uzao wake.

  Kilango amekimbilia makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutaka kiinglie katika vita hivyo.

  Tayari Kilango amemshitaki Dk. Michael Kadeghe, aliyejitokeza kuchukua jimbo hilo, kwa Katibu Mkuu Yusuf Makamba.

  Anadai mwalimu huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anaandaa mazingira ya kutaka kumfunga.

  Mpaka sasa Dk. Kadege ndiye amejitokeza waziwazi kupambana na Kilango katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Same Mashariki.

  "…Nina uhakika mkubwa huu mkakati nisingeugundua ungenimaliza maisha yangu na uzao wangu," anaeleza Kilango katika barua yake kwa Makamba.

  Kilango amedai katika barua yake kwa Makamba kwamba Dk. Kadeghe na watu asiowajua, wamefanya njama za kutaka kumfungulia kesi ya jinai ili wamfunge.

  Mbali ya barua, Kilango ambaye ni mmoja na wabunge machachari, amewasilisha kama ushahidi, mkanda wa CD wenye sauti anayodai ni ya Dk. Kadeghe.

  "Nawasilisha kwako kanda yenye mazungumzo yenye mkakati uliotayarishwa na Ndugu Dk. Kadeghe na wenzie nisiowajua katika mazungumzo ambayo yamerekodiwa," anaeleza katika barua yake.

  "Hapa kuna kauli anayosema ‘tuna mkakati wa kumshitaki yule mama, lakini tunaona sasa siyo wakati mwafaka tutaleta malumbano," imesomeka sehemu ya barua ya Kilango iliyotiwa saini Mei 4, mwaka huu.

  Kilango anahoji, "Swali, kama nina makosa yanayostahili nishtakiwe kwa nini wasifanye hivyo, wafanye kusubiri wakati mwafaka ni upi?"

  Sehemu ya barua hiyo ambayo MwanaHALISI imeona inasema, "Ni moja kwa moja wananitengenezea kesi ya jinai, wanayoijua wao. Mwenyezi Mungu ni mkubwa sana na ndiyo maana anaitwa Mungu. Nina uhakika mkubwa huu mkakati nisingeugundua ungenimaliza maisha yangu na uzao wangu."

  Nakala za barua hiyo zimetumwa kwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu, Pius Msekwa na mwenyekiti wa CCM (W) Same, August Kessy.

  Makamba hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini Makamu Mwenyekiti CCM, Pius Msekwa amesema suala hilo halijafika mezani kwake. Amesema kiutaratibu mambo kama hayo huanzia kwa katibu mkuu.

  Naye Dk. Kadeghe alinukuliwa na vyombo vya habari wiki iliyopita akisema CD ya Kilango ni "feki."

  Katika CD yenye sauti inayodaiwa kuwa ni ya Dk. Kadeghe, kuna maneno, "…opposition (upinzani) walishinda lakini ukafanyika ujanja". Kama hivyo ndivyo, Peter Kuga Mziray aliporwa ushindi.

  Siku Kilango alipoandika barua kumshtaki Dk. Kadeghe, ndiyo siku uliposambazwa ujumbe wa simu ya mkononi ukidai mbunge huyo amesambaza kadi feki kwa lengo la kupata watu wengi zaidi wa kumpigia kura za maoni.

  "Huu ni uzushi. Leo nimezungumza na mwenyekiti wa CCM wilaya," anasema Kilango baada ya kuonyeshwa ujumbe unaosambazwa.

  "Uongo mtupu," aling'aka Kilango alipokuwa akihojiwa na mwandishi Ijumaa iliyopita.

  Ujumbe huo, ambao ulikuwa kiini cha habari nzito kwenye vyombo mbalimbali vya habari Jumamosi unasema, "Leo ukaguzi wa daftari la wanachama wa CCM umefanyika katika Jimbo la Same Mashariki.

  "Kadi feki kibao zimegundulika katika matawi yaliyo katika ngome Kilango. Kadi zimepatikana katika tarafa ya Mamba/Vunta; huko Goha, Myamba, Mbinji, Kirangare, na Vunta," ilisema sehemu ya ujumbe.

  "Mwenyekiti wa CCM (W) Same, makatibu na madiwani wametajwa kuhusika na kashfa hiyo ya kugawa kadi za CCM bure kwa lengo la kumsaidia Kilango ili apite katika kura za maoni," ulisema ujumbe ambao pia ulitumwa kwa Kilango.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, kadi feki zilipelekwa na Kilango mwenyewe na kuzikabidhi kwa watendaji wa CCM (W), madiwani, makatibu kata na matawi.

  Sehemu ya mwisho ya ujumbe huo mrefu inasema, "Ni mradi wa Kilango. Uhakiki ulifanywa na Katibu wa CCM (M) na Katibu CCM (W), Sofia Kilingo."

  Alipoulizwa Kilingo kuhusu madai hayo, alisema naye amesikia tu maneno ya kuwepo kadi feki lakini hajaona kadi hizo.

  "Huyo anayeeneza hayo maneno kuwa kuna kadi feki sijui alifanya ukaguzi wake lini na wapi. Mimi ndiye ninayefanya uandikishaji na uhakiki wa sasa," alisema Kilingo.

  "Hivi ninavyozungumza na wewe niko huku milimani katika eneo la Miamba na nikitoka huku nitakwenda Kihurio," alifafanua.

  Kilingo alitupilia mbali pia madai ya kilichoitwa kusudio la Kilango kushitakiwa.

  Tangu enzi za chama kimoja, kumekuwa na ushindani mzito wa kuwania nafasi ya ubunge katika majimbo mengine nchini. Kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kulifuatiwa na mbinu za kuchafuana zilizoshika kasi 1995.

  Jimbo la Same Mashariki lilipata mtikisiko wa aina yake mwaka 2005 wakati Kilango, Dk. Kadeghe, Naghenjwa Kaboyoka na wengine watatu walipoonyesha nia ya kumng'oa Mbunge wa wakati huo na Waziri wa Madini na Nishati, Daniel Yona.

  Kilango aliibuka mshindi katika kura za maoni ndani ya CCM, akifuatiwa na Kaboyoka, waziri Yona, huku Dk. Kadeghe akishika nafasi ya nne.

  Lakini, baada ya kuangalia alipojikwaa na njia ya kupita aweze kuibuka mshindi ndani ya CCM, Dk. Kadeghe, ambaye ni Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Perfect Vision iliyopo Dar es Salaam ameonyesha nia tena.

  Alipoulizwa iwapo hapendi ushindani jimboni, Kilango alisema, "Hapana. Hapa ninachosema ni kwamba zisiwepo hila. Dk. Kadeghe amepiga kambi mwezi mzima jimboni anajifananisha na mbunge aliyeko madarakani."

  "Twendeni kwenye uchaguzi kwa hoja zenye msingi; tutawafanyia nini wananchi, tutapambana vipi na umaskini wa wananchi na kumaliza kero zao," ameeleza Kilango.

  Amesema anataka watu wajue tofauti ya mbunge aliyeko madarakani na mwanachama wa CCM ambaye ameonyesha nia ya kugombea ubunge.

  "Sasa hivi, wakati wowote, napaswa kufanya mikutano ya hadhara na ya ndani kutatua kero za wananchi na kuibua miradi mpaka Bunge litakapovunjwa," anaeleza Kilango.

  Huku akionyesha kitabu kiitwacho "Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake: Jimbo la Same Mashariki 2005-2010", Kilango anasema mbunge makini anapaswa awe anafanya kazi kubwa sasa, hasa kama ni wa CCM.

  Anasema kupitia chama chake ngazi ya wilaya, anapaswa apite, kuanzia kwenye vitongoji, akieleza amefanya nini; madiwani wamefanya nini na serikali yake imefanya nini katika kipindi cha miaka mitano

  Anakiri kwamba kila mbunge ana staili yake. "Staili yangu ni hii, nimeandika kitabu na ndani yake nimeeleza nilivyotekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa maandishi; na kila diwani nimemwambia aeleze amefanya nini."

  "Kitabu hiki ndiyo silaha ya CCM katika jimbo langu. Akija Chadema au nani silaha ni hii hapa. Nakala 10,000 ziko mikononi mwa wananchi," anaeleza kwa njia ya kujigamba.

  Kilango anasema alikuwa na kikao na mwenyekiti wa CCM (W) wiki nne zilizopita kupanga mikakati; lengo likiwa kutompa mtu yeyote fursa ya kudai kuwa CCM haijafanya kitu.

  "Kwa hiyo, yule aliyeonyesha nia ya kugombea kupitia CCM yuko mbali na mbunge aliyeko madarakani," alijinasibu.

  Katika kitabu hicho cha kurasa 54, MwanaHALISI ina nakala yake, Kilango ameeleza alivyoshiriki kubuni na kuchangia miradi ya ujenzi wa shule za msingi, sekondari za kata za kidato cha nne, sekondari za kata za kidato cha sita, zahanati, kuchimba visima na kujenga barabara.

  Kwa mujibu wa kitabu hicho, Kilango amechanga fedha taslimu, matofali, mabati, saruji, mbao, kuwalipa mafundi na kugharimia usafirishaji na ugawaji wa vitabu vya kiada na ziada. Vilevile amechanga fedha na vifaa kwa wakazi waliokumbwa na mafuriko.

  Hata hivyo, anakiri kwamba CCM ilifanya kazi ya ziada kupata ushindi mwaka 2005 kutokana na mgombea wa ubunge kupitia PPT Maendeleo, Peter Kuga Mziray kujikita hadi ngazi ya chini. CCM ilishinda kwa asilimia 62 tu.

  "Kwa mwanasiasa yeyote aliye makini, PPT Maendeleo mwaka 2005 ni vyema tukubali ilisumbua Jimbo la Same Mashariki na isingetumika siasa ya uhakika na iliyopevuka jimbo lingeweza kuathirika zaidi," anasema.

  Tangu wakati huo Kilango alichukua ajenda za chama hicho cha upinzani na kuziweka kama dira yake.

  Anasema, "Ndugu Kuga agenda zake zote nilizichukua kama dira yangu ya kufanyia kazi jimbo langu na pia kama dira yangu kubwa ya kukidhoofisha chama chake jimboni."

  Chanzo: Mwanahalisi


  My take: Kaza uzi mama, you are a real fighter among many. Hii ndiyo price one pays kupambana na maharamia wa ufisadi. You will succeed.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Duh Mwalimu wa University anang'ang'ana na yeye kuwa mhishimiwa mbunge..Kweli bongo tambarare.
   
 3. Wa Mjengoni

  Wa Mjengoni JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijui kuna nini kwenye huo mjengo maana kazi imekuwa ndio hiyo hiyo kwa kila mtu aliyesoma sana na hata aliyesoma kiasi. Mi naona tungepunguza mshahara tungepata wabunge wenye wito haswa wa kuingia humo!
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Na bado, manyang'au wataumbuana sana mwaka huu - tusubiri tu kwani si ajabu na Tinga Tinga nayo ikashindwa kuwaka, tuendelee kukaa tukisubiri !
   
 5. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anne pambana Kadeghe hana lolote asikutishe na Udaktari wake...unaweza mbona kumshinda huyu! au amekuwekea watu wakukuchanganya? maana kuna mbinu inayotumikaga mpinzani wako ananunua watu unaowaamini na walio karibu halafu wanakuletea habari za kukuvunja moyo na kukuchemsha ili udate ushindwe kupanga mikakati....Anne be careful .....uwezo wa kumshinda unao

  Mix with yours
   
 6. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,835
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Huyo anatumiwa na mafisadi!
  Huyo mwl english hana hata chembe ya aibu! Kama unataka challenge si upambane ki-halali!
   
 7. a

  afande samwel Senior Member

  #7
  Jun 16, 2010
  Joined: Mar 13, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huu ndiyo upumbavu mkubwa.Kila anayejitokeza kugombea, katumwa na mafisadi?So stupid. wasomi kuwa na idea ya kijinga namna hiyo.Watu watashindwa kutumia demokrasia yao,eti wametumwa na mafisadi.
  Kama yeye hana kesi, sasa anaogopa nini?.
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Aaaagh, ndo hao hao wa kila siku, hawana mpya!
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Watu wakiguswa sehemu mbaya ndo hivi wanakuwa wakali....Mambo ya utetezi wa maslahi ya nchi yamewekwa kando!...Mungu saidia inji hii!
   
 10. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa huo ulikuwa mchango wa bajeti ya waziri mkuu au mipasho ya kuelekea uchaguzi, Mama alikuwa off point hapa, ila mwaka huu hata watoto watapata shikamoo kutoka kwa wazee.:hungry:
   
 11. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 60
  Alipokuwa anapambwa na Nipashe na Mwanahalisi kila siku mbona wenzake hawakulalamika?

  Ukipanda sifa kupitia magazeti, utashushwa na magazeti hayo hayo. Yeye aache kulia lia na apambane tu maana hizo ndio siasa.

  Si tuliambiwa hapa kwamba yeye anatembea na waandishi wa habari kila sehemu? Si wamsaidie kujibu mapigo?

  Anamlaumu bure Mkamba kwenye hili. Kilango na wenzake wametumia sana magazeti kuchafua wenzao kwa kusema wanatumwa na mafisadi. Sasa vibao vikielekezwa kwao waache kulia. Si wanasema siasa zina fitna?

  Hata hana akili eti ambaye hatapitia CCM atarogwa? CHADEMA nendeni tu mkampe kipigo chake huyu mama.

  Amwite mzee ES akamsaidie kumtetea na kurusha mpaka matusi ya nguoni.
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mama Kilango ana wasiwasi gani wakati kafanya mema mengi tu kwa watu wake? Yeye ajikite tu kwa watu wake. Nilidhani kwa hadhi yake na umaarufu wake sio tu angepita bila kupingwa huko Same bali hata Ubungo, Rorya, Geita,...... kama alivyo Zitto.
   
 13. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Na naanza kwa kuitikia namna hiii Marahabaaa Mzee wangu hujambo eeh? :becky: Mbona burudani!
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Unajua ukiona mtu anabwata akiona challenge muangalie tia shaka umakini wake. Inaelekea huyu mama anachimba mkwala ili aliyejitokeza aogope mama pambana naye jimboni sio katika magazeti
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hUU UCHAGUZI WA MWAKA HUU NI KASHESHE TUPU YETU MACHO ..
   
 16. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #16
  Jun 17, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo umenena Mdondoaji. Watakuja wengi wa aina hii. Mlikwinaaa??????
   
 17. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mhh yangu mijicho tu
   
 18. Q

  Qadhi JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Binafsi napata taabu mno kuelewa hawa wanasiasa hususwan Wabunge na viongozi wa vyama upinzani.Wabunge wanajua wazi shida za wananchi wao tena kwa kujionea wenyewe,pesa wanazopata ni nyingi sana ukilinganisha na kipato cha mwananchi wa kawaida.
  Kwa mtizamo wangu, kama kweli wangekuwa na uchungu na hao raia,wangeanzisha hata miradi yenye faida ndogo kwao ambayo aidha itawaelimisha wananchi namna ya kuwekeza katika mali zao za asili au itawasaidia kutatua baadhi ya matatizo yao moja kwa moja.
  Nimetembelea baadhi ya maeneo Tz nikaona kuna possibility ya kuweka miradi mingi midogomidogo kama vile:

  • Mabwawa ya samaki

  • Low scale irrigation schemes.Hapa twahitaji vitendea kazi affordable kwa kipato cha wabunge,just vitu kama powertillers,water pumps...ambavyo si zaidi ya laki 5 tshs kila item
  Just to mention a few.

  Wapinzani nao:
  Ukisikia uchambuzi wa namna ya ku utilize our natural resources unaofanywa na Mtaalam wa Uchumi Prof.Lipumba,jamaa huwa anaanzia kwenye matunda yanooza kila kona ya Tanzania hadi madini yanayochotwa hata na Wachina(kweli Tz ni jamvi la wageni..inakera mnoooo).

  Nina hakika kuwa kama Prof.Lipumba akiamua kweli kuwasaidia Wananchi,kwa influence yake aliyokuwa nayo duniani na ruzuku wazipatazo angeweza kusimika schemes kadhaa ambazo directly zitasaidia wananchi ambao asilimia 70% wanalalia hizo embe mbovu huko vijijini bila kujua cha kuzifanyia.

  Nimewataja wabunge na Wapinzani kwa sababu ndio wanaoitwa watetezi wa wananchi,hususwan ukizingatia serikali(executive) imeonekana kutofanya jitihada za kuwatoa wananchi katika lindi la umaskini tulilokuwa nalo.

  Hizi kelelekelele zinazopigwa sasa hivi na hawa wabunge zinatuzingua tu,badala yake waweke hiyo miradi hata kwa faida yao na bila kupoteza capital zao ili tunafaike wote pia kuinua sauti za wananchi ambazo sasa hivi zimefunikwa na njaa.watapata hata uniform za watoto,wata attend hata evening classes etc na pia huenda the executive itawafikia asubuhi na kuamka wakajua kumbe walikuwa wamelala fofo.

  Well,hamna noma,wewe Mbunge jiite mpiganaji hata kama uko pamoja na hao mafisadi,lakini huu upiganaji wako hauzii ku play part yako.

  Na nyie akina DR.Kadeghe,PROF.Lipumba,DR.Mwakwembe,PROF.Mwandosya...(connect the dots) hebu angalieni mfano huu:

  Hii ndio hali halisi iliyopo katika siasa za Tanzania.....how can poverty and democracy co exist?
  "
  Kong'oli hapa

  Nimechanganya na zangu...lol
  Qadhi
   
 19. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Anne Kilango.....Crying Wolf ? ? ? ?:tsk::tsk::tsk:
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mdau Br. Qadhi, maelezo yako nadhifu.

  Kumfananisha thinker Muhammad Yunus na wachumia tumboni akina Mwandosya na Mwakembe et al, ni kumtusi kwa herufi kubwa Dr.Yunus.

  Nilishatoa rai kwamba Tz haihitaji wabunge wala wanasiasa, sababu ninazo japo nyingine sitaziweka wazi kwa sababu fulanifulani. In stead nilishauri ni vyema wataalam wa huko mawilayani wawe empowered ktk mifumo ya taarifa (IT), sera na ujuzi..wangeweza kufanya kazi bora zaidi ya kuwakilisha mawazo na matatizo ya wananchi kuliko mchezo wa kuigiza unaofanywa na watu kati - wabunge, kwa gahrama ya juu, ambao hata hivyo HAWANA TECHNICAL KNOWHOW..bali kazi kujitiatia tu wengine hata kuumba hati hawajui.

  Way forward kwa nchi yetu kupiga hatua ni kuondoa taratibu INFLUENCE YA SIASA na mwisho kufikia taifa ambalo linaendeshwa na mifumo ya kufikia maamuzi na sio kufanya maamuzi.
   
Loading...