MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,772
- 4,054
MBUNGE wa Same Mashariki, ameponda mfumo wa kuwapata mawaziri na kupendekeza kuwa wachaguliwe na wananchi kama ilivyo kwa rais.
Soma habari kamili hapa:
MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ameponda mfumo wa kuwapata mawaziri na kupendekeza kuwa wachaguliwe na wananchi kama ilivyo kwa rais.
Wakati Kilango akisema hayo kwenye uzinduzi wa ripoti ya kujipima kwa kutumia vigezo vya utawala, mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa amesema nchi itavurugika kutokana na muswada wa sheria ya udhibiti wa fedha za uchaguzi unaoandaliwa kuwasilishwa kwenye mkutano ujao wa Bunge.
Kauli ya Kilango inatokana na ripoti hiyo ya Mfumo wa Kupima Utawala Bora wa Umoja wa Afrika (APRM) kutaja kwamba mchanganyiko kati ya Bunge na serikali unakinzana na kanuni.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa juzi na Naibu Spika Anna Makinda katika hafla iliyohudhuriwa na wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge jijini Dar es salaam, imeeleza mafanikio, mapungufu na mpangokazi wa kuyaondoa mapungufu hayo.
Tathimini ya ripoti hiyo iliyofanywa kuanzia mwaka 2007 hadi 2009 imesema: "Mchanganyiko kati ya mhimili wa Bunge na Serikali unakinzana na kanuni zinazotaka mamlaka hizi zitenganishwe kuhakikisha wabunge hawawi sehemu ya utawala, kwa maana kuwa wabunge wasiwe mawaziri wala wakuu wa mikoa."
Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa ripoti hiyo, Kilango alifafanua kwamba mfumo wa sasa wa upatikanaji wa mawaziri haukidhi haja na tija ya Watanzania kwa kuwa unatofautiana na ule wa kumpata rais.
"Tuukatae mfumo wa upatikanaji wa mawaziri ambao ni wa Commonwealth (Jumuiya ya Madola) kwa kuwa hauendani na ule wa kumpata Rais," alisema Kilango.
Kilango, ambaye ni mbunge wa jimbo la Same Mashariki, alifafanua kwamba mfumo wa kumpata rais nchini ni wa Kimarekani ambao rais anachaguliwa moja kwa moja na wananchi tofauti na mawaziri ambao huteuliwa na rais baada ya kuwa wabunge.
"Ni muhimu sasa kwa mawaziri nao wakachaguliwa moja kwa moja kutoka kwa wananchi, kwa kuwa mfumo wa kisasa wa utawala unaonekana kuegemea na kufuata mfumo wa Kimarekani ambao mawaziri huchaguliwa moja kwa moja na wananchi hivyo ni wakati muafaka mfumo huo ukatumika kuwapata mawaziri nchini," alisema Kilango.
Naye Makinda alisema mifumo yote miwili ni mizuri na ina faida na hasara zake.
"Kikubwa itabidi tuangalie na tujadili kwa kina ni mfumo upi una faida na tija zaidi kwa Watanzania, lakini mifumo hii inatofautiana kwa kuwa mfumo mmoja unamruhusu waziri kuwepo bungeni moja kwa moja na mwingine unamtaka aingie bungeni wakati kunapokuwepo suala au hoja inayohusu wizara yake," alisema Makinda.
Mbali na suala hilo, ripoti hiyo inayohusu utawala bora imeeleza kwamba kuwepo kwa mapungufu ya kutojulikana mahali fedha za kugharamia uchaguzi zinakotoka kunahatarisha uwepo wa ushindani katika uchaguzi.
Hivyo imependekeza kutungwa kwa sheria za kusimamia fedha zinazotumiwa katika chaguzi mbalimbali pamoja na kutoa elimu ya uraia na elimu ya wapiga kura ili kuondoa rushwa katika uchaguzi.
Akichangia hoja hiyo, mbunge wa Ukerewe, Dk Getrude Mongela alisema rushwa ya kisiasa ni hatari na inaweza kuchochea vita.
"Watu wanajua kwamba rushwa ipo na wanaiona lakini hawaikemei. Na ningependa nisema kuwa rushwa ya kisiasa ni hatari, italeta mfarakano wa kitaifa," alisema Dk Mongela.
Akizungumza na Mwananchi kuhusu hoja hiyo, katibu mkuu wa Chadema, Dk Slaa alisema kupitishwa kwa sheria ya kuweka wazi watu wanaochangia vyma vya siasa pamoja na kiasi, itasababisha vurugu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.
"Mantiki ya sheria hii ni nzuri katika ulinzi na usalama wa taifa, lakini dhumuni la kutungwa sasa kwa sheria hii ni tofauti na kuna mashaka makubwa hivyo uchaguzi utavurugika zaidi," alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alifafanua kwamba kuvurugika huko kutatokana na utofauti mkubwa wa uwiano wa vyanzo vya mapato baina ya vyama vya siasa.
Alisema kutokana na hilo vyama, hasa vya upinzani ambavyo kwa kiasi kikubwa vinategemea michango ya wanachama wao wenye uwezo mdogo wa kipato, vitakuwa katika wakati mgumu.
"Ukweli ni kuwa CCM ina vyanzo vingi vya mapato na hasa kutokana na kuwa na matajiri wengi na wakubwa tofauti na vyama vya upinzani, hivyo kutakuwa na wakati mgumu katika uchaguzi huo,"alisema Dk Slaa.
Katika hatua nyingine ripoti hiyo imeeleza kuwa kutotekelezwa kwa uamuzi wa kuruhusu mgombea binafsi, kunanyima haki ya msingi ya mtu kuchaguliwa.
"Ili kuweka hali hiyo sawa ni muhimu kupitiwa upya kwa sheria za uchaguzi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ya Zanzibar," imesema sehemu ya ripoti hiyo.
Tayari serikali imetangaza nia ya kwenda mahakamani kupinga suala la kuwepo kwa mgombea binafsi nchini baada ya Mahakama Kuu kubatilisha sheria inayokataza mgombea binafsi kwa kuwa inakiuka katiba ya nchi.
Akizungumza na Mwananchi kuhusu mgombe binafsi, Makinda alisema; "Tusubiri muda utafika na kila kitu kitakuwa sawa."
Katika hatua nyingine, ripoti hiyo imeeleza kwamba kamisheni za uchaguzi, Tanzania Bara (Nec) na upande wa Zanzibar (Zec), hazina uhuru wa kutosha na pia kuna ufinyu wa kupata haki za kisheria nchini.
CHANZO: MWANANCHI