Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Hili ni wazo zuri sana mama.
Huu ni wakati muafaka kwa kila mtanzania kuachana mara moja na utamaduni wa kuchangia harusi na sherehe nyingine zisizokuwa na tija kwa taifa na kuhamia kwenye kuchangia elimu kwa Mtanzania kwa manufaa ya Tanzania ya baadae.
Hakika wazo hili kama likipata msukumo unaostahili, tunaweza tusije kuzungumza tena hapa juu ya watoto wenye ufaulu wanaoshindwa kutimiza ndoto zao za kupata elimu ya juu.
Pesa hii ikishakuwepo, itatolewa kwa walengwa on academic merits. Kulingana na kiasi kitakachokuwepo, itasetiwa cut-off point ya mtoto atakaekuwa eligible kupata hiyo scholarship.
Tatizo ni baada ya hiyo elimu ikishapatikana, tukirudi mtaani tunakutana na changamoto mbalimbali nyingi zikiwa zimetokana na tatizo la mifumo yetu ya kiuchumi,kisiasa na kijamii.

Mtu anakaa bila kuweza kuitumia na kuikomaza elimu au ujuzi wake mwisho wa siku anarudi kufanya vitu vya kawaida tu kama kukatakata matunda na kuyauza(sipingi mtu mwenye elimu ataifanya hii kwa ujuzi wake hususan katika kuikuza na kupanua soko n.k), lakini kiwango cha nguvu ya takribani miaka 17 hadi 20 na kitu shuleni kinakuwa hakijawa na return na ukumbuke miaka yote hiyo wengi ni dependants wa wazazi au walezi wenye mishahara midogo/wastani(Hii inatuzungusha katika poverty circle).

Hili la elimu ya juu liendane na uboreshaji wa mazingira ya kujiajiri na kuajiriwa,otherwise tutakuwa tunasoma na kujaa mtaani na wapumbavu wakitutolea mifano kuwa kusoma sana hakuna faida.
 
Kweli tungepata viongozi wa aina hii katika nchi hii sijui tungefika wapi.

Tungekuwa mbaaali mno na pengine tungehama kutoka dunia hii ya tatu kwa kweli

Wengine nao wapo tu kujinufaisha wao katika ngazi zao

Jamani akina mama bila kujali itikadi yoyote ya vyama vyenu au chochote unganeni kulikomboa taifa,

Kuna shamba na kuna mbegu lakini mpandaji kakosa
Miaka ijayo tutakosa mavunobya wataalam na wajuvi mbalimbali hapo ndipo tutaanza kutafutana wapi tumekosea.

Leo vijana wengi wapo mtaani na si hivyo wwngine hawajui hatma yao aseee ungeni mkono hilo
R.I.P MAMA MAWAZO YAKO YATAENDELEA KUDUMU.
 
RIP mama Anna ulikua mtu smart sana japo ni Kati Ya Waasi wa Mageuzi Wa Mwanzo kabisa ukiwa na kina Mchange Mwigamba na wenzako
 
Nilihuzunika sana baada ya wanafunzi wenzangu wa mwaka wa kwanza kuondolewa kwenye chumba cha mitihani kwa kushindwa kulipa ada...chuo ni cha serikali..pamoja na kusoma kozi zenye kipaumbele (sayansi) bado mikopo tunaisikia kwenye bomba....ambapo ilikuwa vigumu kukosa mkopo kipindi cha jk kama unasoma masomo ya sayansi...

Tulitembea sana bale bodi ya mikopo bila kupata msaada wowote mpaka Dada mmoja miongoni mwa ofisi pale mapokezi aliposema mliambiwa elimu bure hadi chuo kikuu nyie mkachagua had I form 4. Niliondoka pale nikawapigia simu wazazi/walezi nikawaambia sasa ndio mwisho wangu wa elimu nimekosa mkopo naomba nirudi nyumban....
Wakajichanga wakapata ada wakaniambia wewe ni mtoto wa kiume hiyo ada matumizi mengine tutakuapatia Mungu akipenda....

Cha kusikitisha zaidi ni bodi pamoja na serikali yaani wizara kushindwa kusema ukweli juu ya mikopo...idadi kubwa ya wanafunzi tumekosa na wengi wamerudi majumbani kwa kushindwa kumudu gharama za masomo....
Sioni point ya kuwatoa wanafunzi ndani ya chumba cha mtihani, wangewaacha wamalizie mitihani yao then wawadai na hakuna kuwapa matokeo mpaka wamelipa au kuanza semister mpya lazima wamalize deni, wapuuzi kwelikweli huo uongozi wa chuo
 
Back
Top Bottom