Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Nilikuwa nawaza juu ya kutosikia speech yoyote kutoka kwa mama mpendwa. Ni kama Taifa limekosa dira namna ya kuwasaidia watoto wetu, too much politics has drained all good plans and sustain High Education loans. Ni kweli tunahitaji mjadala unashirikisha wadau wote. Tupo pabaya hadi sasa
Ninaikumbuka vema kauli ya mama Salma Kikwete kuwa nanukuu: " Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako." Leo watoto wa wenzetu wameingia tatizo la kukosa mikopo ya elimu ya juu; tuwasaidie kama watoto wetu.

Ninapenda kuwaomba akina mama wote nikianza na Mhe mama Salma Kikwete aliyeasisi usemi na hatua hii, tushirikiane kunusuru maisha ya elimu ya watoto walioko vyuoni wenye sifa ya kuwa na mikopo lakini hawakufanikiwa kupata mkopo. Tuwahamasishe vijana waliobakia mitaani na majumbani kujiunga na vyuo vikuu kuanua akili zao changa kukidhi ushindani wa sasa kimaisha.

Naomba akina mama wote viongozi, wazazi, walezi, wafanya bishara, waajiriwa, wanaharakati bila kujali itikadi zetu za aina yoyote tusimame kama wanawake wazazi wenye nia kuejnga taifa la watu walioelimika tuunde mfuko wa kuwasiadia watoto wetu wafanikiwe kumaliza masomo yao kwa ujenzi wa taifa letu.

Nikitoka na mama Kikwete ninaomba wake za marais wote waliopita kuanzia na mama Karume (mzee marehemu na Rais aliyemaliza mda wake) mpaka mama Janet Magufuli anayenivutia sana kwa kuonesha moyo wa amani sana kwa taifa letu.

Baada ya hao nimuombe mama Anna Makinda na wabunge wanawake wote waliopo na waliomaliza tangu uhuru wa nchi yetu tuungane kumsaidia kila mtoto wa Tanzania mwenye uwezo wa kusoma asome.

Kisha kwa niaba ya wanawake wafanya bishara niombe kitengo cha wanawake cha TCCIA, Baraza la Biashara la wanawake...tukubali wito huu: Tuungane kama wazazi na walezi chini ya kauli mbiu: Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako...tuunde mfuko wa elimu kwa ajili ya vijana wetu.

Niombe vyama vya wana-taaaluma: waalimu, madaktari, wahandisi, watumishi wa umma, mabenki, makampuni yote ya ndani na ya kigeni, asasi za kiraia za ndni na za kimataifa, balozi zetu zote, tuungane kuunda chombo hiki kuwasaidia vijana wetu.

Nimeguswa sana na mahangaiko ya vijana wa vyuo vikuu. Ninawashukuru wachache waliofika kwangu kueleza changamoto zao. Mmenihamasisha kuchangia kidogo elimu yenu lakini ninaomba hili liwe suala la kitaifa.

Ninaomba wanawake wenzangu popote tulipo tuwasiliane tuunde umoja huu kuwaimarisha na kuwapa tumaini vijana na janga la kukosa elimu ya juu kama wana sifa za kuipata.

Tuweke kando siasa, dini, kabila, ukanda ama aina yoyote ya kigezo kufanikisha jambo hili. Ninawashukru sana. Kesho kuna wanafunzi watashindwa kufanya mitihani kwa kukosa ada kidogo tu ya laki kuanzia 5-8. Mfuko wa mama Salma, Mfuko wa mama Mkapa wa Fursa sawa kwa wote, Taasisi ya Benjamini mkapa, Taasisi ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, na zingine, tusaidiane kukamilisha azima hii. Na mimi nimeanzisha Taasisi ya Mama Anna Mghwira kwa ajili ya kushughulikia masuala ya aina hii.

Nitawashukuru sana kwa niaba ya vijana wetu, tuenzi elimu yao kwa kuunganisha nguvu zetu hivi. Mnisamehe kwa kuandika mtandaoni. Nimejaribu njia za kawaida za simu sikufanikiwa sana. Hapa ninajua kila moja atapata taarifa. Mapungufu yangu yasizuie jambo hili kutendeka. Jinsi tulivyo changia madawati, sasatuchangie elimu ya juu.

Niombe wizara na Bodi ya mikopo ya wanafunzi kutoa ushirikiano tutakapouhitaji utaalamu muwe nasi bega kwa bega.

Mungu atubariki wote, aibariki Tanzania.

Asanteni tena, ni mimi mama Anna Mghwira
 
Nadhani sirikali inachoshwa na raia wake...wakulima wanakosa ruzuku,wafanyakazi hawatimiziwi haki kama madaraja kupanda nk. Wasanii hawasaidiwi kazizao kuwanufaisha,wanafunzi ndohivyo tena,elimu ya bure kwelikweli imekuwa sivyo michango inarudi. Hii ni sirikali ya watu kwaajili ya watu ama ya vitu na vituko?
 
Amina! Kila la kheri! And

We are behind you with full support.
Ningepependa kuzindua hii mapema ili mihula mipya inapoanza tuwe na kitu mkononi kwa wanafunzi wa awali...una mapendekezo yoyote? Tayari nina mwnafunzi mmoja mwenye tatizo sugu na tumejaribu kuchangishana na kumlipia term hii, na amefanikiwa kufanya mitihani baadhi. Bado deni ni kubwa, tusipomaliza atakataliwa mitihani mingine...kwa hiyo ni vizuri kuweka nguvu..ya ziada.
 
Alright! This sounds positive!

Then, naamini tayari una watu ambao wanafanya analysis na kuweka mipango ya mawazo ambayo unayapata hapa...

Weka mpango kazi mezani ili ukishaanza utekelezaji inakuwa ni rahisi kuwaeleza watu ambao humu hawapo lakini tunaamini watakuwa na moyo wa kuinua Elima kama wewe.

Uwe na safari njema.

You have our support...!
Amina, tunaendelea vizuri na mipango inakwenda vizuri pia...asante kwa kuonesha moyo huu...tuendelee tusonge mbele. Nia yetu ni watoto wote kadiri iwezekanavyo wapate elimu, wapate ujuzi, wajitambue, wajiamini, wajitume. Nchi itasonga mbele tu. serikali imefanya kazi yake. sisi raia tuongeze nguvu pale panapopungua, tuache kulalamika tu.
 
Ni kweli na ukizingatia teknolojia ya mambo ya kifedha imekua,Aliye Njombe au Kyerwa anaweza kushiriki. Mama,nashauri angalia zaidi mnaoendana kimawazo,ndo uwashirikishe kimkakati kwenye Menejiment ya usimamizi. Ukitaka tuwapendekeze, tuko tayari,tunawajua. Otherwise,nakutakia kila la heri.
Pendekeza tafadhali. Nina timu ndgo hapa arusha, lakini nguvu zaidi bora ni bora zaidi pia. Leta majina inbox if possible. email yangu ni aemghw@gmail.com
 
Mama yangu naomba hili wazo lako lisiishie humu JF kama umekusudia qweli kufanya hivyo naomba amka hata wasipo kusuport wanasiasa kuna wasanii , wanamitindo niseme tasnia ya michezo qwa ujumla watatoa support ya nguvu qwako ktk hili na hakika utakua umeokoa vizazi vilivyopo na hata vijavyo coz first year Waleo ndio taifa lijalo ..
Mama amka uanzishe project hii plz hata qwa mitatu utapata support na nchi nzima itaenea hii a idea yako na itasaidia sons and daughters of poor peasants
Miss, no problem tumeanza tutaendelea...Mungu atusaidie..
 
Maskini nchi yangu....
Natamani sana siku moja mama Anna mghirwa ushike nchi hii qwa roho na Huruma uliyonayo watoto wa maskini watapata ahueni ktk kusoma...coz umeelezea tatizo kma vile tuko wote pale chuoni jamani Kama kuna viongozi wanawake humu Jf embu unganneni na mama Anna mfanikishe hili hakika mtakumbukwa na kuzidishiwa thawabu na Mungu wa mbinguni...
Life la chuo bila mkopo asikwambie mtu haliendi jaman maybe uwe na watu wa karibu yako watakao guswa na hali uliyonayo wawe wanakupiga tafu mdogomdogo jamani.... Coz mahitaji ni mengi sana ya kitaaluma na kiafya namaanisha chakula mpaka inafikia hatua mtu unaona aibu kuomba hela nyumbani coz unahisi utaonekana tapeli..
Ninakuelewa, nafuatwa na wanafunzi, anakuambia sijala tangu jana usiku...nilikopa elf 2 ya chakula, kesho sijui...tayari wapo tumeanza kuchanga na wanasoma hata kama hazijatimia zitafika tu na wao waone nuru hii...Mungu atuone atuonekanie katika hili.
 
POINT! Kuna contradictions nyingi ambazo ufumbuzi wake utahitaji mawazo sahii ya wananchi na wadau kama Mama yetu mleta post. Issue,wataongelea wapi? Nani ataratibu? Na kwa ruhusa ya nani? Ninaona Mawaziri ndo wameachiwa na system kuamua kila kitu. Mfano, unasema Versity waende Div 1 na 2. Hao wote wametokana zaidi na shule za private ambao kwa vigezo hawatapewa mikopo. Ni watoto wa matajiri! Mama kaja JF,tumwunge mkono. Na naomba aunganishe wenye maono kama yeye Ulimwenguni kote,waunge mkono hoja yake.
Kuna wengi hapa Kenya jirani zetu,walisoma kwa michango" Harambee funds",na wakamaliza masomo,sasa wanajenga Taifa.
tutatekeleza chini ya mradi wa shirika linalohudumia vijana na wanawake. Kwa hiyo ni sehemu ya kazi za shirika kwa mwaka huu, japo wazo ni jipya, tuna imani litafanikiwa.
 
Shida ya hiyo approach mama, ni changamoto ya namna bora na effective ya kuweza kuestablish uwezo mdogo wa kiuchumi. Ni namna gani tuta define uwezo mdogo wa kiuchumi na tuta evaluate vipi. Changamoto hii wameendelea kukumbana nayo HESLB na kutokana na subjectivity ktk kuamua, watumishi wasio waaminifu wametumia kama namna ya kujipatia pesa kwa kupitia rushwa. Lakini, ikiwekwa kigezo cha ufaulu, basi awe mtoto wa masikini, awe mtoto wa tajiri, basi ajitahidi ili aweze kumeet kigezo cha kupata huo mkopo/ufadhili.
Asante Analyst, hiyo ni sehemu ya kazi yenyewe. Tukianza tutatemblea Bodi na kujifunza kutoka kwao ili tujue tunaonezaje thamani ya kazi yao. Hii ni kazi yetu wote.Bodi ina kazi ngumu pia, tutoe mchango wetu.
 
Ni Jambo zuri ila kama likipata taswira ya kisiasa tu litakwama
Mkaruka, tujiepushe na siasa zinazorudisha nyuma malengo ya maendeleo! Angalau katika suala la elimu ambalo linabeba taswira ya nchi na utu wetu, tukatae aina ya siasa hizo, la sivyo hakuna haja ya kuwa na siasa hizo pia. Nimeamua kuingia siasa kuchangia maendeleo. Kama siasa itanizuia kuchangia maendeleo, nitapata shida kuendelea nayo. hebu tuliangalie jambo hili kwa namna hii kwanza tuone.
 
Mshauri na mhemiwa magufuli awepo hapa apitie maoni ya wadau asiwaombe malaika wafunge mitandao ataambulia mazur huku jf.
 
Wanasema
Mama Anna;

Umetoa wazo zuri sana! Umetoa mwelekeo..!

Humu najua watu wataliunga mkono kwa maneno tuu na pongezi kwa wazo zuri..

Nilifikiri huu wito ungefanya event kabisa ili uliadress vizuri..either uitishe Press au kitu kama fundraising na kuwaalika watu wote walengwa..

Humu kuna members kama 400,000 hivi...bado tunataka ifike kwa watu zaidi hata watu 24milion ambao ni nusu ya Population yetu...

Ikiwezekana zihusishwe Taasisi tuu, watu binafsi na NGOs ! Serikali ikae pembeni manake wataleta siasa..! Hili suala wameshindwa kwa sababu watu wako after political gain..

Leo tukishindwa kusomesha hiki kizazi..miaka 50 ijayo hili taifa litapotea kabisa..

[HASHTAG]#Elimukwanza[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Uzalendokwanza[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Mikopo[/HASHTAG] elimu ya juu

Wanasema kuwa mabadiliko unayoyataka: Tuanzie hapo. Tufanye sehemu yetu. Kila mtu akitimiza wajibu wake kikamilifu, ataongeza nguvu ya safari. Mungu atusaidie.
 
Mama yangu umetoa wazo zuri,nachelea kusema watu wanaweza kuchukulia unataka kujijenga kisiasa na kumbuka ulikuwa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi.
Kumbuka serikali iliyopo madarakani ilisema watapewa mikopo wale tu waliosoma shule za serikali kwa maana ya kuwa waliosoma private wazazi wao wana uwezo!!!???
Uangalie usije kuwa unataka kuichonganisha serikali na wananchi wake maana tunatofautiana uelewa.
Ili kutoingia kwenye mgogoro,ningeshauri uanzie huko huko serikalini kwa kuwaomba wakukubarie wazo lako.
Naamini,watanzania wengi watakuunga mkono na si wanawake tu kama uluvyoainisha.
Watoto wamebaguliwa, kuna watoto wa watanzania na walipa kodi ndo wanafaidi kodi za wazazi wao!!!!
Hili huwa linatia hasira kama sio kusikitisha....
Hongera mama kwa kuja na hili wazo,simama nali,komaa nalo mpaka uone matunda yake.
Amina, asante, Tuanze
 
Ninawashukuru sana kwa maoni yenu endelevu. Nitakuja na mapendekezo yaliyoratibiwa ili kwa pamoja tuone tutakavyo sogea mbele na jambo hili. Mbarikiwe wote na usiku mwema.
 
Ninaikumbuka vema kauli ya mama Salma Kikwete kuwa nanukuu: " Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako." Leo watoto wa wenzetu wameingia tatizo la kukosa mikopo ya elimu ya juu; tuwasaidie kama watoto wetu.

Ninapenda kuwaomba akina mama wote nikianza na Mhe mama Salma Kikwete aliyeasisi usemi na hatua hii, tushirikiane kunusuru maisha ya elimu ya watoto walioko vyuoni wenye sifa ya kuwa na mikopo lakini hawakufanikiwa kupata mkopo. Tuwahamasishe vijana waliobakia mitaani na majumbani kujiunga na vyuo vikuu kuanua akili zao changa kukidhi ushindani wa sasa kimaisha.

Naomba akina mama wote viongozi, wazazi, walezi, wafanya bishara, waajiriwa, wanaharakati bila kujali itikadi zetu za aina yoyote tusimame kama wanawake wazazi wenye nia kuejnga taifa la watu walioelimika tuunde mfuko wa kuwasiadia watoto wetu wafanikiwe kumaliza masomo yao kwa ujenzi wa taifa letu.

Nikitoka na mama Kikwete ninaomba wake za marais wote waliopita kuanzia na mama Karume (mzee marehemu na Rais aliyemaliza mda wake) mpaka mama Janet Magufuli anayenivutia sana kwa kuonesha moyo wa amani sana kwa taifa letu.

Baada ya hao nimuombe mama Anna Makinda na wabunge wanawake wote waliopo na waliomaliza tangu uhuru wa nchi yetu tuungane kumsaidia kila mtoto wa Tanzania mwenye uwezo wa kusoma asome.

Kisha kwa niaba ya wanawake wafanya bishara niombe kitengo cha wanawake cha TCCIA, Baraza la Biashara la wanawake...tukubali wito huu: Tuungane kama wazazi na walezi chini ya kauli mbiu: Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako...tuunde mfuko wa elimu kwa ajili ya vijana wetu.

Niombe vyama vya wana-taaaluma: waalimu, madaktari, wahandisi, watumishi wa umma, mabenki, makampuni yote ya ndani na ya kigeni, asasi za kiraia za ndni na za kimataifa, balozi zetu zote, tuungane kuunda chombo hiki kuwasaidia vijana wetu.

Nimeguswa sana na mahangaiko ya vijana wa vyuo vikuu. Ninawashukuru wachache waliofika kwangu kueleza changamoto zao. Mmenihamasisha kuchangia kidogo elimu yenu lakini ninaomba hili liwe suala la kitaifa.

Ninaomba wanawake wenzangu popote tulipo tuwasiliane tuunde umoja huu kuwaimarisha na kuwapa tumaini vijana na janga la kukosa elimu ya juu kama wana sifa za kuipata.

Tuweke kando siasa, dini, kabila, ukanda ama aina yoyote ya kigezo kufanikisha jambo hili. Ninawashukru sana. Kesho kuna wanafunzi watashindwa kufanya mitihani kwa kukosa ada kidogo tu ya laki kuanzia 5-8. Mfuko wa mama Salma, Mfuko wa mama Mkapa wa Fursa sawa kwa wote, Taasisi ya Benjamini mkapa, Taasisi ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, na zingine, tusaidiane kukamilisha azima hii. Na mimi nimeanzisha Taasisi ya Mama Anna Mghwira kwa ajili ya kushughulikia masuala ya aina hii.

Nitawashukuru sana kwa niaba ya vijana wetu, tuenzi elimu yao kwa kuunganisha nguvu zetu hivi. Mnisamehe kwa kuandika mtandaoni. Nimejaribu njia za kawaida za simu sikufanikiwa sana. Hapa ninajua kila moja atapata taarifa. Mapungufu yangu yasizuie jambo hili kutendeka. Jinsi tulivyo changia madawati, sasatuchangie elimu ya juu.

Niombe wizara na Bodi ya mikopo ya wanafunzi kutoa ushirikiano tutakapouhitaji utaalamu muwe nasi bega kwa bega.

Mungu atubariki wote, aibariki Tanzania.

Asanteni tena, ni mimi mama Anna Mghwira
Mama kwanza nikusalimu shikamoo.pili niseme asante kwa kuliona hili na kulipa nguvu, kweli wanafunzi tunapata shida sana. Kwa mfano Mimi ni yatima sina wazazi wote na attachment ninazo, ila nimeomba mkopo nimekosa, nimeappeal pia nimekosa. Nimekwenda kuongea na Mkuu wa idara ya matangazo bodi ya mikopo lakn hakunisaidia. Na hii no kutokana sina MTU wa kunisaidia yaan kutia Maji bilikan pindi yachemkapo. Nimekwenda kwa Mkuu wa mkoa, nimekutana na wasaidizi wake lakn hawakunipa ushirikiano. Naomba mama nipe no yako ya simu nikutafute nije kuongea na ww. 0674010013
 
Back
Top Bottom