Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa mikopo ya elimu ya juu na tuchukue hatua

Anna Mghwira

Verified Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
203
Points
500

Anna Mghwira

Verified Member
Joined Mar 9, 2012
203 500
Ninaikumbuka vema kauli ya mama Salma Kikwete kuwa nanukuu: " Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako." Leo watoto wa wenzetu wameingia tatizo la kukosa mikopo ya elimu ya juu; tuwasaidie kama watoto wetu.

Ninapenda kuwaomba akina mama wote nikianza na Mhe mama Salma Kikwete aliyeasisi usemi na hatua hii, tushirikiane kunusuru maisha ya elimu ya watoto walioko vyuoni wenye sifa ya kuwa na mikopo lakini hawakufanikiwa kupata mkopo. Tuwahamasishe vijana waliobakia mitaani na majumbani kujiunga na vyuo vikuu kuanua akili zao changa kukidhi ushindani wa sasa kimaisha.

Naomba akina mama wote viongozi, wazazi, walezi, wafanya bishara, waajiriwa, wanaharakati bila kujali itikadi zetu za aina yoyote tusimame kama wanawake wazazi wenye nia kuejnga taifa la watu walioelimika tuunde mfuko wa kuwasiadia watoto wetu wafanikiwe kumaliza masomo yao kwa ujenzi wa taifa letu.

Nikitoka na mama Kikwete ninaomba wake za marais wote waliopita kuanzia na mama Karume (mzee marehemu na Rais aliyemaliza mda wake) mpaka mama Janet Magufuli anayenivutia sana kwa kuonesha moyo wa amani sana kwa taifa letu.

Baada ya hao nimuombe mama Anna Makinda na wabunge wanawake wote waliopo na waliomaliza tangu uhuru wa nchi yetu tuungane kumsaidia kila mtoto wa Tanzania mwenye uwezo wa kusoma asome.

Kisha kwa niaba ya wanawake wafanya bishara niombe kitengo cha wanawake cha TCCIA, Baraza la Biashara la wanawake...tukubali wito huu: Tuungane kama wazazi na walezi chini ya kauli mbiu: Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako...tuunde mfuko wa elimu kwa ajili ya vijana wetu.

Niombe vyama vya wana-taaaluma: waalimu, madaktari, wahandisi, watumishi wa umma, mabenki, makampuni yote ya ndani na ya kigeni, asasi za kiraia za ndni na za kimataifa, balozi zetu zote, tuungane kuunda chombo hiki kuwasaidia vijana wetu.

Nimeguswa sana na mahangaiko ya vijana wa vyuo vikuu. Ninawashukuru wachache waliofika kwangu kueleza changamoto zao. Mmenihamasisha kuchangia kidogo elimu yenu lakini ninaomba hili liwe suala la kitaifa.

Ninaomba wanawake wenzangu popote tulipo tuwasiliane tuunde umoja huu kuwaimarisha na kuwapa tumaini vijana na janga la kukosa elimu ya juu kama wana sifa za kuipata.

Tuweke kando siasa, dini, kabila, ukanda ama aina yoyote ya kigezo kufanikisha jambo hili. Ninawashukru sana. Kesho kuna wanafunzi watashindwa kufanya mitihani kwa kukosa ada kidogo tu ya laki kuanzia 5-8. Mfuko wa mama Salma, Mfuko wa mama Mkapa wa Fursa sawa kwa wote, Taasisi ya Benjamini mkapa, Taasisi ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, na zingine, tusaidiane kukamilisha azima hii. Na mimi nimeanzisha Taasisi ya Mama Anna Mghwira kwa ajili ya kushughulikia masuala ya aina hii.

Nitawashukuru sana kwa niaba ya vijana wetu, tuenzi elimu yao kwa kuunganisha nguvu zetu hivi. Mnisamehe kwa kuandika mtandaoni. Nimejaribu njia za kawaida za simu sikufanikiwa sana. Hapa ninajua kila moja atapata taarifa. Mapungufu yangu yasizuie jambo hili kutendeka. Jinsi tulivyo changia madawati, sasatuchangie elimu ya juu.

Niombe wizara na Bodi ya mikopo ya wanafunzi kutoa ushirikiano tutakapouhitaji utaalamu muwe nasi bega kwa bega.

Mungu atubariki wote, aibariki Tanzania.

Asanteni tena, ni mimi mama Anna Mghwira
 
S31

Member
Joined
Mar 15, 2018
Messages
40
Points
95

S31

Member
Joined Mar 15, 2018
40 95
Mama kesha kuwa ccm tayari zile akili alizokuwa nazo awali hazipo tena siku hizi kapandikizwa akili mpya na akina polepole,msukuma na kibajaji,atakujarudiwa na akili zake original atakapotumbuliwa
We ndo umenena kwan walikuwa wanashangilia Anna Mgwira kuhamia chama tawala afu Leo wanamtaka apaze sauti mdanganyeni wamtumbue hahahahahahahahahahahahahah
 
Transcend

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Messages
19,806
Points
2,000

Transcend

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2015
19,806 2,000
Kwani huyu si ndo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. mbona ni kama analalamika chakula kibaya wakati wapishi anakaa nao jikoni!!!???
Kipindi anaandika huu uzi alikuwa amevaa miwani yenye clear glass Hivyo aliweza kuona mbali.

Sasa hivi mama haoni tena mbali kwa kuwa amevaa miwani mieusi.
 
john issa

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2017
Messages
257
Points
250

john issa

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2017
257 250
Kweli tungepata viongozi wa aina hii katika nchi hii sijui tungefika wapi.

Tungekuwa mbaaali mno na pengine tungehama kutoka dunia hii ya tatu kwa kweli

Wengine nao wapo tu kujinufaisha wao katika ngazi zao

Jamani akina mama bila kujali itikadi yoyote ya vyama vyenu au chochote unganeni kulikomboa taifa,

Kuna shamba na kuna mbegu lakini mpandaji kakosa
Miaka ijayo tutakosa mavunobya wataalam na wajuvi mbalimbali hapo ndipo tutaanza kutafutana wapi tumekosea.

Leo vijana wengi wapo mtaani na si hivyo wwngine hawajui hatma yao aseee ungeni mkono hilo
 
kishanda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
252
Points
195

kishanda

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2012
252 195
Ninaikumbuka vema kauli ya mama Salma Kikwete kuwa nanukuu: " Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako." Leo watoto wa wenzetu wameingia tatizo la kukosa mikopo ya elimu ya juu; tuwasaidie kama watoto wetu.

Ninapenda kuwaomba akina mama wote nikianza na Mhe mama Salma Kikwete aliyeasisi usemi na hatua hii, tushirikiane kunusuru maisha ya elimu ya watoto walioko vyuoni wenye sifa ya kuwa na mikopo lakini hawakufanikiwa kupata mkopo. Tuwahamasishe vijana waliobakia mitaani na majumbani kujiunga na vyuo vikuu kuanua akili zao changa kukidhi ushindani wa sasa kimaisha.

Naomba akina mama wote viongozi, wazazi, walezi, wafanya bishara, waajiriwa, wanaharakati bila kujali itikadi zetu za aina yoyote tusimame kama wanawake wazazi wenye nia kuejnga taifa la watu walioelimika tuunde mfuko wa kuwasiadia watoto wetu wafanikiwe kumaliza masomo yao kwa ujenzi wa taifa letu.

Nikitoka na mama Kikwete ninaomba wake za marais wote waliopita kuanzia na mama Karume (mzee marehemu na Rais aliyemaliza mda wake) mpaka mama Janet Magufuli anayenivutia sana kwa kuonesha moyo wa amani sana kwa taifa letu.

Baada ya hao nimuombe mama Anna Makinda na wabunge wanawake wote waliopo na waliomaliza tangu uhuru wa nchi yetu tuungane kumsaidia kila mtoto wa Tanzania mwenye uwezo wa kusoma asome.

Kisha kwa niaba ya wanawake wafanya bishara niombe kitengo cha wanawake cha TCCIA, Baraza la Biashara la wanawake...tukubali wito huu: Tuungane kama wazazi na walezi chini ya kauli mbiu: Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako...tuunde mfuko wa elimu kwa ajili ya vijana wetu.

Niombe vyama vya wana-taaaluma: waalimu, madaktari, wahandisi, watumishi wa umma, mabenki, makampuni yote ya ndani na ya kigeni, asasi za kiraia za ndni na za kimataifa, balozi zetu zote, tuungane kuunda chombo hiki kuwasaidia vijana wetu.

Nimeguswa sana na mahangaiko ya vijana wa vyuo vikuu. Ninawashukuru wachache waliofika kwangu kueleza changamoto zao. Mmenihamasisha kuchangia kidogo elimu yenu lakini ninaomba hili liwe suala la kitaifa.

Ninaomba wanawake wenzangu popote tulipo tuwasiliane tuunde umoja huu kuwaimarisha na kuwapa tumaini vijana na janga la kukosa elimu ya juu kama wana sifa za kuipata.

Tuweke kando siasa, dini, kabila, ukanda ama aina yoyote ya kigezo kufanikisha jambo hili. Ninawashukru sana. Kesho kuna wanafunzi watashindwa kufanya mitihani kwa kukosa ada kidogo tu ya laki kuanzia 5-8. Mfuko wa mama Salma, Mfuko wa mama Mkapa wa Fursa sawa kwa wote, Taasisi ya Benjamini mkapa, Taasisi ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, na zingine, tusaidiane kukamilisha azima hii. Na mimi nimeanzisha Taasisi ya Mama Anna Mghwira kwa ajili ya kushughulikia masuala ya aina hii.

Nitawashukuru sana kwa niaba ya vijana wetu, tuenzi elimu yao kwa kuunganisha nguvu zetu hivi. Mnisamehe kwa kuandika mtandaoni. Nimejaribu njia za kawaida za simu sikufanikiwa sana. Hapa ninajua kila moja atapata taarifa. Mapungufu yangu yasizuie jambo hili kutendeka. Jinsi tulivyo changia madawati, sasatuchangie elimu ya juu.

Niombe wizara na Bodi ya mikopo ya wanafunzi kutoa ushirikiano tutakapouhitaji utaalamu muwe nasi bega kwa bega.

Mungu atubariki wote, aibariki Tanzania.

Asanteni tena, ni mimi mama Anna Mghwira
Mama asante maana hiyo itasaidia kuipunguzia serikali mzigo kwa asilimia fulani Mimi nipotayari kuchangia tukihamasishana tutajikomboa watoto wanalia .wakati wazazi wanawasomesha shule za kulipia walikuwa na kazi za kuajiriwa au kufanya bishara ndogondogo sasa aidha wamestafu au uzeee magonjwa ya umri yaani kipindi ambacho wanastahiri msaada sasa msaada hakuna .tufanye harambeee watoto wetu wafikie malengo yao .Mungu akubariki mama ukifanisha hili tutakukumbuka daima .
 
koro-boy

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2017
Messages
344
Points
250

koro-boy

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2017
344 250
Loan Board inafanya nini mbona inabagua Watanzania, eti mzazi akiwa hata na leseni tu mwanae hapati mkopo, mtoto kasoma private school hapati mkopo. Mwishowe mtasema akitoka mkoa fulani asipewe mkopo kwao wamesoma sana. Itaenda itakuja kwenye ajira Mkoa flani asiajiriwe mkoa wao umeendelea sana. Ubaguzi hautaishia hapo. Mkoa huu wasifugungue tena shule mpya wanashule nyingi sana zinatosha. wasijengewe Hospital za Wilaya za misson zinatosha wameendelea sana. Mama mkuu wa Mkoa ubaguzi huu unauona?
 
Mama hebu pigania basi Mji wako wa Moshi upate hadhi ya Jiji hata uache legacy hapo Moshi.
 
Forum statistics

Threads 1,380,699
Members 525,851
Posts 33,776,938
Top