Anna Makinda: Sijawahi kuolewa ila tunakoenda wanawake watakuwa na nguvu kuliko waume zao

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Anne Makinda ameelezea historia yake fupi ya maisha toka enzi anasoma hadi kuja kufanikiwa kuwa kiongozi mkubwa bungeni.


Mhe. Anne Makinda
Mhe. Makinda amesema maisha yake yote yalikuwa bungeni na kipindi hicho amesema kuwa alikuwa na fujo sana kuliko hizi ambazo zinafanywa na baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani bungeni.

“Mimi maisha yangu yote yalikuwa bungeni, mimi mwenyewe kama kuwa mtu wa fujo i was of those.. nilikuwaga backbencher nilikuwa na fujo nawambia ndugu zangu akina Tundu Lissu kuwa kwanza nyie hamuwezi kunifikia mimi,“amesema Anna Makinda.

Akielezea upande wa mahusiano Bi. Makinda amesema yeye hakuwahi kubahatika kuolewa na amewaasa wanawake waliokwenye ndoa kuwa makini sana pale wanapopata mafanikio kwani ndio kipindi cha kushirikiana karibu sana na wanaume zao ili kufika mbali.

“Mimi sikuwahi kuolewa lakini nilipopata mtoto wangu, aliyenisaidia sana ni dada yangu. Kwa hiyo nikiwa shuleni tu IDM nikipata ile shilingi 20 kumi napeleka kwa dada, 10 nabaki nazo kwa hiyo toka huko nilikuwa nafanya kazi I have to survive .“amesema Bi. Makinda na kusisitiza jambo kwa wanawake walioolewa.

“Tunakokwenda najua kabisa akina mama watakuwa na nguvu zaidi kuliko akina baba, na ndio maana nawa-advice pia tujifunze kuwapenda hawa watu. Kwa sababu kama wewe ni Couple umeolewa halafu unakuwa successful kuliko mume wako, usipoweza kumeneji hiyo anaweza kukuharibia hata wewe, ni vizuri kumshirikisha ikawa ile successful yako ikawa ni part ya familia yako au successful ya couple yenu,“amesema Anne Makinda akielezea historia yake kwenye mahojiano na TGNP Mtandao


Mhe. Anne Makinda ndiye mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na alishawahi kuhudumu pia kwenye shirika la UNICEF .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akiwa Binti mdogo Sana nami nikiwa kijana Barobaro hasa nilikuwa namkuta pale Tanzania Audit Corporation it was katikati ya 1970s

Anna alikuwa Anna Kweli Ila alikuwa anasuka ( twende kilioni style)Sio kuvaa Yale makofia ya nywele
 
Ngoja nianze na ishu ya msingi.

Fujo zake bungeni anazifananisha vipi na hoja za mtu kama Tundu Lissu?. Bunge ni uwanja wa hoja sio fujo. Hapa tulipo ni matokeo ya Fujo za wana CCM bungeni.

Pili,
Sijaona hoja yake kwa kauli ya wanawake kuwa na nguvu kuliko kina baba huko mbeleni, hii ni kauli ya fujo fujo tu haina mantiki.

Ushauri.
Fujo hazina maana kwenye jamii.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom