Anna Makinda: Siasa ni wakati wa uchaguzi tu, vinginevyo wananchi mtakufa masikini

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Jana niliwona ktk TV Spika Anne Makinda akiwa jimboni kwake akihutubia wananchi kwa kuwaambia kwamba waache mambo ya kushabikia siasa ama sivyo watakua masikini. Alisema siasa zinapaswa kufanywa wakati wa uchaguzi tu - yaani kila baada ya miaka mitano basi.

Miaka mingine kusiwepo siasa ama sivyo watakufa masikini. Nina hakika kuna wengine walimsikia vizuri Zaidi kwani mie nilimuona ktk TV kidogo tu akiwa anamalizia hotuba yake.

Swali: anaogopa nini kuwepo jukwa la siasa jimboni mwake hadi kuwatisha na kuwadanganya wananchi wake?
 
Maisha ya siku hadi siku yamegubikwa na siasa. Maisha ni sehemu ya siasa.

Sent from my GT-I9100 using Tapatalk
 
Huyu mama nashindwa kumwelewa bosi wake ndani ya chama aliwaambia wananchi kipindi cha kampeni wasichague vyama vya msimu yaani vyama vinavyo fanya siasa kipindi kampeni tu sasa vimeanza kufanya siasa kipindi chote wanaanza kujiharishia,yeye sihana mpinzani alipita bila kupingwa atulie tuone yeyesianaogopwa jimboni kwake mpaka hapati mpnzani sasa atulie aone.
 
Hii ndiyo tabu ya kuwa na viongozi mambumbumbu. Makinda anajua siasa ni nini au akili yake imezama kwenye posho? Pengine nimkumbushe maneno ya Baba wa Taifa kuwa ili taifa liendelee linahitaji vitu vikuu: Watu, Siasa safi na Uongozi bora.

sukari ni siasa, bei ya mafuta ya taa ni siasa, mabomu ya Gongo la Mboto ni siasa, umeme ni siasa, mbolea ni siasa, power tiller ni siasa! Sasa Makinda anataka wananchi waachane ni nini hasa?
 
Wananchi Jimboni kwake Njombe Kusini hata kama Hawashabikii siasa Mbona ni Masikini tu, ameshindwa kuwapa wananchi wake Maji Safi na Salama, Wananchi wanalazimishwa kuchangia Ujenzi wa Madarasa na kutengeneza Madawati sasa anaongelea kuhusu siasa. Namwakikishia Makinda, 2015 lazima Chama kingine Kichukue Jimbo.
 
Huyu hana uelewa wowote kuhusu nini hasa maana ya siasa. Hana visheni kabisa. Hawa ndio watu system yetu imewabeba miaka nenda rudi katika nafasi muhimu za uongozi halafu tunategemea kusonga mbele!
 
Back
Top Bottom