ANNA MAKINDA ametumwa kutupoteza maboya watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ANNA MAKINDA ametumwa kutupoteza maboya watanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Dec 15, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hili la utata wa sakata la posho za wabunge napata wasiwasi kuwa ni njama ya kutufumba akili zetu na kutupoteza maboya watanzania ili tusahau suala nyeti la mchakato wa kutungwa kwa katiba mpya. Suala muhimu ambalo ghafla limesahaulika baada ya kuzimwa na mada iliyozuka kuhusu ongezeko tata la posho za wabunge. Hapa kuna kitu, huyu huyu spika ndiye aliyeuburuza muswada wa sheria ya mchakato wa katiba mpya kiasi cha kuzua mtafaruku mkubwa. Wakati bado watanzania wakiendelea kuhoji juu ya kiini macho kile, kachomeka suala la posho akijua mambo yanayohusu maslahi hugonga vichwa vya watu. Sasa wananchi wamechanganyikiwa, masikio na macho yetu yameelekea huko. Suala la katiba mpya halipo tena. Chondechonde mama Anna jaribu kupunguza kasi yako, usije ukaingia kwenye mtaro. Kama unatumiwa kutupoteza maboya ili mpate mwanya wa kutuletea katiba inayolinda maslahi yenu! Tumeanza kuwashitukia... Sisi sio wadanganyika tena, ni watanzania halisi. Usijaribu kutukata stimu yetu ya mchakato wa katiba mpya.
   
Loading...